Mbeya vijijini: Kampeni, uchaguzi na yatokanayo

Mbona wewe hauhitaji chakula cha msaada? Imekuwaje ukaweza kula milo zaidi ya mmoja kwa siku?

Ilongo; du ni kweli kabisa umenipa somo zuri enzi zile za utaratibu wa kisheria na hatima ya Chadema; na ulivyo-spot ndivyo tume ilivyoamua; lakini unanipa wasi wasi kama swala la kupanuka kwa pengo kati ya maskini wengi na matajiri wengi hulijui; huenda labda hujafika Tanzania kwa kipindi; hali iko hivyo; ila cha msingi hayo mambo na mengineyo kama vile ufisadi (umeenea mno sasa), kutokujali na kusikilizwa kundi kubwa la maskini; wanasiasa kuegemea Mjini tu na kuwasahau wapi kura wao ni mambo ambayo sasa Chifu kayaona; hakika kama sisi tuna malengo mazuri na nchi yetu; watu hawa tungeanza kuwachagiza sasa ili kupata hatimaye timu inayoweza kudai haki yake pale ilipopotea(iwe kwa makusudi au kwa sheria zisizokidhi haja ya wengi ya mkoloni). Nafikiri kumkatisha tamaa huyu chifu kweli sidhani kama tunamtendea haki; kuna vikongwe hata US wakati wa uchaguzi walijitokeza wazi kummunga mkono Barack (mkumbuke bibi aliyemtaja obana siku ya kukubali); hizi huwa tunu ktk jamii; maana naona tatizo lako ni Uchifu; mie tatizo langu ni kule kuanza kuona umhimu wa kudai haki panapotakiwa
 
Ilongo; du ni kweli kabisa umenipa somo zuri enzi zile za utaratibu wa kisheria na hatima ya Chadema; na ulivyo-spot ndivyo tume ilivyoamua; lakini unanipa wasi wasi kama swala la kupanuka kwa pengo kati ya maskini wengi na matajiri wengi hulijui; huenda labda hujafika Tanzania kwa kipindi; hali iko hivyo; ila cha msingi hayo mambo na mengineyo kama vile ufisadi (umeenea mno sasa), kutokujali na kusikilizwa kundi kubwa la maskini; wanasiasa kuegemea Mjini tu na kuwasahau wapi kura wao ni mambo ambayo sasa Chifu kayaona; hakika kama sisi tuna malengo mazuri na nchi yetu; watu hawa tungeanza kuwachagiza sasa ili kupata hatimaye timu inayoweza kudai haki yake pale ilipopotea(iwe kwa makusudi au kwa sheria zisizokidhi haja ya wengi ya mkoloni). Nafikiri kumkatisha tamaa huyu chifu kweli sidhani kama tunamtendea haki; kuna vikongwe hata US wakati wa uchaguzi walijitokeza wazi kummunga mkono Barack (mkumbuke bibi aliyemtaja obana siku ya kukubali); hizi huwa tunu ktk jamii; maana naona tatizo lako ni Uchifu; mie tatizo langu ni kule kuanza kuona umhimu wa kudai haki panapotakiwa


Ndugu yangu Malunde-malundi,

Mimi nipo nipo tu hapa nyumbani. Kwa hiyo nafuatilia vema hali ya Taifa letu.

Well, huyo chifu nina tatizo naye kwa sababu najua haelewi sheria inasemaje. Kwa hiyo inawezekana naye anadhani Chadema wameonewa. Lakini kama angekuwa anatoa ushauri kwamba tugange yajayo, hapo sina tatizo naye kabisa.

Kuhusu mlo mmoja kwa siku (maana yake watu wana njaa, siyo), ni suala la kuangalia kwa mapana zaidi na nadhani linahitaji "thread" yake mahsusi ... Nimekuwa nikipitiapitia humu ndani kutafuta "thread" inayoongelea suala hili sijaiona ingawaje nadhani Mzee Mwanakijiji alianzisha mojawapo kuhusu Hotuba ya Rais Kikwete ya Disemba 2008.

Unajua ndugu yangu, mimi hadi leo hii sielewi ni kwa nini mtu binafsi na familia yake ashindwe kujitosheleza kwa chakula (iwapo kama hakuna maafa ya kiasili kama ukame n.k., ama hao wahusika hawajaathirika kwa njia yoyote inayoweza kuwalazimisha washindwe kujihudumia). Watu wa aina hiyo siwezi kuwaonea huruma hata kidogo.
 
Date::1/9/2009
Pingamizi la CUF kwa Chadema lawagawa wapinzani
Salim Said na Latifa Karugila
Mwananchi​

PINGAMIZI lililowekwa na Chama cha Wananchi (CUF), dhidi ya mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Sambwee Shitambala, limeongeza ufa kwenye ndoa ya wapinzani, baada ya Chadema kutangaza rasmi kujitoa kwenye umoja wa vyama hivyo.

Wakati vyama vya CUF, NCCR-Mageuzi, Tanzania Labour (TLP) na PPT Maendeleo vikikutana jana na kutangaza nia ya kumwunga mkono mgombea wa CUF katika uchaguzi mdogo wa Mbeya Vijijini, Daudi Mponzi, Chadema imesema haipo tayari kuungana navyo kwa kuwa umoja huo ni wa kinafiki.

CUF na Chama Cha Mapinduzi (CCM), vilimwekea pingamizi mgombea wa Chadema na kufanikiwa kumwondoa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi huo ulioitishwa kuziba pengo lililoachwa wazi na Richard Nyaulawa aliyefariki dunia baada ya kuugua muda mrefu.

Mbali na kugoma kuhudhuria kikao cha vyama hivyo kilichofanyika Buguruni makao makuu ya CUF, Chadema ilieleza msimamo wake kwamba kamwe hakitamwunga mkono mgombea huyo wa CUF kwa kuwa umoja huo una mashaka.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema katika kikao hicho kuwa Alimwandikia barua mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kutaka chama chake kimwunge mkono mgombea wa CUF, lakini Mbowe hakujibu barua hiyo.

"Nilimwandikia barua Freeman Mbowe na kumwomba kutuunga mkono katika uchaguzi mdogo wa Mbeya Vijijini lakini hakunijibu. Hivyo hatukumwalika katika kikao hicho kwa kuwa hatujui nia yake, kama ana nia ya kutuunga mkono au la," alisema Profesa Lipumba.

Wenyeviti hao waliokutana ni Profesa Lipumba (CUF), James Mbatia (NCCR-Mageuzi), Agostine Mrema (TLP); na Peter Mzirai (PPT Maendeleo) huku Freeman Mbowe ambaye awali alikuwa hakosi katika vikao kama hivyo kutoonekana.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa alisema, hana hakika kama chama chake kimealikwa kwenye mkutano huo, lakini hata kama wangealikwa wasingehudhuria kwa kuwa ndoa hiyo ni ya kinafiki.

Alifafanua kwamba, wao walishasema na hawatabadilisha msimamo wao wa kutoshiriki vikao vya muungano huo kwa kuwa hakuna umoja wa dhati.

"Siwezi kuzungumzia suala la kualikwa au kutoalikwa, lakini hata kama tungealikwa tusingehudhuria kwa sababu sisi tunaungana na vyama makini vyenye ukweli na sio muungano wa kinafiki, kudanganyana na kuwadanganya Watanzania, muungano wa kuchekeana mchana na kupigana visu usiku," alisema Dk Slaa.

Awali, akifungua kikao cha jana, mwenyekiti wa CUF Profesa Lipumba alisema, wananchi wana kila sababu ya kuking’oa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na ugumu wa maisha na kutokuwepo kwa haki nchini.

"Tuna uhakika kupitia ushirikiano huu kwamba, CCM haina tena chochoro za kupenyea Mbeya Vijijini na Daudi Mponzi atakuwa mbunge wa jimbo hilo," alijigamba Profesa Lipumba.

Naye Mwenyekiti wa TLP, Agostine Mrema alisema, uchaguzi wa Mbeya ni mtihani wao wote na si wa CUF pekee kwani aibu ya kushindwa ikitokea si ya kwao tu bali ni ya wapinzani wote.

"CUF na TLP vina mtandao mzuri sana Mbeya Vijijini hivyo cha msingi ni kushirikiana wote ili kuimarisha mtandao huo badala ya kupoteza kura kwa hasira za kijinga na ubabe, tunaomba wananchi wasipige kura za maruhani na wasigomee uchaguzi bali tumpigie Mponzi," alisisitiza Mrema.

Alisema, kazi ni ngumu na safari bado ni ndefu kuelekea Ikulu kwa hiyo tusijisahau CCM hatujaikamata popote kinachoendelea ni sawa na siafu aliyepanda mgongo wa tembo.

"Kwa hiyo, piga ua garagaza, lakini Mponzi ashinde uchaguzi wa Mbeya Vijijini," alihamasisha Mrema.

Peter Mzirai, Mwenyekiti wa PPT Maendeleo taifa, alitamka wazi kuwa chama chake kina muunga mkono Mponzi na kwamba wako tayari kushirikiana katika kampeni Mbeya Vijijini.

"Tuligundua kuwa, CUF iko juu Mbeya na ina kura nyingi sasa sisi kazi yetu ni kuongezea tu katika zile kura za CUF ili Mponzi ashinde. Hivyo salamu zetu kwa CCM ni kwamba 2010 ni serikali ya mseto au CCM kung'oka," alitamba Mzirai.

Ndoa ya wapinzani nchini iliingia doa katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Tarime mjini ambapo baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa vyama vilivyomo ndani ya ndoa hiyo walikuwa wakijibizana, kulumbana na hata kuhujumiana.
 
Mkandara,
Swala la kwamba sheria zina mapungufu linajadilika lakini mpaka litakapojadiliwa na kufanyiwa marekebisho kwa kufuata taratibu husika ambayo kwa nchi yetu ni kupitia bunge bado sheria inakuwa sheria tu,Sasa yote yaliyofanyika mpaka sasa ni kwa mujibu wa sheria iliyopo na sheria hiyo hiyo ndiyo iliyotoa fursa kwa CHADEMA Kukata rufaa,kwa mtazamo wangu bado sheria inafuatwa na haki itapatikana kwa vyombo husika kwa mujibu wa sheria kuona nani ana haki kwenye hili.
Hizi sheria zilikuwepo na chaguzi zote zilifanyika kwa sheria hizi sasa iweje leo kwasababu kuna pingamizi ambalo limewekwa kwa mujibu wa sheria hizo hizo tulizozikubali kuingia nazo kwenye Uchaguzi ionekane haifai baada ya pingamizi.
Kuhusu swala la walioweka pingamizi wamejuaje mbona hii si siri hata hao wagombea wanaelewa kwamba kila kitu kinaanikwa na kuna muda wa pingamizi sasa haijali pingamizi imewekwa na nani ?iwe chama,mfuasi wa chama ,mwanachama wa chama fulani au hata mpiga kura wa jimbo husika ana haki ili mradi wote niliowataja wawe kisheria wanaruhusiwa kupiga kura ktk jimbo husika.Majuu wana sheria zao nasi tuna za kwetu lakini iwe majuu au kwetu bado sheria ni sheria hata kama ina mapungufu mpaka pale itakapofanyiwa marekebisho na inatakiwa kufuatwa.
Huko nyuma wakati nachangia hili nilieleza kwamba hatujifunzi kutokana na makosa ili kuhakisha tunarekebisha ili isitokee tena.Sasa huko bungeni wapinzani na chama tawala ni wakikilishi wetu ikiwemo wa chadema kadhaa ,je ni lini walipeleka angalau mswada wa kuomba marekebisho wa sheria hii au sheria kibao ambazo zinamapungufu wao ni kukalia kula posho na kulalamika kupitia vyombo vya habari hili si suluhisho bado walikuwa na uwezo kisheria angalau wa kuandaa mswada na kufikishwa bungeni na kama kukwama ukwame huko hapo angalau tungeweza kuona walijitahidi kufanya angalau kitu cha maana kama tulivyoona jitihada zao kwenye Ufisadi,Lakini tunangoja tukichemsha na sheria kuchukua mkondo wake na kuanza ulalamishi.Hebu tuwaulize kina Mh Dr Slaa,Mh Zitto na wabunge wengine kama wao wakati wanarudisha hizo fomu kama hawakuapishwa kwa hakimu?Utetezi wao wa awali unaonyesha wazi kwamba walielewa hili lakini kwa kutokua makini na kupanga tarehe ya kikao cha kumpitisha mgombea kugongana na sikukuu na kutokuwa na uwezo wa kumpata hakimu kutokana na kuwa si siku ya kazi, ndiyo walitafuta njia ya mkato au mbadala ili kuweka doubt kwenye sheria tata,Si mbaya ilikuwa strategy nzuri kwa wakati husika na ndiyo mpaka sasa kisheria bado wapo mguu moja ndani na uamuzi utakaofikiwa wa rufaa kama utawapatia wao haki watashiriki lakini wakishindwa vile vile waelewe wana sehemu yao ktk hili na hata wakishinda iwe fundisho na waanzie hapo kupitia wabunge wao ambao tayari wapo bungeni kuandaa mjadala wa mswada wa mabadiliko ya sheria tata zote ikiwemo hii ya uchaguzi.

wachambuzi wapo ,sema ambao ni popular kwa sasa ni Edo na Dauda
 
Back
Top Bottom