Malunde-Malundi
JF-Expert Member
- Jan 10, 2008
- 1,288
- 130
Kwanza nikupongeze kwa kauli nzito kama hii. Ni vizuri umelisemea hili la udini, maana nilidhani wanasingiziwa hawa jamaa. Kumbe hata ninyi wanasiasa mnakubaliana nalo huko kwenye vyama vyenu.
Pili, kama kweli kuna ukiukwaji wa sheria katika ujazaji wa hizo fomu, haijalishi ni nani anaweka pingamizi as long as amefuata taratibu zilizopo kisheria. Haya mambo ya kujifanyia mambo kiholela ndiyo yameifikisha hii nchi hapa mahali tulipo. Lazima tukubali kumeza machungu yatokanayo na kukurupuka kwetu bila kuangalia taratibu zikoje. Na kwa chama makini, linapotokea kosa la kiufundi kama hilo suluhu siyo kukimbilia kulaumu waliokuwekea pingamizi ama sheria iliyopo ila ni kujipanga upya ili kesho na keshokutwa haya yasijitokeze. CUF wana haki kabisa ya kuweka pingamizi kwa vile ni chama cha siasa cha upinzani dhidi ya vyama vingine vyote vyenye usajili hapa nchini. Haya mambo ya kujitengenezea sijui muungano wa vyama ni upumbavu tu, labda viamue kujiua na kuunda chama kimoja ndipo nitawaelewa.
Suala la tatu ni hivi: Hao wagombea wa vyama vingine waliapishwa na nani iwapo ilikuwa vigumu kwa mgombea wa Chadema kupata mahali halali (kwa sheria za uchaguzi) pa kwenda kuapa kwa kisingizio cha siyo siku ya kazi?
Na je, ni kwa nini hakuna aliyelalamikia kwamba fomu za wagombea zisingeweza kurudishwa siku hiyo kwa vile ingekuwa vigumu kwa wahusika kukamilisha matakwa ya kisheria ikiwemo ni pamoja na kuapa kwa mamlaka halali? Hii yote ni kwa sababu ya kukurupuka tu bila kuwa makini.
MKuu; viapo vyangu vya chuoni kusoma; kwenda nje; kiwanja; shamba; mkopo wangu vyote sikwenda kwa Hakimu wilaya- je ni batili- maanake mamlaka zote hizo zinafanya kazi kinyume? kiapoa cha uchaguzi kina sheria yake? mnijuze jamani sio ushabiki maana hapa ni sheria tu