Mbeya: Jeshi la Polisi lawanasa watu wawili wakiwa na noti Bandia za Sh 10,000

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya katika kipindi cha kuanzia Novemba 01, 2023 hadi Novemba 11, 2023 limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 34 kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo mauaji, utoroshaji madini, wahamiaji haramu, wavunjaji na watengenezaji na wasambazaji wa noti bandia.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na kikosi kazi cha kudhibiti utoroshaji madini linawashikilia watuhumiwa wawili EDWARD FRANCIS KESSY [31] na FEISAL MOHAMED ABDULLAH [23] wote wakazi wa Mji Mdogo wa Makongolosi Wilaya ya Chunya wakiwa wanatorosha madini aina ya dhahabu yenye uzito wa Gramu 1,083.73.

Watuhumiwa walikamatwa Novemba 11, 2023 majira ya saa 6:20 usiku huko maeneo ya Kawetele mkoani Mbeya wakiwa kwenye Gari aina ya Mark X, rangi ya silver yenye namba za usajili T.866 EAV wakitokea Makongolosi wilaya ya Chunya.

Katika upekuzi uliofanywa kwenye Gari hilo, watuhumiwa walikutwa wakiwa na vipande 28 vya madini ya dhahabu yenye thamani ya Tsh. 141,929,564.52/= bila kuwa na kibali cha kusafirisha madini hayo. Watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa na mara baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani.

Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia wawili JAMES JOHN MWAMATEPELA [29] na WILLE GODEN MWANDWANI [23] wote wakazi wa Kijiji cha Ngyeke wilaya ya Kyela kwa tuhuma za kupatikana na noti bandia 42 za Tsh.10,000/=.

Watuhumiwa walikamatwa Novemba 11, 2023 majira ya saa 8:00 mchana huko Kijiji cha Ngyeke, Wilaya ya Kyela, katika muendelezo wa Misako inayofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya.

Watuhumiwa wamekuwa wakitumia noti hizo kununulia bidhaa mbalimbali kwa wafanyabiashara wakiwaaminisha kuwa ni fedha halali, wanaendelea kuhojiwa na mara baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani.
 
Je wakisema nao walipewa hizo noti bila kujua? Na wakimtaja aliyewapa nae aseme alipewa kama bila kujua?
 
Back
Top Bottom