Mbona Majanga

Mbona Majanga

Majangaaa Mbona Majangaaa! - 34-

"Hujui?"
"Sijui…" alijibu Eddy
"Mbona inaonekana kama vile umetoka kufanya kazi muda si mrefu?"
"Sikuelewi…" alijitetea Eddy.
"Unaonekana kama vile ulikuwa bafuni…"

"Ndiyo…"
"Lakini mbona nimewaona yule mtoto wa mwenye nyumba na Pat nao wakitoka bafuni?"
"Miye nilitoka kabla yao," alijitetea Eddy.
"Siyo kweli… miye nilitoka kukuangalia barazani hukuwepo, nikaja chumbani kwako, hukuwepo…nikaenda uani ndipo nilipowaona wao wakitoka kisha nikahisi mtu akitoka bafuni, nadhani ulikuwa wewe…" alisema Rehema.

Moja kwa moja Eddy akatengeneza picha kichwani mwake, akaamini kwamba mwanamke huyo alikuwa sahihi katika maongezi yake.
Lakini siku zote Eddy alikuwa amejifunza kitu kimoja tu, kukataa kitu chochote ambacho kingeweza kumfanya mtu amfikirie vibaya.

"Sasa kama umewaona wao wananihusu nini mimi?"
"Siyo kukuhusu, inawezekana ulikuwa nao bafuni…"
"Umenichoka sasa…" alisema Eddy huku akionesha hasira usoni mwake na kutoka katika mikono ya Rehema, akasimama na kuvaa bukta yake.

Ilimbidi kufanya hivyo ili kuweza kukwepa kuingia msambweni na Rehema kwa kuwa alihisi msichana huyo hakuwa na lingine zaidi ya wivu na kutaka kutimiziwa jambo hilo.
Aidha Eddy alifikiria kwamba asingekuwa na nguvu za kupiga naye shoo kwa kuwa muda mchache alikuwa ametoka kugonga shoo za nguvu.
"Sasa unaenda wapi?" Rehema aliuliza kwa jazba.

"Nitakaaje na wewe ambaye unanihisi vibaya hata kwa vitoto vinavyonuka haja ndogo?"
"Siyo hivyo, nilikuwa nikihisi tu kutokana na mazingira na wewe hujaniambia ulikuwa wapi mpenzi wangu…" Rehema alianza kupunguza wasiwasi wake.
"Sawa ndiyo unihisi na vile vitoto?"
"Basi rudi nikwambie kitu kingine."

"Kuhusu nini?"
"Kuhusu Queen, roho ya Eddy ikashtuka na kutaka kujua kuhusiana na msichana huyo.
"Kafanya nini?"
"Nilijua lazima hilo hutataka kulisikia tu."

"Tatizo lako wewe wivu umejaa, unanihisi kila mtu ni halali yangu… ndiyo maana unaniudhi," Eddy alitengeneza ndita za uongo usoni mwake.
"Basi usikasirike, ni kwamba Queen amekuja na mwanaume wake… wako chumbani kwao…"
"Mimi inanihusu nini?"
"Si mpenzi wako?"

"Mpenzi wa nani? Miye sijawahi hata siku moja kutoka na Queen wewe mawazo yako yanakutuma vibaya," alisema Eddy na kutoka nje.
Moja kwa moja, Eddy alitoka hadi barazani na kuwakuta Muddy na Queen wakiwa huku baada ya kutoka chumbani kwa msichana huyo.

Queen alipomuona Eddy akafurahi na kuona ni sehemu ya kuweza kuweka mambo yake sawa, akamwita na kumtambulisha kwa Muddy.
"Huyu ni shemejio anaitwa Eddy ni mgeni hapa nyumbani kwetu, anakaa chumba kile cha mwisho..." Queen alitoa utambulisho huo mfupi.

"Sawasawa nimefurahi kukufahamu bwana Eddy…" alisema Muddy.
"Na huyu ni Muddy, ni mpenzi wangu wa muda mrefu sana, hapa katikati alipotea kutokana na kuzuzuliwa na wasichana wa mjini," Rehema alimtambulisha Muddy kwa Eddy.
"Sawasawa, nami nimefurahi kukufahamu bwana Muddy karibu sana kwetu… ndiyo tumeanza maisha…" alihitimisha Eddy huku akishikana mkono na Muddy.

Wakati hayo yakiendelea Rehema alishatoka ndani na kushuhudia utambulisho huo.
Akabaki akishangaa na kujiuliza maswali mengi kama kweli Queen hajawahi kutembea na Eddy.
Siyo yeye peke yake, hata Pat, Mwamvita na Tabu nao walikuwa barazani hapo wakishuhudia kitendo hicho.

Wote walibaki midomo wazi, wakashangaa kwa nini Eddy anakubali kutambulishwa kwa mwanaume mwenzake.
Wote hao walikuwa na uhakika wa asilimia mia kwamba Eddy alishatembea na Queen, Pat mdogo wake Queen alijua hivyo, Mwamvita alijua hivyo na hata Tabu alilijua hilo.

Mbali na kujua hivyo, wote walikuwa wakijua kwamba tayari walishatembea na mwanaume huyo, maswali yakawavagaa akilini mwao na kushindwa kupata jibu.
Walikuwa wakijiuliza kwamba, Eddy alikuwa akikubali kutoka moyoni au alikuwa akiigiza?

Pamoja na Rehema naye kujua kwamba aliingia katika ugomvi na Queen kwa sababu ya Eddy lakini kidogo alifarijika na kuamini kuwa mwanaume huyo alikuwa mkweli.
Hakuona sababu ya kumhisi Eddy vibaya, aliamini kwamba kama Eddy angekuwa ametembea na Queen asingekubali kutambulishwa kwa mwanaume mwenzake.

Hapohapo Rehema akawa mpole, akafuta mawazo yote mabaya juu ya Eddy.
Akahisi hata kuhusu wale watoto, Pat na Mwamvita zilikuwa ni hisia zake tu.
Akapanga kuondoa tofauti zake na Queen huku akidhamiria kumuomba msamaha kwa ugomvi wao wa siku za nyuma.
"Eddy…" Rehema hakutaka kulaza damu hapohapo akamwita mwanaume huyo.
"Unasemaje?"

"Twende ndani tukaongee," alisema Rehema huku akimvutia ndani mwanaume huyo. Bila kinyongo Eddy akamfuata kama vile mbwa anavyomfuata chatu.
Kitendo hicho kilimfurahisha sana Queen kwa kuona kuwa ameweza kuwahadaa wote waliokuwa wakimfikiria vibaya juu ya Eddy, akatoka kumsindikiza jamaa yake.
"Samahani mpenzi wangu?" Rehema alijikuta akisema mara baada ya kuingia chumbani na Eddy.

"Samahani ya nini?"
"Kwa jinsi nilivyokuwa nikikufikiria vibaya, naomba unisamehe juu ya Queen..-."
"Ni hilo tu?" Eddy alihoji
"Na mengine yote nayo naomba unisamehe…" Rehema alijikuta akiwa mtumwa ghafla wa kufuta mawazo yake na kusadiki mawazo ya mtu mwingine.

"Na kuhusu Queen?" Eddy alisema huku akimkazia macho Rehema.
"Hata yeye niko radhi kumuomba msamaha pia…" alisisitiza.

Nini kiliendelea? Usikose kusoma Jumatatu.
 
Sijawahi kuona story kama hii kwakweli. Hivi mtunzi ni nani? Iko kimajanga majanga. Bongo movie wako wapi waigize hii aisee? Story kali sana
 
Majanga Mbona Majangaaa! -35-


ILIPOISHIA RISASI JUMAMOSI
"Wala sikijui, hebu nipe utamu shoga…"
"Si nimemkuta Pat na mgeni wakiwa wanakula uroda?"
"Mhhh! Pat au unamsingizia?" alihoji Tabu.

"Nimsingizie kwa nini?"
"Si anajua kama Queen amekula uroda na mgeni kwa hiyo ameamua kula chungu kimoja na dada'ke?"
POROMOKA NAYO…

"Sijui kitu gani kimemfika…?"
"Hebu nipe mchapo ilikuwaje..?" Tabu alitaka kujua zaidi.
"Nilikuwa natoka bafuni, ghafla nikasikia kelele za kimahabati zikirindima upande wa kutokea bafuni… si nikazifuatilia?"
"Enheee…" Tabu akachombeza kutaka kujua zaidi huku roho ikimuuma kwa kuwa alikumbuka kwamba na yeye alikuwa ameshakula uroda na mgeni.

Pia, akakumbuka jinsi Pat alivyomhisi siku alipokuwa akitoka chumbani kwa Eddy, ndani ya nafsi yake akasema kumbe msichana huyo aliamua kumfuatilia Eddy na kwenda kula naye raha bafuni.
"Basi kila nilivyokuwa nikisogea ndivyo kelele zilivyokuwa zikiongezeka…, acha mchezo Pat akiwa mchezoni anajua kulalamika shoga," alisema Mwamvita kumsifia mwanamke mwenzake.

"Mwanzo nilidhani nilihisi kuna mtu alikuwa akinyongwa nikazama hadi bafuni… nikamkuta Pat kaandika namba saba na mgeni kaandika namba moja nyuma yake…"
"Weee…" Tabu alishtuka.
"Ndiyo nakwambia…"
"Enhee, ukafanyaje au wakafanyaje?" alihoji huku akikaa vizuri.

"Nikawaangalia kwa muda kisha nikawashtua, baada ya hapo wote wakanywea na kama vile walikuwa wamelowana na mvua…"
"Mh ikawawaje?" ushawishi ukamzidi Tabu.
"Pat alikuwa akitaka kujifanya mjanja kwa kujitetea, nikaona isiwe tabu, kwa kuwa jogoo la mgeni lilikuwa limeshanywea, nikaingia mzigoni na kuanza kulipandisha ili liweze kufanya kazi….

"Mtoto wa kike nikachukua usukani na kuanza kumpekecha mgeni ili kumpandisha mori upya, Pat akashangaa, kitu kilipokuwa sawasawa, nikampisha ili aendelee na starehe zake…"
"Na wewe ulitoka nje au ulibaki mle bafuni?"
"Niende wapi wakati miye ndiye niliyekuwa kocha mwenyewe tena…nikakaa na kuangalia mapigo yao."
"Tobaaa!" alisema Tabu huku akiushangaa uamuzi huo wa Mwamvita.

"Sasa unashangaa nini…?"
"Miye nisingeweza kupiga shoo huku mwanamke mwenzangu akiwa ananiangalia…" Tabu alisema na kuongeza " Hebu niambie lakini hadi mwisho ikawaje?"
"Ulitaka iweje, alipomaliza raundi yake moja na miye nikaingia kwenye gemu… nikamuonesha jinsi ya kupiga shoo kiutu uzima," alisema Mwamvita na kuzidi kumshangaza Tabu.

"Ina maana na wewe ukapiga shoo?" Tabu alisema huku akitaka ufafanuzi kutoka kwa Mwavita kwa kuwa alikuwa hajamuelewa kile alichokuwa akikimaanisha. "Unasema?"
"Sirudii kwa kuwa miye sitangazaji matangozo ya vifo shoga…" alisema kwa utani Mwamvita huku macho yake yakiwa makavu.
" Hivi ulichosema ni kweli au nimekusikia vibaya?" Tabu aliendelea kudadisi.
"Naamini kabisa kwamba masikio yako hayana matatizo, yako sawasawa, utakuwa umenisikia vizuri…"

"Kwamba baada ya Pat kumaliza na wewe ukachukua nafasi yake…?"
"Ndiyo maana yake…" alisema Mwamvita.
Ghafla baada ya kauli hiyo, Tabu akaonekana kukosa raha na kuonesha kama vile hakuwa amependezwa na maneno yake yale lakini Mwamvita akaendelea kushusha mistari yake:

"Basi nikagonga shoo ya nguvu…" Mwamvita alikuwa akiendelea kumwadithia Tabu lakini msichana huyo aligundua tofauti iliyokuwepo wakati walipokuwa wakianza mazungumzo yao na hadi hapo walipofikia.
"Vipi mbona kama vile umekatika stimu gafla, kuna kitu kimekugusa nini…? Maana nakuona huna raha na umekuwa mpole ghafla…?"

"Kuna kitu nataka nikuambie…" Tabu alisema na kuonekana dhahiri kwama alikuwa ameguswa na kitu ambacho hakikumpendeza.
"Kitu gani hicho, Kinahusiana na mambo haya niliyokuadithia au una lingine shoga?"
"Kuhusiana na huyohuyo mgeni…" alisema Tabu kisha kumeza funda la mate.

"Haya mwaga mtama shoga… isiwe na wewe umeshagonga naye shoo?" Mwamvita alisema huku akijiweka sawa na yeye kusikia kile alichokuwa akitaka kukisema Tabu.
"Unajua…" Tabu alianza.
"Sijui…" Mwamvita alimdakia na kumkazia macho kwa umakini mkubwa.

"Acha utani shoga nataka kukuambia kitu cha maana sana maana naiona hatari mbele yetu…"
"Sijakuelewa…" Mwamvita alisema.
"Unajua kama Queen ametembea na mgeni…?"
"najua…" Mwamvita alisema.

"Unajua tena kama Rehema ametembea na mgeni?"
"Hata hilo hakuna asiyejulia, kwa maana hata sasa wako msambweni…" alijibu Mwamvita kwa kujiamini.
" Hapa unaniambia kuwa Pat ametembea na mgeni…?"
"Siyo Pat peke yake na miye vilevile nilikuwepo na nikashiriki katika tendo lao…" alisema Mwamvita.

"Haya sasa na miye nimetembea na huyo mgeni…" alisema Tabu na kumfanya Tabu kuachama mdomo bila ya kusema kitu kwa muda mrefu.
"Na wewe tayari…?"
"Ndiyo maana yake," alijibu Tabu kwa unyonge kama mtu aliyekata tamaa.

"Haya sasa Majanga…" alijibu Mwamvita.
"Siyo Majanga tu, ni zaidi ya Majanga… hivi unadhani mmoja wetu akiwa ameathirika hapa inakuwaje, si wote tutaondoka na ugonjwa huu wa Ukimwi?" alihoji Tabu.
"Katika siku zote leo ndiyo umeongea jambo la msingi, sasa tutafanyaje?"

"Hebu tumwite Pat hapa kisha tupange mkakati wa kuweza kuchukua hatua zaidi…" alipendekeza Tabu.
Mwamvita alisimama na kwenda kumwita Pat ili waweze kumweleza kuhusiana na mkakati ambao wanaweza kuupanga kutokana na kuchanganywa na mwanaume huyo.

"Eeeh mnasemaje?" Pat aliuliza baada ya kuitikia wito huo.
Mwamvita akachukua jukumu la kumwambia ukweli wa kile kilichotokea.


Unadhani ni nini kiliendelea? Usikose kusoma jumatatu
 
Back
Top Bottom