Mbeya vijijini: Kampeni, uchaguzi na yatokanayo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbeya vijijini: Kampeni, uchaguzi na yatokanayo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ibrah, Nov 14, 2008.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Juzi Waziri wa Nishati Mh. Ngeleja alinukuliwa akisema kuwa Serikali imeamua kumuenzi aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Vijijini Marehemu Richard Nyaulawa kwa kupeleka Umeme katika Jimbo la Mbeya vijijini.

  Jana Rais Kikwete aliwaongoza waombolezaji kwenye mazishi ya Mbunge huyo huko Kijijini Inyala, Mbeya vijijini. Ukweli ni kwamba ilikuwa ni jambo zuri na la Kibinadamu Rais kufanya hivyo.

  Hata hivyo kuna hisia kuwa CCM wameanza kampeni ya ubunge jimboni hapo kwa sababu zifuatazo:-

  Je, ni kwa nini Waziri Ngeleja atoe kauli hiyo baada ya kifo cha Nyaulawa? Ni kweli kuwa katika Bajeti ya mwaka huu ya Wizara kuna fungu kwa ajili ya kupeleka umeme katika Jimbo hilo au ni kiwewe cha Uchaguzi mdogo baada ya CCM kushindwa vibaya huko Tarime? Yaani kumuenzi mtu ni hadi pale anapokufa tu au kuna maslahi binafsi ya kisiasa? Hata Mhariri wa Mtanzania jana amemtuhumu Waziri Ngeleja kwa kauli yake kuwa Serikali itamuenzi Marehemu Nyaulawa kwa kuweka umeme Jimboni kwake baada ya kufa!

  Je, ni kwanini Mh. Rais hakuwahi kuhudhuria mazishi ya Wabunge wengine waliofariki kabla ya Nyaulawa (Sikumbuki kama alihudhuria mazishi ya Mbunge wa Kiteto) kama y aMbunge wa Kiteto, Amina Chifupa, Salome Mbatia, na Chacha Wangwe Zakayo? Marehemu Nyaulawa ndiye Mbunge muhimu kuliko wote waliotangulia mbele za haki? (Sisemi hiovyo kwa nia mbaya lakini ni muhimu pia kujiuliza na tunapokosea turekebishwe na kujifunza).

  Au ni kiwewe cha Matokeo ya Uchaguzi wa Jimbo la Tarime ndiyo imepelekea kauli pofu na matukio ya Utu kama haya kwa viongozi wetu? Vinginevyo nashawishika kuamini kuwa hizo ni Kampeni za mapema kwa nia ya Maslahi ya Kisiasa tu.

  Mnisamehe wana JF hayo ni maoni/maswali maana ni vema Nchi na Wizara inongozwe kwa mujibu wa Bajeti na Mipango iliyokwisha weka kabla na si baada ya matukio.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Wameshasoma alama za nyakati.
   
 3. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  La kujiuliza hapa ni kuwa iwapo jimbo la Mbeya Vijijini kwa kupoteza Mbunge wake linaenziwa kwa kupelekewa Umeme.

  Je, wabunge wengine waliotangulia mbinguni wao kwenye majimbo yao Serikali iliwaenzi kwa Miradi Gani?
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hata wapeleke rami mwaka wa shetani huu ni chaliiiiiiiiii.
  Wanakumbuka kuvuta blanket wakati kumekucha watakiuona cha mtema kuni CCM.
  Wamepewa miaka kibao toka miaka ya 1961-2008 mpaka hesabu miaka mingapi imepita leo ndo wanawakumbuka kupeleka umeme.
  Moto uliowashwa Tarime unasambaa kote sasa.
   
 5. m

  macinkus JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2008
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 260
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  rais wetu ana muda kweli wa kuhudhuria shughuli. alionekana akiaga mwili wa marehemu dare es salaam pamoja na waheshiwa wengine wengi tu. kesho yake akachukua pipa la serikali kuelekea mbeya kwenda kushuhudia mazishi kijijini inyala. heko rais wetu kwa roho ya ubinadamu!!

  macinkus
   
 6. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Viongozi wetu ni Washenzi.
  Ni UShenzi wa hali ya juu kuwaambia wananchi kwamba watapata huduma muhimu ya umeme kwa sababu ya kumuenzi Mbunge ambaye sasa ni Marehemu.
  Nasema Huu ni Ushenzi wa hali ya juu na ni dalili moja kwamba Viongozi wa CCM bado wako nyuma kifikra, kisiasa na kiutamaduni.
  Viongozi wa CCM bila aibu wanasimama wima kwa miguu miwili na kutangaza nia yao yenye hila ya kutumia Mafungu ya Serikali kama Fimbo, Shoka, Nyengo au Msemeno wa kuwakata maini wananchi waliowaweka madarakani.
  Kuna mambo yanaweza kuvumiliwa angalau kidogo lakini hili ni moja kati ya mambo yanayo takiwa kukemewa kwa nguvu zote.

  Umeme wa maeneo yote ya nchi uliwekwa kuwaenzi nani?
  Ni kitu gani kingine zaidi ya umeme hutumika kuwaenzi marehemu?
  Tangu lini huduma muhimu kama umeme zinakuwa ni sehemu za kuwaenzi Marehemu?
  Kwa nini baada ya miaka 47 ya Uhuru CCM bado hawajanawa Matongotongo ya ushenzi?

  CCM ni washenzi kweli kweli.
   
 7. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #7
  Nov 14, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Wanafunzi wanalia chuo kule raisi anaenda kwenye msiba hana muda wa kusikiliza wanafunzi hii kali sana
   
 8. m

  macinkus JF-Expert Member

  #8
  Nov 14, 2008
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 260
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  na hasa ikizingatiwa kwamba alikwisha kuuaga mwili wa marehemu, yeye akiwa na mkewe, ukiwa haujaondoka kwenda kijijini, ni la ajabu kuamua kwenda kushuhudia mazishi!ni kweli rais wetu ni rahisi sana. hana kazi za kufanya ofisini. sitashangaa wiki hii akipata safari nyingine nje ya nchi au akaamua kumalizia wiki ijayo kwenye mkoa mojawapo na msafara kafiri wa mashangingi (baada ya kula yule kondoo aliepewa na wapare kumpongeza kazi nzurri ya EPA!!

  macinkus
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Nov 14, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mengine yanastahili yawafike kwani pale viongozi wa upinzani wanapokauka sauti na kukohoa kwa kuzunguluka nchi nzima kusema na kuisema CCM na selikali yake hazina dira na hakuna mabadiliko yatakayoletwa na CCM zaidi ya kasi ya maisha kuzidi kuwa makali ,nasema ziki na shida tunajitakia wenyewe kwa maana ufikapo wakati wa Uchaguzi wananchi husahau matatizo na madai yao yasiosikilizwa na CCM na kuwapigia kura CCM ili waongoze nchi kwa muhula mwengine.
  Hivi pale upinzani wanaposema msihadaike na fulana,vikofia na khanga wanazogawa hawa CCM ,ikataeni CCM ,musiipe kura CCM ,wananchi hawa hawa ambao leo wanafukuzwa kwenye vyuo ,wanabaguliwa kwenye posho na misaada malipo baadae ,hawa hawa ndio waliopigia kura CCM na naamini huenda 2010 wakaipa tena kura CCM, hawa ndio wale wasio sikia la mkuu ,hawa ndio wale wa majuto ni mjukuu .
  Katika hotuba za Lipumba wakati akirapu katika kujieleza iwapo wananchi waliowengi watamchagua kuingia ikulu na kuwa Raisi wa nchi ,Mh.Lipumba aliahidi mlo kwa wanafunzi wote ,mlo ambao utapatikana shuleni tena wanafunzi watakula bure ,hivyo hivyo aliahidi elimu bure kuanzia ya msingi hadi ya juu ,mwanafunzi hatadaiwa senti moja hadi anamaliza masomo yake au awe amechoka mwenyewe katika kutafuta elimu ,Je leo kama Lipumba angekuwa ni Raisi hamuoni haya majuto yasimkuta mwanafunzi hata mmoja.
  Jamani mabilioni yalioibiwa haya yangetosha kuwasomesha wanafunzi wote waTanzania na kuwapa mahitajio yote watakayohitajia bila ya mikwaruzano.
  Majuto ni mukuu ,hongera Wapemba kwa kuikataa CCM milele.mnapo pa kukamata lakini hawa walioipa kipau mbele CCM sijui watanamlilia nani maana hawalielewi walitendalo ?
   
 10. DDT

  DDT Member

  #10
  Nov 14, 2008
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu
  Usicheze na populisti, hizo ni mbinu za kuzuia waosha vinywa wa kijamii
   
 11. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #11
  Nov 14, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Waswahili wanasema ishi uone. This will go down in the history books. Lakini kubwa hapa naona ni rais wetu kutafuta sympathy ya wananchi wa huko Mbeya kwa ujumla. Maana walimpiga mawe kipindi kile. Sasa amerudi huko kwa style ya kuomboleza ili angalau wamuonee huruma. Its very dissapointing kumuona kiongozi wa nchi akiwa anafanya cheap politics kama hizo. Sijui uhusiano wake na marehemu ulikuwaje (nje ya kazi), lakini hakuwa na sababu ya msingi ya kuhudhuria ibada mbili za mazishi. Huyu ni kiongozi wa nchi jamani. Mbona ajiaibisha hivi? Wananchi wa Mbeya hawawezi kununuliwa kwa rais kwenda kwenye msiba. Thats very cheap. Ningependa kuona wapinzani wanacapitalize kwenye hili. Ningependa wananchi wa Mbeya watoe fundisho kwa CCM kama ilivyokuwa kule Tarime. Ningependa watanzania wote tuamke na kusema sasa basi kwa utawala mbovu wa CCM.
   
 12. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #12
  Nov 14, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa watanzania wanatakiwa wato fundisho kubwa sana kwa serikali iliyo madarakani manake mwezi huu peke yake mambo kibao yametokea angalia vyuo vimefungwa , wale wazee wa afrika mashariki walileta balaa kule town , ripoti ya vifo tabora hatuioni na hata katika hotuba yake raisi hakutilia maanani jambo hivi pamoja na mengine mengi
   
 13. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #13
  Nov 14, 2008
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kingine kilichonishitua ni kukodi ndege sita kwa ajili ya kupeleka mwili na waombolezaji mbeya, inasound kama "Helikopta 2" za Tarime vile. Hii ni dalili mbaya na wabunge wote kwa nguvu zao lazima wakemee kauli ya ngeleja kuhusu kumuenzi mbunge baada ya kufa kwa kupeleka miradi, "hii inaweza leta dhana kwa wananchi kuwatoa kafara wabunge wao" ili serikali ipeleke miradi. Usiniulize kafara kivipi wabunge wenyewe wanajua ungaunga style.
   
 14. isambe

  isambe JF-Expert Member

  #14
  Nov 14, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 2,053
  Likes Received: 881
  Trophy Points: 280
  Ndio hivyo tena wanashtuka wakati chupi iko magotini!!!
   
 15. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #15
  Nov 15, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Vipi, je alihudhuria mazishi ya Mheshimwa Wangwe huko kijijini Tarime pia?
   
 16. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #16
  Nov 15, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,968
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Kuanza kuhoji maneno ya kusikia kunaonyesha umbumbumbu wa mawazo.
   
 17. M

  Malila JF-Expert Member

  #17
  Nov 15, 2008
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Hivi hizi siasa za kibulicheka zitaisha lini? Ngeleja, hivi watu waliothubutu kumwonyesha rais wako kuwa hawamwelewi unaweza kuwadanganya kitoto hivi? Ngeleja najua unapita humu jf au wapambe wako wanakusomea.Nakushauri acha kudanganya watu. Wembe ni ule ule wa Tarime.
   
 18. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #18
  Nov 15, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Kuna mtu amesema mahali nafikiri ni 'Masatu" kwamba sheria mpya inakataza uchaguzi kufanyika ikiwa tuna miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu.
   
 19. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #19
  Nov 15, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280

  Duh! Huu ndio mfano murua kupita yote au?
   
 20. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #20
  Nov 15, 2008
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Duuh, kumbe mbunge akifa umeme unaletwa! Watu wa Rukwa barabara zenu mbovu miaka nenda rudi, kila hotuba ya bajeti waziri wa wizara yenye dhamana ya barabara anasema ipo kwenye mpango, au inafanyiwa upembuzi yakinifu !! Au hamtaki wabunge wenu waenziwe kwa barabara? Kazi kwenu!
   
Loading...