JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,462
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia wahamiaji haramu 16 raia wa nchini Ethiopia, wote wanaume, umri kati ya miaka 18 - 53 kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.
Watuhumiwa walikamatwa Novemba 09, 2023 majira ya 2:00 asubuhi huko kijiji cha Kasumulu, Wilaya ya Kyela, wakati Askari wa Kikosi maalum cha kuzuia na kupambana na uhalifu cha Jeshi la Polisi kikiwa doria.
Watuhumiwa walikuwa wanasafirishwa kwa kutumia gari lenye namba za usajili T.392 DCP aina ya Toyota Ipsum ambayo mmiliki wake anatafutwa. Dereva wa gari hilo anatafutwa kwani amekimbia na kutelekeza gari mara baada ya kuwaona askari wakilifuatilia gari hilo. Watuhumiwa walikuwa na lengo la kuvuka kupitia vivuko visivyo rasmi kwenda Afrika Kusini kupitia nchini malawi.
Vile vile katika muendelezo wa misako Novemba 11, 2023 majira ya saa 7:20 usiku huko katika Kijiji cha Kyimo, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa mbeya, Jeshi la Polisi liliwakamata watuhumiwa watatu ambao ni 1. ASAYA ASAJILE [32] Mkazi wa Kyimo, 2. FRANK GOOLUCK [21] Mkazi wa Mpemba na 3. WATSON SIMON [28] Mkazi wa Tunduma wakiwa na vifaa mbalimbali vya kuvunjia majengo kwa lengo la kufanya uhalifu.
Baada ya kukamatwa walifanyiwa upekuzi kwenye nyumba waliyokuwa wanaishi na kukutwa wakiwa na TV moja inchi 32 aina ya Hometech, Godoro moja 5x6, Mtungi mdogo wa Gas, Radio 3 aina ya Subwoofer, Bag 2 ndogo za mgongoni, viatu pea 6 na nguo mbalimbali ambavyo ni mali za wizi.