Mbeya vijijini: Kampeni, uchaguzi na yatokanayo

Mheshimiwa NL,
CCM ni nambari wani,
CCM watalirudisha hili Jimbo, penda usipende.
Tumuombe Muumba ili uone kwa macho yako na usikie kwa masikio yako.
Stay blessed.

Zilezile kauli za vitisho na ubabe. Sasa kama ni hivyo kuna haja gani ya uchaguzi. Sasa Wana Mbeya wakiamua kuigomea CCM kama Tarime hiyo penda usipende matokeo yake yatakuwaje? Vurugu, Polisi na virungu au kucheza na matokeo?

Watch your words, tusonge mbele tusirudi tulikotoka.
 
Mheshimiwa NL,
CCM ni nambari wani,
CCM watalirudisha hili Jimbo, penda usipende.
Tumuombe Muumba ili uone kwa macho yako na usikie kwa masikio yako.
Stay blessed.

Mkuu,

Nambari wani kwa lipi? kwa rushwa na ufisadi au kwa kuwaahidi wananchi maisha bora tu bila kutekeleza hayo kwa vitendo?

Pastor how far are you sure kwamba wanalirudisha hilo Jimbo? unajua nani atagombea kwa tiketi ya CCM na je, unajua nani watagombea kutoka vyama vingine vya upinzania as of now?

Huko kujihakikishia mapema kunanipa mashaka sana!

Cheers
 
Nambari wani au Number one, kwa lipi? 40 years in power hakuna cha maana walichokifanya ukilinganisha na muda waliokaa madarakani, ni politics tu.

To mention few, TRL aka TRC hoi, TAZARA, ATC, Ujenzi wa miundo mbinu ovyo eg barabara za JIJI la DSM zinazofurika maji na magari kila kukicha, hospitali hoi, shule hoi, wananchi hoi, Mashirika ya Umma hoi, SUKITA hoi, Ranchi za Taifa hoi, Viwanda vya umma hoi, ufisadi ndio umeshamili kuanzia EPA, RICHMOND, IPTL, BUZWAGI, IMPORT SUPPORT, ATCL, NBC, KILOMBERO SUGAR, MTIBWA SUGAR. Just to mention a few.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi, CCM hoye, Watanzania hoi, wapiga kura hoi

Hope baba mchungaji amekupata vilivyo hapa.......Mungu atakushushia malaika wake wakupe mwangaza wa kweli ili macho yako yenye utando mzito wa ''kijani'' kama (water lilies) yaweza safishika, na kuona vizuri na kuyakiri haya yasemwayo na ndipo baba mchungaji na wengine kama wewe mtanena kwa lugha mkiitangaza kweli hii na ukweli huo utawaweka huru milele!

Amen
 
Hili Jimbo ni la CCM.
CCM ni 'lazima' tulirudishe.
(Hata kama mtaanzisha operation 'mjebuka')

huko hatukupigwa mawee!! Mimi ni mwenzako lakini kwa hilo tutofautiane ikiwezekana tusigombee kabisa maana inabidi tupungue bungeni ili 2010 wasije kutuuliza tuliwapa wabunge wengi tupeni maendeleo siku hizi nchi imekuwa na watu wa department ya monitoring and evaluation, tukienda watatudai wale ndugu zao tuliowafunga kwa kurusha mawe na hela za EAC, halafu wanachuo wengi wamerudi kwao watatuuliza tunawafikiriaje na watakuwa wameanza kulima watauliza hela za EPA zitawafikia lini na unajua tunataka tuzitumie kwa kuwadanganya wakulima kati ya 2009 mwishoni na 2010, huku mjini si unajua hatuna bao????
 
CCM Mbeya wamkataa Makamba

2008-11-24 10:03:03
Na Thobias Mwanakatwe, Mbeya

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya, wamempiga marufuku Katibu Mkuu wao, Yusuph Makamba kushiriki katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijijini.

Wana-CCM hao wamedai kuwa, hatua hiyo imelenga katika kukinusuru chama chao kusiangushwe kwenye uchaguzi huo.

Walitoa msimamo huo wakati wakizungumza kwa nyakati tofauti na Nipashe kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Mbeya uliofanyika Chuo cha Kilimo Uyole wilayani hapa.

Jimbo la Mbeya Vijijini, limeachwa wazi kufuatia kifo cha Richard Nyaulawa aliyefariki dunia Novemba 9, mwaka huu kwa ugonjwa wa saratani ya ini na kuzikwa kijijini kwao Inyala wilaya ya Mbeya vijijini Novemba 13, mwaka huu.

Uchaguzi huo utafanyika baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutangaza tarehe.

Wakizungumzia mtazamo wao kuhusu uchaguzi wa jimbo hilo, walisema Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete pamoja na viongozi wengine wa juu wa chama hicho, wasimpendekeze Makamba kushiriki kwenye kampeni za uchaguzi wa jimboni humo.

Walisema kutokana na hali ya sasa ilivyo ndani ya chama mkoani Mbeya pamoja na jimbo hilo, iwapo Makamba atapendekezwa kuendesha kampeni kwenye uchaguzi huo, kuna hatari CCM jimbo hilo litanyakuliwa na wapinzani.

Wanachama hao walisema hivi sasa vyama vya upinzani vimevamia jimbo hilo kwa kuendesha kampeni za chini chini, hivyo lazima iwateue viongozi makini ambao wataweza kuendesha kampeni nzuri na za kistaarabu na kukiwezesha chama kulitetea jimbo hilo.

``Makamba hivi sasa hatakiwi na wabunge wengi hasa kutokana na mwelekeo wa chama kuwa mbaya kwa sababu ameshindwa kukiweka chama kwenye mstari, sasa tukithubutu kumleta hapa Mbeya ashiriki kwenye uchaguzi wa Mbeya Vijijini, hili jimbo watalinyakua wapinzani,`` alisema mwanachama mmoja toka Wilaya ya Chunya.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya, Albert Mgumba akizungumza na Nipashe kuhusiana na tamko hilo la wana-CCM, alijibu kwa kifupi kuwa, madai hayo hayana msingi kwani Makamba ni Katibu Mkuu wa chama hivyo ni lazima atakuja kwenye kampeni za uchaguzi wa Jimbo la Mbeya Vijijini.

Hivi karibuni, wabunge wa CCM, walinukuliwa na vyombo vya habari wakimtaka Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Kikwete kutowarundikia vyeo wateule anaowapa nafasi mbalimbali za uongozi kama alivyofanya kwa Makamba.

Miongoni mwa wabunge waliotoa msimamo huo ni Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (CCM) na Benson Mpesya (CCM-Mbeya Mjini).

Zambi na Mpesya, walisema tabia ya Rais kumteua mtu mmoja kushika nafasi mbalimbali za uongozi kwa wakati mmoja, imekuwa sababu ya kuzorota na kushuka kwa ufanisi miongoni mwa viongozi wa namna hiyo.

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mpesya alisema Makamba hakustahili kupewa vyeo vyote hivyo kwani hana uwezo na wanataka aondoke si kwa sababu wanamwonea wivu bali wanafanya hivyo kwa maslahi ya chama chao.

Alisema Makamba amekuwa akikumbatia watu wenye fedha na kuacha wenye uwezo, hali iliyokigawa chama hicho hata kusababisha kushindwa katika uchaguzi mdogo wa Tarime.

``Katibu Mkuu si anakuwa mtu mmoja tu? Ndiyo maana tunasema hana uwezo hana hoja. Yeye kazi yake ni kukigawa chama katika makundi, � alisema Mpesya.

Mbali na hilo alisema, Makamba amekuwa ni kiongozi anayezungumza maneno mengi kuliko kuwa mtendaji wakati nafasi ya Ukatibu Mkuu ni ya utendaji.

Naye Zambi alisema wakiwa Dodoma, hakuna wabunge wa CCM waliowahi kujadili jambo lolote kuhusu suala zima la wao kutoridhishwa na namna Rais Kikwete alivyolishughulikia jambo hilo.

Badala yake, alisema wabunge wa chama hicho tawala walieleza kuhusu msimamo wao wa kutoridhishwa na utendaji na ufanisi wa kikazi wa Katibu Mkuu wa CCM, Makamba na wakafikia hatua ya kutaka kiongozi huyo aondolewe na vikao vya juu.

Alisema kukwama kwa Makamba kutimiza sawasawa majukumu yake, kunasababishwa na ukweli kwamba, kiongozi huyo amelimbikiziwa madaraka mengi hali ambayo inasababisha akwame kutimiza wajibu wake sawasawa.

Mtu huyo huyo mmoja ni Katibu Mkuu wa chama na pia ni Mbunge wa Kuteuliwa. Ukatibu mkuu ni cheo kikubwa ndiyo nafasi ya utendaji, unaingia vikao vingi vya chama. Vyeo hivi vinamzidia, chama kinazorota,`` alisema Zambi.

Alisisitiza kuwa, Makamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Chiligati, wameshindwa kutekeleza majukumu yao hali iliyochangia chama hicho kufanya vibaya katika uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani uliofanyika hivi karibuni jimboni Tarime.

SOURCE: Nipashe
 
Sisiemu bwana weeee jamaa yao hata hajamaliza wiki mbili Kabrini tayari wanazungumzia uchaguzi? si wampe urithi wa uchaguzi mwanae Nyaulawa maana walisema kumuenzi?
 
Anaweza asifike Mbeya mjini kwani njia nzima toka mpakani mwa Iringa na Mbeya ni mawe matupu barabarani huhitaji kuyasomba toka mbali !!!!!!!!
 
Ukabila waitafuna CCM Mbeya vijijini



na Christopher Nyenyembe, Mbeya




DHAMBI ya ukabila imeanza kukitafuna Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Mbeya Vijijini, baada ya baadhi ya makada wa chama hicho kuanza kupita vijijini wakihimiza wapiga kura kumchagua mgombea wa kabila la Wamalila.

Harakati hizo za makada wa CCM kuanza kupita kwa wapiga kura, zinafuatia kiti cha ubunge cha jimbo hilo kuwa wazi, baada ya kufariki kwa aliyekuwa mbunge wake, Richard Nyaulawa.

Uchunguzi wa Tanzania Daima umebaini kuwa baadhi ya viongozi CCM wa mkoa na wilaya wamekuwa wakizunguka kata zote 17 zinazounda jimbo hilo, kutoa pole kwa wananchi kwa kupotelewa na mbunge wao, huku wakitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea kutoka kabila la Wamalila.

Baadhi ya wanachama wa chama hicho wamelieleza gazeti hili kuwa viongozi wa chama hicho wanaopita kuwapa pole, wamekuwa wakiwaomba kumchagua mgombea kutoka kabila hilo kwa sababu safari hii ni zamu ya kabila hilo kutoa mbunge kwa sababu wabunge waliotangulia walitoka makabila mengine.

“Hivi sasa lazima mgombea wetu wa ubunge atoke upande wa Umalila, Nyaulawa alitoka Tarafa ya Tembela na Mwalyego alitoka Tarafa ya Bonde la Songwe, sasa zamu hii ni yetu lazima mgombea atoke Tarafa ya Umalila,” alikaririwa mmoja wa makada wa chama hicho ambaye jina lake tunalifadhi kwa sasa.

Kada huyo alikaririwa zaidi akieleza kuwa awali katika kipindi kisichozidi vipindi viwili vya kukaa jimboni kwa wabunge wawili waliofariki wakiwa madarakani. Jimbo hilo lilikuwa likiongozwa na Dk Edward Shiwa aliyetoka katika kabila la Wamalila na sasa wanataka kumpata mbunge mwingine kutoka upande huo.

Mazingira hayo na pilikapilika za wagombea wa CCM ambao wengi walijinadi katika kura za maoni za mwaka 2005, sasa yanaonekana kwa kasi na inadaiwa kuwa ndio wanaowashawishi wanachama wengi kuwawekea ngumu wagombea wengine kutoka nje ya mkoa huo ambao ni wazaliwa wa jimbo hilo .

Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya, Albert Mgumba, alipohojiwa kuhusu harakati za baadhi ya wanachama wa chama hicho kuanza kubomoana na kujijenga kwa dhana ya ukabila na kuwakataa ndugu zao wanaoishi nje ya mkoa huo, alisema hana taarifa hizo.

Hana taarifa rasmi kama kuna dhana ya kutaka ubunge wa jimbo hilo kwa mgawanyo wa ukabila, bali anachofahamu ni kuwa mchakato kamili haujaanza hadi hapo tume ya uchaguzi itakapotangaza, ili kazi kamili ya kuwachuja wagombea watakaojitokeza itakapoanza ndani ya vikao vya chama.





juu
Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 8 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Tunamtaka mmalila mwenye sifa za kijeshi,aliefikia ngazi ya mwisho kabisa kwenye uongozi wa kijeshi wa nchi hii,na pasipo mjadala ndie mbunge ajae wa mbeya vijijini.Ni suala la muda tu kila kitu kimekwisha kuwekwa mezani.

na Lupakisyo, Mbeya, - 29.11.08 @ 14:07 | #1207

Dhambi ya ubaguzi na ukabili imeshatamalaki ndani ya CCM, wanachofanya Mbeya ndiyo picha halisi ya wana CCM

na nguno buchenja, mwanza, - 29.11.08 @ 14:15 | #1210

KAMA MPIGIWA DEBE NI MWANA CCM ASUBIRI SIKU YA KIFO CHAKE NDIO MBEYA WATAJENGEWA CHUO KIKUU KAMA CHA DODOMA ILI KUMUENZI HIZO NI SERA ZA WAZI ZA CCM.HAPAJENGWI KITU KWENYE JIMBO LAKO HADI UFARIKI.

na OLE LENGAI, TANZANIA, - 29.11.08 @ 15:54 | #1227

Wapinzani maadui wenu wanaanza kutengana nanyi muwe mkono mmoja. Tazameni uchaguzi wa 2005 chama gani chapili baada ya ccm kilipata kura nyingi zaidi baadae vyama vilivobakia vikiunge mkono chama hicho ili upizani uhakikishe ushindi wapili nasi tufurahi.

Hii ndio njia pekee ya kuiangusha ccm. Mungu awe pamoja na wapinzani ili ufisadi utokomee

na Mshindo, Boko, - 29.11.08 @ 16:38 | #1233

TUNAMUOMBA MUNGU UKABILA UWATAFUNE MPAKA UWAMALIZE NA WAANGAMIE NA UPINZANI UJE JUU ILI WATULETEE MEMA AMBAYO YAMETOWEKA KWA MIAKA MINGI

na BOSKO, PUGU, - 29.11.08 @ 16:43 | #1234

Tunataka kuiona alfajiri mpya ikizaliwa kwani tumechoka kuishi kizani. Umoja ni nguvu na utengano utazidi kutuletea maafa na majuto mjukuu.

na Yusufu, La Mboto, - 29.11.08 @ 16:47 | #1235

Huko Mbeya angelipelekwa Mikamba ili akavune wanachama wapya. Lakini huyu babu yuhai maana sijamuona wala kumsikia, au ndio keshatimuliwa ccm? Ikiwa ni hivo haraka ajiunge na upinzani

na ismai, dar, - 29.11.08 @ 20:22 | #1258

Ni kukosa busara kama wako watu wanasumbuliwa na ukabila.Sijui Wananchi wanasemaje au wanaafiki sera za kikabila kama hizo.Mimi nilifikiri kiongozi anachaguliwa kwa kufuata anavyowafaa Wale ataowaongoza lakini picha hii inanikanganya kwani kanaonekana karoho ka ukabila kameshika mhimili hapo.kumbe ndg zangu wa Mbeya bado mnasera za kizamani?Mnajiaibisha hata wale wasio kuwa na tabia hizo.Wamalila! Wamalila!

na rachel, Mtz, - 30.11.08 @ 11:19 | #1313
 
Wabunge wa CCM watakufa mmoja mmoja mpaka wamalizike ,nahisi ukimaliza uchaguzi huu basi mwengine ataanguka na kufilia mbali maana hawa hawakushinda katika uchaguzi mkuu kwa nguvu za raia bali walishinda kwa nguvu za chama Tawala na waliozulumiwa katika mikoa ambayo zambi hii ilitendeka wataangamia tu mmoja mmoja,nani atabaki huyo atakuwa amebahatika ,ole wao wanaoiba kura na wanaosaidia kuiba kura na kubadilisha matokeo kwa nguvu na kasi ,hao hawana salama kwenye mkono wa Mwenyezi Mungu na Mheshimiwa Raisi analijua hilo ,anaezulumu huwa ni mwenye kula hasara tu hata afanye nini.
 
Mwiba,
Wabunge wa CCM watakufa mmoja mmoja mpaka wamalizike ,nahisi ukimaliza uchaguzi huu basi mwengine ataanguka na kufilia mbali maana hawa hawakushinda katika uchaguzi mkuu kwa nguvu za raia bali walishinda kwa nguvu za chama Tawala na waliozulumiwa katika mikoa ambayo zambi hii ilitendeka wataangamia tu mmoja mmoja,
..
Whew!... hiki kimbunga mkuu wangu hivi hapo juu ulikuwa unamtolea mfano marehemu Richard Nyaulawa?...
 
Kumbe uko vijijivni CCM wanapukutika kama usufi unaozuia upepo.kama nilivyowahi kusema hawa CCM walioiba kura watakufa vifo vya mende mpaka wengine au wenzao wataogopa kugombea maana ukishionda kwa varange jamaa atamaliza njia zote hata za ushirikina kuhakikisha humalizi n'ngwe ,yaani mikakati ya waliozulumiwa naitarajia sana hasa kwa nchi yetu yenye watu wengi wanaoamini ushirikina ,ni kazi kweli kuwepo salama na hasa huko vijijini watamalizana tu ikiwa hakuna uchaguzi wa haki na usawa. kwa habari iliyopo hapa chini mwisho wa habari inaonekana sasa wezi na waandaaji wa wizi kura wameanza kuogopa.Hivyo haki imeanza kutawala .

CUF yazidi kuiliza CCM Ruangwa

2008-12-02 11:16:45
Na Abdul Mitumba, Ruangwa Lindi


Chama cha Wananchi (CUF), kimezidi kukiliza chama tawala (CCM) mkoani hapa, baada ya kushinda kiti cha tatu cha Uenyekiti wa Serikali ya kijiji kati ya vijiji vinne vinavyounda Kata ya Nambilanje iliyopo wilayani Ruangwa katika mkoa wa Lindi.

Awali, CUF ilifanikiwa kushinda katika vijiji vya Nanjaru na Mtondo, huku CCM ikipata ushindi katika Kijiji kimoja tu cha Nambilanje ambako ndiko yalipo makao makuu ya Kata hiyo.

Katika uchaguzi mdogo wa nafasi za Wenyeviti uliofanyika juzi katika vijiji vya Nambilanje na Nanjaru, CCM kupitia kwa mgombea wake, Said Manyali ilishinda baada ya kupata kura 229 dhidi ya 121 za mgombea wa CUF, Abdallah Mkwindinga.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Dk. Julius Anga, alisema mjini hapa kuwa, CUF imeshinda katika kijiji cha Nanjaru kwa mgombea wake, Ally Wania baada ya kupata kura 195 dhidi ya 150 za Said Nangalapa wa CCM.

Dk. Anga alisema kwa matokeo hayo, CUF imefanikiwa kushinda vijiji vitatu kati ya vinne vinavyounda Kata ya Nambiranje, ambavyo ni Nanjaru, Mkaranga na Mtondo.

Alifafanua kuwa, uchaguzi huo mdogo umefanyika kufuatia wenyeviti wa zamani kufariki dunia baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchi nzima mwishoni mwa mwaka 2004.

Alisema kwa ujumla uchaguzi huo ulifanyika kwa haki, huru na kwamba kila upande ulioshiriki ulimeridhika.
 
Kipyenga cha kinyang'anyiro cha uchaguzi wa marudio Mbeya Vijijini kinakaribia kupulizwa. Wachunguzi wa mambo wanaona ushindani mkali utakuwepo baina ya Mchungaji Mwanjali na Wakili Shitambala. Mchungaji Mwanjali ni mtu muhimu wa lile kundi maarufu kama mtandao na ndiye aliyempa mshike mshike wakati wote marehemu Nyaulawa. Nyuma ya mchungaji huyu yupo Mzungu anayejulikana kama Leiner ambaye kanisa lake pamoja na kutoa huduma ya kiroho limewekeza katika sekta ya madini, ambaye amewahi kuandikwa magezitini akiwa na kashfa ambazo alizakanusha. Kwa upande mwingine, bwana Sambwee Shitambala anaelekea kukubalika miongoni mwa vijana wa kijijini na wasomi wenye asili ya jimbo hilo.

Tusubiri tuone

PM
 
[COLOR="Red" said:
Paparazi Muwazi;347049]Kipyenga cha kinyang'anyiro cha uchaguzi wa marudio Mbeya Vijijini kinakaribia kupulizwa. Wachunguzi wa mambo wanaona ushindani mkali utakuwepo baina ya Mchungaji Mwanjali na Wakili Shitambala. Mchungaji Mwanjali ni mtu muhimu wa lile kundi maarufu kama mtandao na ndiye aliyempa mshike mshike wakati wote marehemu Nyaulawa. Nyuma ya mchungaji huyu yupo Mzungu anayejulikana kama Leiner ambaye kanisa lake pamoja na kutoa huduma ya kiroho limewekeza katika sekta ya madini, ambaye amewahi kuandikwa magezitini akiwa na kashfa ambazo alizakanusha. Kwa upande mwingine, bwana Sambwee Shitambala anaelekea kukubalika miongoni mwa vijana wa kijijini na wasomi wenye asili ya jimbo hilo.[/COLOR]

Tusubiri tuone

Inatakiwa ipatikane brain inayoweza kuwakwamua wananchi wa lile jimbo. Wana resources kibao lakini bado wanahaha na maisha. Wenyewe issue ni mbolea tu. Bei yake imekwamisha shughuli za kilimo kwa muda mrefu sana.
 
CUF hawana mtu wao huko?Au wameamua kuwaunga mkono chadema kama tarime?

CUF wanaye soma hapa http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=1025 toka Tanzania daima '' WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Wilaya ya Mbeya Vijijini jana wamemchagua na kumthibitisha Mhandisi wa Mawasiliano, Daudi Mponzi, kuwa mteule wa chama hicho katika kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Mbeya Vijijini.

Ila hawa wapiganaji ni busara waunganishe nguvu badala ya kugawana kura kwani hiyo itawapa nafasi wezi wa kura kufanya vitu vyao!
 
Kipyenga cha kinyang'anyiro cha uchaguzi wa marudio Mbeya Vijijini kinakaribia kupulizwa. Wachunguzi wa mambo wanaona ushindani mkali utakuwepo baina ya Mchungaji Mwanjali na Wakili Shitambala. Mchungaji Mwanjali ni mtu muhimu wa lile kundi maarufu kama mtandao na ndiye aliyempa mshike mshike wakati wote marehemu Nyaulawa. Nyuma ya mchungaji huyu yupo Mzungu anayejulikana kama Leiner ambaye kanisa lake pamoja na kutoa huduma ya kiroho limewekeza katika sekta ya madini, ambaye amewahi kuandikwa magezitini akiwa na kashfa ambazo alizakanusha. Kwa upande mwingine, bwana Sambwee Shitambala anaelekea kukubalika miongoni mwa vijana wa kijijini na wasomi wenye asili ya jimbo hilo.

Tusubiri tuone

PM

Huyo mzungu Leiner naye ana kanisa? Unaweza kutufafanulia hizo kashfa za madini alizozikanusha?
 
Back
Top Bottom