Indume Yene
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 2,950
- 711
Hizi habari za SISIEMU kotofautiana kutokana na mgombea wao ni kwa mujibu wa habari iliyoko katika gazeti la Mtanzania Daima. Soma hapa chini:
CCM sasa ngoma nzito Mbeya Vijijini
Wabunge wake wagawanyika
na Mwandishi Wetu
ZIKIWA zimebaki siku tano kabla ya kuanza kampeni za uchaguzi mdogo Mbeya Vijijini, hali ya kisiasa ndani na nje ya vyama vinavyoshiriki kwenye uchaguzi huo inaonyesha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kipo katika wakati ngumu wa kuendelea kushikilia kiti hicho kilichokuwa chini ya mbunge wake, marehemu Richard Nyaulawa.
Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima, unaonyesha kuwa moja ya mambo yanayoiweka CCM katika nafasi ngumu kwenye uchaguzi huo ni mgombea wake, Mchungaji Luckson Mwanjale, kutoungwa mkono na wabunge wa mkoa huo kutokana na tofauti za makundi yaliyokuwapo mwaka 2005 wakati wa mchakato wa kusaka mgombea urais.
Mmoja wa wabunge wa mkoa huo aliyezungumza na Tanzania Daima kwa sharti la kutotajwa, alisema Mchungaji Mwanjale alikuwa mwana mtandao asilia, hivyo hakumuunga mkono Profesa Mark Mwandosya (kutoka Mbeya) aliyewania kiti hicho na kushindwa na Rais Jakaya Kikwete.
Makundi hayo ndiyo yanayoendelea kuutafuna Mkoa wa Mbeya na ndiyo sababu ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba kushindwa kufika mkoani Mbeya katika ziara yake ya hivi karibuni aliyoishia mkoani Iringa, baadaye Dodoma na Arusha.
Wakati Makamba akiwa mkoani Iringa, iliwahi kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa CCM Mbeya hawamtaki Makamba mkoani humo, taarifa ambayo hata hivyo baadaye ilikanushwa na chama hicho tawala.
Ukiachia mpasuko huo, habari zaidi zinadai kuwa mgombea huyo hana sifa za kutosha kuungwa mkono na wananchi wa jimbo hilo kutokana na elimu yake, ikilinganishwa na wagombea waliopitishwa na vyama vingine vya CHADEMA na CUF.
Mwanjale alishaomba kuteuliwa kuwania ubunge katika jimbo hilo kupitia CCM mara tatu na mara zote alishindwa kutokana na kuzidiwa sifa na wagombea wenzake kama alivyozidiwa na marehemu Nyaulawa katika uteuzi wa ubunge, mwaka 2005, sasa safari hii sifa hizo amezipata wapi? alisema mchambuzi huyo wa siasa ambaye hakupenda jina lake litajwe.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanailezea hali hiyo kuwa inaweza kumwathiri mgombea huyo na chama chake, kwa kuwa wananchi wanaweza kuhofia kumchagua kwa sababu alishathibitika kuzidiwa sifa na wagombea waliopita.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati, aliripotiwa na waandishi wa habari Jumapili iliyopita, akikiri kuwa Mwanjale alishaomba kuteuliwa kuwania kiti hicho katika chaguzi zilizopita lakini hakupitishwa kwa madai kuwa alikuwa hajakomaa kisiasa.
Chiligati alisema CCM imempitisha mgombea huyo baada ya kuona sasa amekomaa na kudhihirisha uvumilivu na ustahimilivu mkubwa wa kisiasa, kwani angeweza kukimbilia upinzani.
Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wanauona msimamo huo wa CCM kumtetea mgombea wake, kuwa unakiweka chama hicho kikongwe nchini katika mazingira hatarishi kwenye uchaguzi huo.
Wanaona kuwa itawawia vigumu wananchi kuamini kwa haraka ukomavu wa mgombea huyo katika kipindi cha kampeni, hasa ikizingatiwa kuwa hakuungwa mkono na chama chake huko nyuma.
Hii inaweza kusababisha wananchi kuamua kutafuta chaguo lililo bora kutoka vyama vingine, alisema mmoja wa wataalamu hao.
Baadhi yao wanakitafsiri kitendo cha CCM kumpitisha mgombea huyo kuwa kimechangiwa na kukosa mgombea mwingine mwenye umaarufu kati ya waliojitokeza, baada ya kuepuka kumpitisha, Jenerali Mstaafu Robert Mboma, kutokana na kushambuliwa tangu awali.
Mwanjale (58), Katibu wa CCM jimboni humo na mchungaji wa dhehebu la Uinjilisiti, mwenye stashahada ya ufundi, anaonekana kuwa dhaifu mbele ya mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Shambwee Shitambala, ambaye kitaaluma ni wakili, na mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Daudi Mponzi, ambaye ni Mhandisi wa Mawasiliano.
Aidha, katika miaka ya hivi karibuni, CCM inaonekana kupungukiwa wanasiasa wenye mvuto na uwezo wa kulitawala jukwaa la kisiasa katika mikutano ya kampeni zake, hasa baada ya gwiji lake la kampeni, Makamu Mwenyekiti Mstaafu, John Malecela, kutopenda kushiriki kwenye kampeni kama ilivyokuwa Tarime, ambapo CCM ilimteua kuwa mmoja wa wapiga debe wake, lakini hakushiriki.
Uamuzi wa CCM kupanga kumtumia Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, katika uzinduzi wa kampeni zake, unadaiwa kuwa unaweza kutia doa kampeni hizo, kutokana na tuhuma nyingi za ufisadi kudaiwa kuwa zilianzia katika awamu yake.
Kwa upande mwingine, umaarufu wa CCM katika jimbo hilo na Mkoa wa Mbeya kwa ujumla unaonekana kupungua, hasa ikizingatiwa kuwa Rais Kikwete, alipofanya ziara mkoani humo, msafara wake uliripotiwa kutupiwa mawe na wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira na kutotekelezwa kwa ahadi ya maisha bora kwa kila Mtanzania.
CCM inatarajiwa kuzindua kampeni zake Januari 4, mwaka 2009.