Mbeya na mambo yao

mkuu una kumbukumbu safi niliwahi kukaa nzovwe miaka ya 80 hayo uliyoeleza yalikuepo,kuna visa vingi sana niliviona,km mvua ikinyesha tulijipanga barabarani hapo nzovwe ilikua lazima ajali itokee,pia kulikua na kundi la washkaji zake jombi kina kibo nao walikua mtata,wababe huo mkoa usiulize sikumoja mdogo wao kibo alimninginiza mwanae nzovwe sokoni kataka kumchinja live mbele ya umati wa watu,fununu zikaja kwamba ndio alikua mkuu wa wachinjaji na wachunaji forest,mara ya mwisho nasikia kibo mwingine alitaka kulipua hicho kitongoji nzovwe kwa bomu akaghairi akajiua mwenyewe,na jombi alikuja kamatwa itigi huko kwa oda ya rais baada ya kupora mbeya,huko kote umetaja umesahau nzovwe mkuu pale ndo ilikua kitongoji cha uharamia,ukikusanya watoto wa sokolo,mbembela,mzee kalongoti*hatari zaidi*,kibo,mwamwaja,tunyande,kina chande na jairo,yani ilikua baraa,jombi wafuasi wake wote alitoa nzovwe na walikua watu wa kazi kweli,lakini sidhani kama kuna mmojawapo aliishia pazuri

huyo mzee kwenye red aliwahi kukutwa na sufuria kuubwa limejaa nyama ya binadamu,mikono miguu,etc alikua anaaminika kwa uchawi,sijui alikufa kifo gani
 
Kuna mzungu alioa mwanamke wa kinyakyusa yule mzungu alimnunulia mkewe gari basi yule mama alishukuru kwa kilugha: ndanga fijo, mzungu akajua mkewe anamwambia anataka pijo akamnunulia pijo yele mama akasema ndanga fijo na loli: mzungu alibaki ameduaaa kuwa anataka na loli?

hahaaaa umeniacha hoi maana naona mzungu aliona mwishowe itakua ndaga fijo na meli.
 
Haya ni baadhi tu ya mambo yaliyowahi kutokea huko Mbeya.
  • Eneo la Forest kulikuwa na msitu mkubwa ambako mauji yalikuwa yakifanyika kila uchao.
  • Eneo la soweto kulikuwa na wachinjaji, kila mara miili ya watu waliochinjwa ilikuwa ikukutwa eneo hilo.
  • Nonde ni kitongoji kilichopo Mbeya mjini, ila kimekaa kama kiko maili elfu tatu kutoka mjini. Bangi inavutwa hadharani kuanzia kwenye ngazi ya familia. Huko kazi yao kubwa, kinababa ni kuchinja ng'ombe na wanawake kufanya biashara ndogondogo soko la Mabatini. Kiongozi asiye rasmi aliyewahi kusimika bendera na kudai kuwa Nonde ni nchi yake alikuwa ni Baunsa mchinja ng'ombe maarufu akiitwa Mwasimba.
  • Jombi alikuwa ni jambazi maarufu zambia na tanzania akiteka magari, kupora magari na mali za watu.Alikuwa akitoa taarifa kabla hajafanya uhalifu wake. Wazungu wa Denmark waliokuwa wakifadhili mradi wa maji danida walikatisha msaada wao baada ya Jombi kuua na kubaka mke wa mkurugenzi wa mradi huo. Mkapa akatoa amri kuwa jombi akamatwe. Vikosi maalum ndio vilivyoenda kumkamata jombi.
  • Mbeya kuna makanisa mengi sana yenye majina ya Kiingereza, Kiswahili, Kinyiha, Kisafwa, Kimalila na Kikimbu. Makanisa mengi na uovu mwingi vyaenda sambamba.
  • Waimbaji wa nyimbo za injili wanaovuma wengi wao wana asili ya Mbeya.
  • Pombe ya kadansana ilikuwa maarufu sana mwaka 2000, haijuulikani ilikokuwa ikitokea. Ilikuwa ikiua sana watu, na watu waliendelea kuishabikia hadi ilipogundulika kuwa inatoka Malawi, ikapigwa marufuku kabisa.
  • Mauaji na uchunaji wa ngozi uliwatisha sana watu waishio nje ya mkoa wa Mbeya, Mbeya hali ilikuwa shwari kabisa.
  • matukio ya kupigana na nondo ilikuwa gumzo sana mwaka juzi na mwaka jana, wengi walijeruhiwa.
  • Leo Mbeya kuku na nguruwe wananenepeshwa kwa dawa za kuzuia makali ya ugonjwa wa ukimwi.
  • Pombe inayoitwa kiduchu ndio sasa iko kwenye midomo ya watu. lmeacha gumzo kwa kuwa ukiiweka kwenye chupa inavimbisha chupa hadi inapasuka. pombe hiyo inahifadhiwa kwenye vyungu.Ni ya hatari lakini wana Mbeya wanaendelea tu kuinywa.
  • Kuna vivutio kibao vya utalii lakini havitangazwi, sijui ni kwanini.
  • Pichani ni kijana Peter muongoza watalii akijipumzisha baada ya kazi ngumu ya kutwa nzima.
  • 2338502-Peter_after_a_hard_days_work-Mbeya.jpg
Bujibuji bana umenikumbusha kukaja,Mbeya bana balaa,umesahau kuwa wanawake wa mbeya wengi ni Kalolait na wana ndevu kama maruhum Osama,pia ndio wa kwanza kumpopoa na kuzuia msafara wa baba wa kaya
 
Kitu kimenikuna kuliko vyote kwenye hii mada ni hii picha hapa chini. Ubarikiwe sana uliyeiweka.

Mie nikiwa Bongo huwa sikubali kabisa kula wali kama si wa Mbeya. Wa Shinyanga wanachanganya mchanga, kwa hivyo hata bure siutaki.

Ila kuna dosari moja kubwa: Kwanini Mbeya hamna gazeti? Hamjui umuhimu wa kuwa na gazeti? Arusha wanalo Arushatimes, na linawapatia umaarufu na kuinua biashara zao, hasa za utalii. Anzisheni gazeti. Msiogope. Mnaweza. It's is the best way to promote yourselves.

IMG_5284.jpg
 
ascofu Mwakasege,
prof Mwandosya,
Mwakyembe,
Bahati Bukuku,
cpwaa,
sugu,
wengine nimewasahau,
 
daah mby co mchezo ukiongelea kimichezo mbeya enzi hizo ilikuwa mbali sana,
Nakumbuka enzi zile ligi ya tanzania bara ilipokuwa bora huku tukuyu starz,kule prisons na tiger na meko!ndani ya sokoine stadium ilikuwa ni burudani sana,
Mkuu pia kuna ligi ilikuwa inapigwa pale UWANJA NGOMA daah ilikuwa ni noma sana vijana wengi sana wamekuwa wachezaji wakubwa nchi hii toka uwanja ngoma,kama kina fuso,mwamanda samson,mgaza na wengine kibao!
Nakumbuka kama hood ye2 ya ghana tulikuwa na timu ze2 mazoezi pale mbata huku sarakasi kwenye mapululiro huku vijana wanapasha,watoto wa kishua enzi zile walikuwa na timu yao saitama ya uzunguni kwa mzee samatta(r.i.p),af kulikuwa na snow white,dah by dat tym ukiongelea soka basi hii ndo ilikuwa ndo 2po ktk peak ya soka!
Leo maisha yamechange sana kila mtoto akizaliwa anafikiria kupaka powder,kujipiga scrub na kwenda club michezo atacheza saa ngapi?tena ctashangaa kuckia leo pale uwanja ngoma kuna stage wa2 wanafanya show!
Daah nilisahau ishu ya kupanda mlimani kwenda kula mang'ang'a after then 2nashukia loleza high school kuwaona dada zetu hahaha
 
Mgodi wa makaa ya mawe uko mbeya
Gesi nyingi na safi inapatikana mbeya
Migodi midogo ya dhahabu mbeya
Kiwanda kizuri ca cement mbeya
kimwondo kilichoanguka mbeya
Shule nzuri a nyingi sana za sekondary za private mbeya
wasomi wengi wanapatikana/wametokea mbeya
hoteli nzuri na za kisasa zipi mbeya
international airport wanataka kuizuia mbeya
madini(gemstone-pandahill) ambayo hayapatikani sehemu nyingine duniani
watu wakarimu zaidi wanaparikana mbeya
kitu gani nimesahau, yes hospital ya rufaa siyo kitu kidogo
bonde la ufa na matetemeko ya ardhi-mbeya
ziwa nyasa-lenye mawimbi makali


kwanza niendelee kukumbuka ....


1. Waberoya anatoka Mbeya
2. Mbeya is among the giant mikoa ktk uzalishaji wa chakula cha binadam
3. Mtu aweza kupita Mbeya kwenda Zambia, Malawi na Zaire
4. Maziwa na mito mingi ya kuvutia isiyo kauka kwa takribani majira yote ya mwaka ipo Mbeya
5. Mawaziri Mark Mwandosya na Harison Mwakyembe chanzo cha maradhi yao kinaisikitisha sana Mbeya
6.
 
Kuna Mto unaisihia kwenye chungu ,pale Inyala karibu na TAZAMA pipeline uliwahi kutupwa mpira ukaenda kutokea ziwa tanganyika inaaminika mto unaishia kwenye mkondo wa bonde la ufa hiyo ndio mbeya
Mashamba makubwa ya mpunga usangu na mbarali utapenda madhari ya bonde
Kila wilaya ya mbeya ina mabonde na uwanda mkubwa sanaaa kwa kilimo kizuri ,chunya,Kyela,mbarali mbozi utapenda kwa kwa kweli
Wanake wa mbeya ni wajasiriamali waliokubuhu tangu enzi hizo za kusafirisha malori ya ndizi nchi nzima
 
95 percent ya kokoa inayozalishwa tanzania inatoka kyela-mbeya. Ila na ukwimwi kanaongoza huko
 
1. Waberoya anatoka Mbeya
2. Mbeya is among the giant mikoa ktk uzalishaji wa chakula cha binadam
3. Mtu aweza kupita Mbeya kwenda Zambia, Malawi na Zaire
4. Maziwa na mito mingi ya kuvutia isiyo kauka kwa takribani majira yote ya mwaka ipo Mbeya
5. Mawaziri Mark Mwandosya na Harison Mwakyembe chanzo cha maradhi yao kinaisikitisha sana Mbeya
6.

6.Penguine anatokea Mbeya
7. wanawake wenye uasili halisi wa ubantu wanatokea mbeya..wazuri I mean,,
8.Sugu anapatikana Mbeya
9.
 
Hata big brother wa kwanza si alitoka mbeya?! - kwanza Mwampamba!, mwisho mbeya.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom