Mbona Majanga

Mbona Majanga

Majangaaa Mbona Majangaaa! - 26-

ILIPOISHIA JUMAMOSI…
Tabu aliogopa sana, kwa kuwa alikuwa amebadilika na macho yake yamekuwa mekundu, mwili wake ulikuwa umechoka kama aliyekuwa ametoka kubeba mizigo mizito.

“Tabu,” Pat alisimmama na kumwita.“Abee,” aliitikia.
“Una nini?” aliuliza Pat ambaye alikuwa amejawa na udadisi baada ya kumuona Tabu akiwa katika hali tofauti.
SASA POROMOKA NAYO…

Hata hivyo, Tabu hakutaka kuendelea kumsikiliza Pat, alijifanya kama vile hakumwelewa, ingawaje alishajua kwamba udadisi wa msichana huyo ulikuwa umebaini kitu fulani.
Moja kwa moja Tabu akaamua kuingia katika chumba alichokuwa akilala na wasichana wengine huku akijitahidi kumkwepa Pat.
“Tabu… Tabu… Tabuu…,” aliendelea kuita Pat bila ya mafanikio. Pamoja na kuona kwamba hakuitikiwa, Pat hakukata tamaa akaingia chumbani humo.
Alipoingia akamkuta Tabu akiwa amejitupa kitandani, akamwita tena na tena lakini Tabu alijikausha kimya kama vile alikuwa hamsikii.
“Wee Tabu unaumwa au…?”
Bila ya kugeuka na kumwangalia, Tabu akiitikia kwa kichwa kukubali kwamba alikuwa anaumwa kwa kuwa alishaona Pat alikuwa amemsaidia kumtafutia jibu la kumpa.
“Nini kinakusumbua?”
“Tumbo…” alijibu swali hilo huku mikono yake akiwa ameiviringisha kwenye tumbo lake kuonesha kwamba lilikuwa likimsumbua.
“Pole sana… lakini Tabu mbona nguo yako imejikunja? Na hata nywele zako zimevurugika halafu nimekuona ukitokea katika chumba cha Eddy?” alihoji Pat.
“Haaa hamna kitu…” alijibu Tabu huku akigeuka na kujiweka sawa nywele zake na kujaribu kuikunjua nguo yake iliyokuwa imejikunja.
“Hamna kitu, haiwezekani… kuna kitu… tena angalia macho yako yamekuwa mekundu, hebu niambie ulikuwa ukifanya nini chumbani kwa Eddy?” Pat aliendelea kumkomalia Tabu.
Tayari kengele ya hatari ilikuwa imeshagonga akilini mwa Pat, akahisi kuwa Tabu alikuwa ametoka kugonga shoo na Eddy.
“Kwani wewe unafikiria nini?” alijibu Tabu kwa swali huku akisimama.
“Hee yamekuwa hayo tena… kwani tumbo limepona, hebu niambie basi ulikuwa ukifanya nini chumbani kwa Eddy?” Pat alizidi kumdodosa Tabu.
“Hayakuhusu… kila mtu ana mambo yake, kwa nini unapenda kufuatilia mambo ya watu?”
“Mambo gani niliyofuatilia?”
“Si haya ya kuniuliza kwamba nimetoka kufanya nini chumbabi kwa Eddy kwani wewe unafikiria nimetoka kufanya nini? Mbona miye sijakuuliza huko ulikotoka umetoka wapi?” alisema Tabu kwa hasira.
“Wee niambie tu umetoka kufanya nini?”
“Kumpelekea chakula…?”
“Chakula gani?”
“Kwani wee unajua kuna chakula gani na gani? Nakuomba uelewe kwamba nimetoka kumpelekea chakula…” alisisitiza Tabu.
“Samahani kama nimefuatilia mambo yako, lakini kumpelekea chakula tu ndiyo nguo yako ikunjikekunjike na macho yako yawe mekundu…?”
“Kwani wewe unataka nini, nishakwambia kuwa nimetoka kumpelekea chakula kwa nini huelewi?”
“Kweli umempelekea chakula maana una kila dalili kwamba umepeleka chakula chenye ladha ya nyama ya binaadamu… lakini ole wako dada Queen na Rehema wajue kama umempelekea chakula hicho chenye ladha ya nyama ya binaadamu,” alisema.
“Watafanifanya nini…?”
“Ngoja wajue ndiyo utajua watakufanya nini, wee si unajifanya mwanamke kweli…?”
“Ndiyo mimi ni mwanamke kweli… nina kila kitu ambacho wao wanacho na ninaweza kufanya chochote kile ambacho wao wanaweza kufanya…” alisema Tabu kwa hasira.
“Sawasawa, nimekuelewa…” alisema Pat huku akitoka nje akiwa amehisi kwamba pamoja na Tabu kudai kwamba alikuwa amempelekea chakula Eddy lakini kulikuwa na zaidi ya chakula alipoingia chumbani kwake.
Tabu akarudi kitandani na kujipumzisha kutokana na kile alichokuwa amekifanya na Eddy, huku akiwa na wasiwasi kwamba Pat anaweza kwenda kusambaza maneno hayo kwa watu wengine.
“Shauri yake, kama anataka kwenda kusema mwache aseme… kwani ana ushahidi gani?” alijifariji.
Mara baada ya kutoka nje, Pat akagongana na Eddy akiwa anatoka chumbani kwake, akamwangalia kwa udadisi na kujiuliza mwanaume huyo ana nini mpaka anawapanga foleni wasichana wa nyumba hiyo.
“Shikamoo?” akatoa salamu.
“Marhaba…” Eddy akaitikia huku akifunga mlango wake kuashiria kuwa alikuwa akitoka na kwenda mbali na eneo hilo.
Pamoja na kusalimiana Pat aliendelea kumkodolea macho Eddy kama vile ndiyo kwanza alikuwa akimuona.
Kitendo hicho kilimshangaza Eddy na kujiuliza, kwa nini msichana huyo alikuwa akimwangalia kwa umakini kiasi hicho.
“Vipi mbona unaniangalia hivyo?”
“Aaah, nilikuwa nakuangalia tu,” alijibu Pat huku akiona aibu kwa jinsi alivyoshtukiwa na Eddy.
“Sema unataka tutoke wote nini?”
“Walaaa!” alijibu huku akiumauma vidole vyake vya miongoni.
Eddy alitoka zake huku akimwacha Pat pale ukumbini akiendelea kumwangalia kwa udadisi. Moyoni mwake Pat aliamini kwamba kijana huyo alikuwa na kitu cha ziada kwa wasichana.
“Kwanza mchangamfu halafu amekaa vizuri…” aliwaza moyoni mwake huku akiwa anasumbuliwa na kutaka kujua kama kweli Tabu alikuwa amegonga naye shoo.
Baada ya kutafakari kwa muda, Pat akatoka na kuamua kumfuata tena Tabu chumbani ili kwenda kumuuliza kama kweli alikuwa amevunja amri ya uzinzi na Eddy.

Je, Pat atakapomuuliza Tabu kama alicheza shoo na Eddy atakubali? Usikose kufuatilia utamu huu Jumapili ijayo...
 
[h=1]Majangaaa Mbona Majangaaa! - 27-[/h]
ILIPOISHIA …
Eddy alitoka zake huku akimwacha Pat pale ukumbini akiendelea kumwangalia kwa udadisi. Moyoni mwake Pat aliamini kwamba kijana huyo alikuwa na kitu cha ziada kwa wasichana.

"Kwanza mchangamfu halafu amekaa vizuri…" aliwaza huku akiwa anasumbuka kutaka kujua kama kweli Tabu alikuwa amegonga naye shoo.
Baada ya kutafakari kwa muda, Pat aliamua kumfuata tena Tabu chumbani ili kumuuliza kama kweli alikuwa amevunja amri ya uzinzi na Eddy.
SASA POROMOKA NAYO…

Alipoingia chumbani akamkuta Tabu akiwa bado amelala, akaanza kumwamsha kwa upole tofauti na mwanzo alivyoingia chumbani humo kwa mara ya kwanza na kumwamsha kwa ukali.
Mbali na kufanya hivyo, awali alikuwa akimlazimisha Tabu kuhusu ishu ya kugonga shoo na Eddy, safari hii ilikuwa tofauti.
Tabu alipoamka, Pat akaanza kumuuliza kwa upole ili aweze kujua ukweli, moyoni wivu ulikuwa ukimtafuna kwa kuhisi kuwa amepigwa bao na msichana mwenzake.
"Shoga hebu tuache utani mimi na wewe ni marafiki wa muda mrefu, hebu niambie kile ulichokifanya na Eddy chumbani kwake…" alianza kwa kumbembeleza.
"Wee si umesema unaenda kuwaambia dada Rehema na Queen? Nenda tu miye wala sina wasiwasi…"
"Hebu tuachane na hayo, miye na wewe ni damu damu, yale yamepita shoga'angu maana nimekutana na huyu mwanaume hapo ukumbini, wee acha tu…"
"Unamaanisha nini kwani na wewe unamtaka?"
"Hivi katika akili yako kuna mwanamke ambaye anaweza kukataa kuwa na mwanaume kama yule?" Pat alijibu kwa kuuliza swali.
"Mh! Makubwa."
"Madogo yana nafuu shoga, hebu niambie basi kama mwenzangu umeshawahi?" alichombeza Tabu.
Tabu hakuweza kumjibu Pat akabaki akicheka na kumfanya Pat kuendelea kuhisi kwamba kulikuwa na ukweli kwa kile alichokuwa akikifikiria ndani ya nafsi yake, hata hivyo hakutaka kujiridhisha kwa hisia tu, akataka kuambiwa ukweli na mhusika.
Akaendelea kumuuliza Tabu ili amwambie kwa mdomo wake kile kilichojiri.
Baada ya kutafakari kwa kina, Tabu akaona hakukuwa na haja ya kumficha, akaamua kumwambia Pat kile kilichojiri chumbani kwa Eddy.
"Yaani shoga wee acha tu," akaanza kusema huku akijiinua kutoka kitandani na kukaa.
"Mh! Lete habari…" Pat alichombeza huku naye akijiweka sawa kwa ajili ya kupata ukweli kamili.
"Yule mwanamme sijui hata ana nini… maana ghafla tu nilijikuta nikimtamani… lakini alifanya kosa moja tu, alianza kunidharau… pale aliponiambia kwamba miye ni mtoto mpaka nilipomhakikishia kwamba miye ni mkubwa mwenziwe…"
"Kweli…?" alihoji Pat na kumfanya Tabu kuendelea kuhadithia kile kilichotokea kati yake ya Eddy…
"Nilipomhakikishia hivyo, akanifuata pale nilipokuwa nimesimama, ilikuwa ni katikati ya chumba na kunipeleka kwenye uwanja wa fundi seremala.
"Hapo akapitisha mikono yake kwenye nywele zangu na kuzichambua kwa vidole vyake, kisha akachora ramani mwilini mwangu kwa kutumia mikono yake na kunisisimua vya kutosha.
"Kisha akaanza kutumia silaha ya nyoka…" Tabu alisema na kukatishwa na Pat.
"Silaha ya nyoka ndiyo nini Tabu mbona unaniacha kama kishada kinachokwenda halijojo…?"

"Aaah aaah kumbe nilikuwa nakuacha…, pole shoga'angu si unajua inanibidi nitumie lugha ya tafsida, basi namaanisha ile silaha anayoitumia nyoka akitaka kutema sumu yake.""
"Hapo nimekupata ni ulimi…" alisema Pat.
"Yesii, ulimi wake ulipita nyuma kidogo ya shingo yangu na kuzidi kunipandishwa wazimu… nilikuwa nasikia raha kama vile natambaliwa na sisimizi shingoni," aliendelea Tabu na kumfanya Pat kukaa vizuri ili kupata uhondo zaidi.
"Baada ya hapo akawa anasafiri na ulimi wake kwa kupita kila sehemu aliyoiona inafaa, sehemu ya kuweka kituo kwa muda aliweka na kuendeleza utundu wake.
"Kisha akahamia kwenye embe sindano zangu, akawa anazivuta kwa ndani na kisha kuzitoa nje kwa kutumia njia yake ya kupitishia chakula, weee acha tu… wazimu si wazimu raha si raha, sijui hata nikwambieje…"
"Mh!"
"Alipotoka hapo alipitisha silaha ya nyoka katika maeneo mengine nyeti kwenye maungo yangu na kunifanya nizidi kumchemka kwa hisia kali, akafika hadi kwenye kile kitu ambacho mara baada ya mtoto kuzaliwa baada ya muda huwa kinakatika chenyewe…"
"Nini hicho?"
"Kwani wee hujawahi kusikia kuanguka kwa kitovu cha mtoto…?"
"Aaah nimewahi kusikia shoga…" aliitikia Pat.
"Basi alipofika hapo, mashetani yalitaka kunipanda… nilitamani hata kupiga kelele ili anichie au nipate msaada wa kusaidiwa maana aliniweza kwelikweli…"
"Wee acha utani…" Pat alihoji.
"Kweli vile…" alisisitiza Tabu.
"Mh! Basi makubwa," Pat aliguna.
Mwili ulinitoka vipele kama vile nilikuwa nikitambaliwa na sisimizi au nilikuwa nikitaka kuugua ugonjwa wa malaria. Alipotosheka akapitiliza hadi kwenye bastola zangu…"
"Halafu… ikawaje…" Pat alijawa na udadisi wa kina wa kutaka kujua kile kilichoendelea.
"Hapo kwenye bastola zangu hakukaa sana, akaenda moja kwa moja kumsalimia bibi kule shambani."
"Acha utani…?"
"Kweli vile, yule kijana ana heshima kwelikweli… kwani alipofika kwa bibi aliamua kumwamkia kwa heshima zote, alipiga magoti na kumsalimia kwa kuzungumza naye kwa kinywa chake… huku silaha yake ikiwa ni ileile anayoitumia nyoka."
"Aiseee…" Pat aliropoka bila ya kujijua na kumfanya Tabu ageuke na kumwangalia.
" Hapo ndipo nilipoanza kusikia kizunguzungu kama siyo kichinachina… nilisi kama vile nataka kukata roho, kuna wakati nilifikiria kama vile sikuwa duniani… kweli dada Rehema na Queen walikuwa wanafaidi…
"Mh! Endelea basi akawa anafanyaje…? Pat alikuwa akitaka kujua uhondo huo aliokuwa akisimuliwa na Tabu jinsi ulivyonoga.
"Wee acha mwanaume pale yupo, alipomaliza kumsalimia bibi wakati huo miye nusu nilikuwa duniani na nusu nilikuwa peponi, nilikuwa kama vile niko ndotoni…"
"Aisee ulifaidi…" Pat alisema.
"Si kidogo, lakini mchezo kamili ulikuwa kwenye shoo yenyewe maana hiyo yote ilikuwa ni kama rasharasha vile vumbi lenyewe lilitimka pale alipoingiza kisu kwenye ala ndipo nilipochoka… kweli nilijiona ni mtoto…," alisema Tabu.
"Kwa nini," Pat aliendelea kuhoji.
"Kisu chake kilipoingia kwenye ala nilisikia kama vile mawimbi ya maji yakipiga kisimani, kali mawimbi yenyewe yalikuwa yanafanana na yale ya baharini lakini hayo yalikuwa kama yana mvutano wa umeme, aah Pat wee acha nilipiga kelele," alisema Tabu.
"Kwa hiyo umemvulia kofia…?"
"Si kidogo hapa unaponiona niko hoi, ulipokuwa ukinisemesha muda ule nilikuwa nakuona kama vile ulikuwa unanizungua tu…" alisema Tabu.
"Kumbe?"
"Eeeh wee acha tu, Eddy anajua kuizungusha funguo katika kufuli kwelikweli…" alisisitiza Tabu na kumfanya Pat kuanza kupatwa na hamu ya kile alichokuwa akifanyiwa mwenzake.


Nini kiliendelea? Usikose kufuatilia siku ya Alkhamisi ijayo.....
 
Nimependa hilo neno la utam unakuja utam unakata!

si unaona utam ukija utam ukikata lazima uanze tenna kuvuta stimu toka mwanzo bhana!!!!
ndo mana napenda uguswapo penyewe pagusweee weee hadi climax.........
sasa MziziMkavu anagusa anaacha, anagusa anaacha kweli anatenda haki kwa siye wapate utam??
 
Last edited by a moderator:
Majanga Mbona Majangaaa! -28-


ILIPOISHIA ...................
"Kwa hiyo umemvulia kofia…?"
"Si kidogo hapa unaponiona niko hoi, ulipokuwa ukinisemesha muda ule nilikuwa nakuona kama vile ulikuwa unanizingua tu…" alisema Tabu.
"Kumbe?"
"Eeeh wee acha tu, Eddy anajua kuizungusha funguo katika kufuli kwelikweli…" alisisitiza Tabu na kumfanya Pat kuanza kupatwa na hamu ya kile alichokuwa akifanyiwa mwenzake.
POROMOKA NAYO…



Mpaka kufikia hapo, Pat alikuwa amesha-lowanisha kila nguo iliyokuwa katika maungo yake. Kijasho chembamba kilikuwa kikimvuja kutokana na kile alichokuwa akihadithiwa na Tabu.

Binti huyo naye alikuwa hajiwezi tena, hali yake ilikuwa mbaya akatoka na kwenda msalani ili kujiweka sawa.
Hilo lilitokana na Pat kupagawisha na kile alichokuwa akihadithiwa na Tabu jinsi alivyopiga shoo na Eddy mawazo yake aliyachukua na kujiona kama vile yeye ndiye aliyekuwa msambweni akigonga shoo na mwanaume huyo.
Alifikiria kama kuhadithiwa tu amedata je akikutana na mwanaume huyo itakuwaje? Akaweka wazo kwamba na yeye lazima agonge bonge la shoo na kijana huyo.
Alikuwa amechanganyikiwa kabisa, akajuta kuchelewa kukutana na Eddy, alitamani angekuwa wa kwanza kukutana na mwanaume huyo kabla ya Tabu, Queen na Rehema.
Moyoni alihisi kwamba wenzake hao walikuwa wamefaidi kwelikweli.
Baada ya muda Pat alirejea tena chumbani kwa Tabu na kuanza kuzungumza na msichana huyo na kumwambia msimamo wake kutokana na kile alichokisikia.
"Tabu ndugu yangu, kitu kizuri kula na nduguyo, kuna haja ya miye kupiga shoo na Eddy," alisema Pat na kumfanya Tabu amshangae.
"Yaani kukuhadithia kidogo tu umedata na unataka kuchonga mzinga, je ningekupa kila kitu ingekuwaje?"
"Kwa hiyo hicho ulichonihadithia ni kidogo? Basi nitamtafuta Eddy anipe kikubwa zaidi maana naona wewe unataka kunibania," alisema Pat.
"Siyo hivyo, kwanza utaanzaje kumwingia kijana wa watu, kwani unajua kama anakutaka au hakutaki? Nakushangaa sana shoga'angu."
"Nitajua cha kufanya wala hilo lisikupe shida ninachotaka ni kumtia mikononi mwangu, iwe kwa kujitongozesha au kwa kunitongoza yeye mwenyewe," alisema Pat kwa kujiamini.
"Miye sitakuwa na tatizo kwa kuwa miye mwenyewe ni mwizi tu, tatizo ni kwa Rehema na Queen wakijua umekwisha, utahama humu ndani…" Tabu alimtisha.
"Kwa hiyo wewe ushajipanga kuhama?"
"Utajuaje?" Tabu alijibu kwa swali na kufanya Pat kuzidi kuchanganyikiwa kama asuke au anyoe.

***
Wakati Pat akiwa na mawazo ya kumwingia Eddy ili aweze kupata kile ambacho roho yake inataka, wakati huo mama mwenye nyumba alikuwa chumbani kwake, alikuwa amemwita mwanaye Mwamvita kwa ajili ya maongezi muhimu.
Mama huyo alikuwa amesubiri muda huo kwa kuwa mumewe ambaye ni baba mwenye nyumba hiyo hakuwepo, alikuwa ameenda kucheza bao nyumba ya jirani.
"Mwamvita mwanangu hivi utakuja kuolewa kweli wewe…?"
"Kwa nini unasema hivyo mama?"
"Nakuona umejikalia tu wakati wenzio wanachangamkia tenda…" alisema mama mwenye nyumba bila ya kufafanua na kumfanya mwanaye atawaliwe na maswali.
"Bado sijakuelewa mama, unamaanisha nini?"
"Utanielewa tu, unaona wenzio wanavyomchangamkia mgeni wewe umejikalia tu huna mbele wala nyuma."
"Mama unamaanisha kwamba unataka na mimi nimgombee huyu mgeni aliyehamia humu ndani?"
"Siyo umgombee, unatakiwa umchukue kabisa na kummiliki awe wako kabisakabisa…" mama mwenye nyumba alisema.
"Hai mamaaa…"
"Ndiyo hivyo, nataka uache kuhangaika na vibwana vyako uchwara, unatakiwa kuwa na mwanaume kama yule ambaye anaweza hata kuleta kilo ya sukari nyumbani… siyo kile kijamaa chako kinachoitwa Beka… mpaka leo sijakula hata senti yake…" alisema mama mwenye nyumba.
"Mama achana na Beka, sasa hivi niko na Peter ambaye tayari umeshakula pesa yake, kwanza hata Beka umeshakula hela yake, sema umesahau tu…?"
"Labda unikumbushe, lakini hata kama nimekula… ni lini alileta hata nusu kilo ya sukari humu ndani wakati unajua kabisa maisha yetu ni ya mkandamkanda…?" aliendelea kuhoji mama huyo.
"Hilo halijafanyika si kwa kuwa bado hawajanioa… mmoja wao akinioa atafanya hivyo unavyotaka," alijibu Mwamvita.
"Mmoja wapo akinioa atafanya…," alisema mama mwenye nyumba huku akimwigiza mwanaye kisha kumwambia:
"Utabaki hivyohivyo, mwanaume yuko humu ndani wewe unahangaika na hao wahuni, wanakuchezea kama ganda la mua."
"Mama lakini sasa unafika mbali…"
"Sifiki mbali, siku hizi mwanangu watu wanaangalia uwezo wa mwanaume… siyo mapenzi, siye zamani ndiyo tulikuwa tukijali mapenzi, hatima yetu si unaiona?"
"Lakini mama unasema kweli, inaonekana enzi zako ulikuwa unamtii baba kwelikweli…"
"Nakushangaaa wewe una kila kitu halafu unakubali kuchezewa sijui na Beka sijui na nani… shauri yako… mwanaume yuko humuhumu ndani…"
"Sasa unanishauri nifanyeje?" Mwamvita alimuuliza mama yake huku akionekana kuanza kukubaliana na ushauri aliopewa.
"Hilo ndilo jibu, kwani mkoleni tulikupeleka kufanya nini?"
"Akishaingia kwenye kumi na nane, nitajua cha kufanya lakini kabla ya hapo ndiyo nashindwa kwa kuwa namuona yuko na Queen na Rehema…?"
"Usiwe na shaka, wewe jilengeshe na siku zote nataka kukwambia kitu kimoja, mwanaume hana ujanja kwa mwanamke…"
"Ndiyo nifanyeje sasa?" Mwamvita aliendelea kuhoji huku akiwa ameweka masikio yake wazi kuweza kupata elimu hiyo kutoka kwa mama yake.


Je, nini kiliendelea kati ya mama huyo na mwanaye? Fuatilia Jumapili ijayo.......Musikonde ndio Utamu wake huo
 
Majangaa Mbona Majangaa - 29-


ILIPOISHIA JUMATANO…
“Lakini wakati mwingine mama huwa unaona mbali…” alisema Mwamvita akionekana kukubaliana na mawazo ya mama yake. “Msaada mkubwa nitakupa… ukimnasa tu, nitakwambia cha kufanya kisha tutaenda kwa yule mtaalamu wa kule Tandale…” alisema mama mwenye nyumba. “Tukamroge…?” Mwamvita alitahamaki na kuhoji. “Wee mtoto sijui unaishi dunia gani, hivi mpaka leo unadhani mambo huwa yanakwenda hivihivi…?” “Sasa ndiyo mpaka tukamroge?” “Shauri yako, humu ndani kuna mambo ya ajabu kama hujui wee kaa hivyohivyo kama hujazeekea hapahapa, unatoka chumba kile unahamia kile…”
POROMOKA NAYO…

“Dah… kwa hiyo natakiwa kufanya nini mama?” “Unaniuliza miye? N’shakwambia kila kitu…” alisema mama mwenye nyumba huku akiinuka na kupangusa makalio yake na kuondoka akimuacha mwanaye Mwamvita.

“Sijui nifanye nini?” aliwaza Mwamvita huku akianza kutafakari kauli za mama yake. Kauli ambayo ilimsumbua kichwa ni ile ya kumwambia “Humu ndani kuna mambo ya ajabu kama hujui wee kaa hivyohivyo.” “Ina aana hata akina Rehema na Queen wamemroga Eddy? Kama ni hivyo hii si itakuwa vita kubwa!” Baada ya kutafakari kwa muda akaona hakuwa na njia nyingine zaidi ya kujiingiza katika vita ya kumwania mwanaume huyo.
Alijua alikuwa na upinzani na watu wiwili tu, Queen na Rehema, hakuwa akijua kama Tabu na Pat nao walikuwa ni washindani wengine wasiojulikana. Usiku wa siku hiyo Mwamvita akaanza pilikapilika za kumnasa Eddy. Hakutaka watu wengine wajue lakini aliamini kuwa anaweza kuwaambia mashoga zake wawili tu juu ya mpango huo. Mashoga zake hao hawakuwa wengine zaidi ya Pat na Tabu, aliwaamini sana marafiki zake hao kwa kuwa walikuwa ni rika lake na kwamba hawakuwa na ndoto za kuwa na Eddy.
Wakati akipiga hesabu hizo, Pat naye alikuwa akipiga hesabu zake za kumnasa mwanaume huyo, Tabu hali kadhalika alikuwa akiwaza jinsi atakavyoweza kumdhibiti mwanaume huyo asiweze kuangukia katika mikono ya Pat. Kama vile haitoshi, vita ya Rehema na Queen ilikuwa palepale kama wapinzani wakuu wa mchakato huo wa kumwania Eddy.
***
Siku hiyo, Queen alijitahidi hadi akaonana na Eddy uso kwa uso, alichokifanya ni kumuwahi maeneo ya nje ya nyumba hiyo, yaani alikwenda kumfanyia ‘taimingi’ kituoni kabla ya mwanaume huyo hajafika nyumbani na wakazungumza kwa kina. “Sasa pale imeshakuwa balaa, miye naonekana nimeingilia penzi la Rehema,” alisema Queen. “Sasa tufanyeje?” alihoji Eddy. “ Hakuna cha kufanya, ila wewe endelea na mwanamke wako.. miye niache..” “Haiwezekani…” Eddy alisisitiza. “Haiwezekani kwa nini… unajua hata miye nina bwana wangu, lakini nilimweka pembeni kwa sababu yako…” “Kwa hiyo unataka kuniambia nini?” “Nataka kukukwambia kwamba wewe endelea na mwanamke wako na miye niendelee na bwana wangu…” “Halafu miye na wewe?”
“Ndiyo inakuwa adiosi amigo tena…” “Haiwezekani…” alisema tena Eddy. “Miye sioni ugumu wa hilo au ukitaka… lakini hapana ni heri kila mmoja awe na mpango wake.” “Ulikuwa ukitaka kusema nini kwani?” “Nilitaka kusema wewe uwe na mwanamke wako na miye niwe na bwana wangu na tuendelee na uhusiano wetu kwa siri, wewe huruhusiwi kuleta mwanamke mwingine mle ndani na miye siruhusiwi kuleta mwanaume mwingine zaidi ya huyo bwana wangu…” “Halafu miye na wewe tutakuwa tunaduu wapi?” “Nje ya nyumba ile, tukiwa pale kila mmoja akimuona mwenzake ni heshima na adabu kwa kwenda mbele…”
“Utaweza kuvumilia kuniona na Rehema tukitanua?” “Kimpango wako, ila tu asiwepo mwanamke mwingine zaidi ya Rehema, sawa?” “Sawa, nawe usiwe na mwanaume mwingine zaidi ya huyo bwana wako, kwanza sijui hata anaitwa nani? “Muddy…” “Oke, nawe usiwe na bwana mwingine zaidi ya huyo Muddy, sawa?” “Sawa,” alisema Rehema. Wakakubaliana na kila mmoja akarudi katika nyumba wanayoishi akiwa ameridhika na makubaliano yao ambayo waliamua kuyafanya kuwa siri.
***
Eddy aliingia chumbani na kubadilisha nguo, kisha akatoka na kwenda zake msalani kwa lengo la kujisaidia na kisha akaingia bafuni kwa ajili ya kujimwagia maji. Akachota maji yake katika ndoo na kuingia nayo bafuni, akiwa huko akaanza kuoga huku akiwa na raha akiamini kuwa makubaliano yake na Queen yalikuwa ya msingi sana. Akiwa ameshajimwagia makopo kadhaa ya maji na kujipaka sabuni usoni alihisi kitu kikimnyemelea, akashtuka na kuwahi kunawa maji usoni. Alipofumbua macho alishangaa kumuona Pat akiwa bafuni humo. Kwa sauti ya upole huku akihangaika kulitafuta taulo lake ili ajihifadhi akamuuuliza:
“Wewe Pat umefuata nini humu?” “Nimekufuata wewe…” Pat alimjibu akiwa haoneshi wasiwasi wowote kama alikuwa amefanya kitu kibaya. Ndiyo kwanza alikuwa akijiandaa kusaula viwalo vyake ili ajumuike na Eddy katika kuoga. Eddy akavuta kumbukumbu ya mchana wa siku hiyo mara baada ya kutoka kula raha na Tabu, akakumbuka jinsi binti huyo alivyokuwa akimwangalia. “Haya sasa majanga!” akawaza na kushangazwa jinsi ambavyo wasichana wa nyumba hiyo walivyokuwa wanakubali kujitoa sadaka kwake. “Umenifuata kufanya nini?” Eddy alingong’ona tena.

Itaendelea Alkhamisi ijayo.........
 
Back
Top Bottom