Mbona Majanga

Mbona Majanga

Hapa mpaka mama mwenye nyumba apate!Na si jamaa hatumii ile mifuko ya plastik basi wote nyumba nzima mimba na ngoma juu!Chezea Eddy wewe! MziziMkavu,mwanangu katu simuiti Eddy,majina mengine majanga!
 
Last edited by a moderator:
Majangaa mbona majangaa-33-


ILIPOISHIA
Rehema alitoka hadi barazani kumtafuta Eddy lakini hakumuona, akafika hadi chumbani kwake lakini pia hakumuona ingawaje aliona dalili za mwanaume huyo kurudi.
Ishara kubwa aliyoiona ni taa ya chumbani kwa Eddy ambayo ilikuwa ikiwaka na kuashiria kwamba alikuwepo, Rehema akatoka hadi uwani na kuangaza huku na kule ili kujiridhisha kwamba labda mwanaume huyo alikuwa ametoka na kwenda msalani.
Akaangaza huku na kule lakini hakumuona Eddy, akasimama hapo na kujiuliza mwanaume huyo alikuwa amekwenda wapi.
Akiwa anatafakari nini cha kufanya, akajisikia haja ya kwenda msalani.
POROMOKA NAYO…


Rehema akawa anaelekea msalani lakini akilini mwake alikuwa akiwaza ni wapi Eddy alipokuwa. Alikuwa na kiu kubwa ya kumuona mwanaume huyu ili amwambie kuhusu Queen kuleta mwanaume mwingine ndani ya nyumba hiyo.

Rehema alihisi kwamba, Eddy akijua kwamba Queen ambaye ndiye mpinzani wake pekee ndani ya nyumba hiyo akimuona mwanaume wa msichana huyo ataamua kuachana naye na yeye atabaki kuwa peke yake.
Akionekana kuwa na mawazo mengi, Rehema alipiga hatua kuelekea msalani, ghafla mbele yake akamuona msichana akitoka msalani.
Kwa kuwa giza lilikuwa limetanda hakuweza kumfahamu kwa haraka, akasimama ili aweze kupishana naye.
Aliposogea, aliweza kumtambua kuwa ni Pat aliyekuwa akitokea upande wa bafuni. Hata hivyo hakuweza kusalimiana naye kwa kuwa alimuona kama adui yake kwa kuwa alikuwa ni mdogo wa Queen.
Rehema akasita kwenda msalani kwa kuingiwa na hofu ukizingitia msalani kwao hakukuwa na taa, akiwa amesimama kwa muda bila ya kuamua cha kufanya mbele yake tena akamuona mtu mwingine akija usawa wake.
Akamwangalia kwa umakini kutaka kumjua kama alikuwa Eddy au nani… alipokaza macho yake vizuri akamtambua kuwa aliyekuwa akitokea kule alikuwa ni msichana.
"Weee nani…?" alimuuliza.
"Mwamvita…"
"Aaaah kumbe wewe…" alisema Rehema na hofu kumtoka kidogo.
Maneno yao yalisikika kwa Eddy aliyekuwa amebaki bafuni kwa kuwa walikuwa wamepanga kwamba awe mtu wa mwisho kutoka bafuni humo baada ya wasichana hao wawili kutoka.
Hata hivyo, Rehema alipatwa na wasiwasi kuona Pat na Mwamvita wakiwa wanatokea bafuni muda huo na kujiuliza kulikoni wawili hao watoke bafuni kwa wakati mmoja.
Aliyaondoa mawazo ya kuwafikiria vibaya na hisia zake zikamwambia kwamba labda walikuwa wakioga pamoja baada ya mmoja wao kuogopa kuoga peke yake.
"Mwamvita…!" aliita Rehema.
"Abee!"
"Nisubiri hapa wakati nikiingia msalani… si unajua kuwa kunatisha kwa kuwa hakuna taa…"
"Sawa…" aliitikia Mwamvita huku moyoni kiroho kikimdunda.
Kwa uwepo wa Mwamvita pale nje, Rehema aliweza kuelekea msalani na alipoingia msalani aliiachia haja ndogo karibu kabisa na mlango.
Akiwa anaendelea kujihudumia alihisi kama kuna mtu amepita kutokea bafuni, awali alihisi ni uoga wake lakini akili yake ikamwambia kuwa kuna mtu ametoka bafuni tena kwa kunyata.
Hakumuona mtu huyo ila hisia zake ndizo zilizomtuma kuamini hivyo, akaziamini ingawaje hakuweza kuacha kumalizia jukumu lililompeleka msalani humo na kumfuatilia mtu huyo.
Alijua tu Mwamvita atamwambia ni nani aliyetoka bafuni kwa kuwa alikuwa amepanga kumuuliza mara baada ya kutoka msalani.
Baada ya kumaliza haja yake akatoka lakini alipofika nje hakumkuta Mwamvita wala kivuli chake.
Akajiuliza kama msichana huyo alikuwa amemdharau au kulikuwa na kitu kinachoendelea ambacho kilimfanya asimsubiri kama alivyomtaka.
"Kama amefanya makusudi atakuwa akimjua mtu aliyetoka bafuni…" aliwaza Rehema akapanga kumfuata Mwamvita na kumuuliza kwa nini aliondoka bila ya kumsubiri.
Rehema akapata wasiwasi mkubwa ndani ya nafsi yake bila ya kujua kile kilichotokea.
Akiwa na wasiwasi wake akaamua kurudi ndani, cha kwanza kumshangaza alipofika usawa wa chumba cha Eddy ni dalili za kuwepo kwa mtu ndani ya chumba hicho.
Aliziona kandambili za mwanaume huyo zilizokuwa zimelowana maji, wasiwasi wake ukaongezeka na kuhisi kwamba huenda Eddy ndiye aliyekuwa mtu wa tatu kutoka bafuni.
Hakutaka kuamini hilo pamoja na kwamba hakutaka kumchukulia dhamana mwanaume huyo, akaamua kugongea mlango ili aweze kuonana naye na ikiwezekana amuulize kabla ya kumvaa Mwamvita.
Eddy alipatwa na wasiwasi pale aliposikia mikono ya kike ikiugonga mlango wake, akawa anajiuliza ni nani.

Kwanza alihisi labda ni mmoja kati ya wale wasichana aliokuwa nao bafuni ndiye aliyekuwa akigonga wake muda huo.
Pili, akahisi kwamba mgongaji angeweza kuwa ni Queen lakini akaliondoa wazo hilo baada ya kukumbuka makubaliano yake na msichana huyo kwamba wasiwasiliane wanapokuwa ndani ya nyumba hiyo.
Tatu akamfikiria Rehema kwamba, angeweza kuwa ni yeye kwa kuwa hakuwa ameonana naye usiku huo.
Hata hivyo, hakutaka kujipa usumbufu wa akili kwa muda mrefu, akaamua kuusogelea mlango na kuufungua.
Macho yake yakagongana na Rehema, haraka akayakwepesha na kuangalia pembeni, kisha akarudi chumbani kwake na kuendelea kufanya kile alichokuwa akikifanya.
Rehema aliingia chumbani humo na moja kwa moja akamsogelea Eddy na kumkumbatia kwa nyuma akipitisha mikono yake kiunoni kwa mwanaume huyo kisha akamwita:
"Baby…!"
"Eeeh!" Eddy aliitikia bila ya kuonesha uchangamfu uliokuwa umezoeleka kati yao.
"Una nini?"
"Sina kitu," alijitetea Eddy huku akitaka kuvaa bukta yake ya kulalia.
"Hauko kawaida, kuna nini hebu niambie…?" Rehema aliendelea kusema katika hali ya kuonesha kwamba alikuwa akitaka kupata undani wa kile kitu alichokuwa akikitaka.
"N'shakwambia kwamba hakuna kitu…" alisema Eddy kwa ukali kidogo.
Rehema hakukubali akamgeuza Eddy upande wake na kuwafanya waangaliane, kisha akamzuia kuvaa bukta, akamsogeza hadi kwenye uwanja wa fundi seremala.
Bila ya Eddy kutarajia, akiwa amesimama huku akiangaliana na Rehema, msichana huyo akamsukuma kidogo na kumwangusha Eddy juu ya uwanja huo.
Kabla ya Eddy hatajatafakari kitendo cha kuangushiwa dimbani, Rehema akampandia juu yake na kulala juu ya kifua chake na kuhakikisha kwamba nyuso zao zinagusana na macho yao yanaangaliana.
"Nimekutafuta kwa muda mrefu ulikuwa wapi?" Rehema alisema kwa sauti ya upole iliyojaa kila aina ya bashasha za mahaba.
"Nilikuwepo…" Eddy alipoa kidogo
"Wapi?" alisisitiza Rehema na hapohapo akafanya kitu ambacho Eddy hakukitarajia.
Rehema akaushusha mkono wake hadi kwenye ikulu ya Eddy na kugusa msumari.
"Kha! Kwa nini iko hivi?"
"Kwani ikoje?" alisema Eddy huku akitaka kujiondoa chini ya udhibiti wa msichana huyu, kwani alishajua kwamba mambo yatakuwa makubwa kama akiendelea kujilegeza.
"Mbona siku zote haiwagi hivi…?"
"Ikoje?" Eddy aliendelea kuhoji akimtaka Rehema amwambie anahisi msumari wake umekuwaje.
Bado unataka kujua kilichotokea? Usikose kufuatilia jumapili ijayo
 
Sijaona. Ila Eddy asipokufa na ngoma sijui. Kijana kiwembe mno!!!

Ila labda kwa kua anajua kuviandaa vya kutosha tu vibinti vyake kabla ya game kuanza, may be "liquid" inakuwepo ya kutosha kulainisha maeneo na kuzuia uwezekano wa michubuano.
 
Huu uzii haufai kusoma ukiwa public maana unaweza aibika hasa dushelele akikasirika...heheheheee majanga eddy ni nouma....
 
Back
Top Bottom