Mbeya na mambo yao


Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
42,580
Likes
38,994
Points
280
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
42,580 38,994 280
Haya ni baadhi tu ya mambo yaliyowahi kutokea huko Mbeya.
 • Eneo la Forest kulikuwa na msitu mkubwa ambako mauji yalikuwa yakifanyika kila uchao.
 • Eneo la soweto kulikuwa na wachinjaji, kila mara miili ya watu waliochinjwa ilikuwa ikukutwa eneo hilo.
 • Nonde ni kitongoji kilichopo Mbeya mjini, ila kimekaa kama kiko maili elfu tatu kutoka mjini. Bangi inavutwa hadharani kuanzia kwenye ngazi ya familia. Huko kazi yao kubwa, kinababa ni kuchinja ng'ombe na wanawake kufanya biashara ndogondogo soko la Mabatini. Kiongozi asiye rasmi aliyewahi kusimika bendera na kudai kuwa Nonde ni nchi yake alikuwa ni Baunsa mchinja ng'ombe maarufu akiitwa Mwasimba.
 • Jombi alikuwa ni jambazi maarufu zambia na tanzania akiteka magari, kupora magari na mali za watu.Alikuwa akitoa taarifa kabla hajafanya uhalifu wake. Wazungu wa Denmark waliokuwa wakifadhili mradi wa maji danida walikatisha msaada wao baada ya Jombi kuua na kubaka mke wa mkurugenzi wa mradi huo. Mkapa akatoa amri kuwa jombi akamatwe. Vikosi maalum ndio vilivyoenda kumkamata jombi.
 • Mbeya kuna makanisa mengi sana yenye majina ya Kiingereza, Kiswahili, Kinyiha, Kisafwa, Kimalila na Kikimbu. Makanisa mengi na uovu mwingi vyaenda sambamba.
 • Waimbaji wa nyimbo za injili wanaovuma wengi wao wana asili ya Mbeya.
 • Pombe ya kadansana ilikuwa maarufu sana mwaka 2000, haijuulikani ilikokuwa ikitokea. Ilikuwa ikiua sana watu, na watu waliendelea kuishabikia hadi ilipogundulika kuwa inatoka Malawi, ikapigwa marufuku kabisa.
 • Mauaji na uchunaji wa ngozi uliwatisha sana watu waishio nje ya mkoa wa Mbeya, Mbeya hali ilikuwa shwari kabisa.
 • matukio ya kupigana na nondo ilikuwa gumzo sana mwaka juzi na mwaka jana, wengi walijeruhiwa.
 • Leo Mbeya kuku na nguruwe wananenepeshwa kwa dawa za kuzuia makali ya ugonjwa wa ukimwi.
 • Pombe inayoitwa kiduchu ndio sasa iko kwenye midomo ya watu. lmeacha gumzo kwa kuwa ukiiweka kwenye chupa inavimbisha chupa hadi inapasuka. pombe hiyo inahifadhiwa kwenye vyungu.Ni ya hatari lakini wana Mbeya wanaendelea tu kuinywa.
 • Kuna vivutio kibao vya utalii lakini havitangazwi, sijui ni kwanini.
 • Pichani ni kijana Peter muongoza watalii akijipumzisha baada ya kazi ngumu ya kutwa nzima.
 
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined
Aug 3, 2008
Messages
12,673
Likes
5,076
Points
280
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined Aug 3, 2008
12,673 5,076 280
Mgodi wa makaa ya mawe uko mbeya
Gesi nyingi na safi inapatikana mbeya
Migodi midogo ya dhahabu mbeya
Kiwanda kizuri ca cement mbeya
kimwondo kilichoanguka mbeya
Shule nzuri sana za sekondary za private ziko mbeya
wasomi wengi wanapatikana/wametokea mbeya
hoteli nzuri na za kisasa zipi mbeya
international airport wanataka kuizuia mbeya
madini(gemstone-pandahill) ambayo hayapatikani sehemu nyingine duniani
watu wakarimu zaidi wanaparikana mbeya
kitu gani nimesahau, yes hospital ya rufaa siyo kitu kidogo
bonde la ufa na matetemeko ya ardhi-mbeya
ziwa nyasa-lenye mawimbi makali


kwanza niendelee kukumbuka ....
 
Next Level

Next Level

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2008
Messages
3,158
Likes
22
Points
135
Next Level

Next Level

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2008
3,158 22 135
Mgodi wa makaa ya mawe uko mbeya
Gesi nyingi na safi inapatikana mbeya
Migodi midogo ya dhahabu mbeya
Kiwanda kizuri ca cement mbeya
kimwondo kilichoanguka mbeya
Shule nzuri a nyingi sana za sekondary za private mbeya
wasomi wengi wanapatikana/wametokea mbeya
hoteli nzuri na za kisasa zipi mbeya
international airport wanataka kuizuia mbeya
madini(gemstone-pandahill) ambayo hayapatikani sehemu nyingine duniani
watu wakarimu zaidi wanaparikana mbeya
kitu gani nimesahau, yes hospital ya rufaa siyo kitu kidogo
bonde la ufa na matetemeko ya ardhi-mbeya
ziwa nyasa-lenye mawimbi makali


kwanza niendelee kukumbuka ....
Wabe........! humo kny bold ....mmmmmmmhh???
 
Baba_Enock

Baba_Enock

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
6,901
Likes
339
Points
180
Baba_Enock

Baba_Enock

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
6,901 339 180
Maharage mazuri yanapatikana Mbeya
Mpunga swaafi unapatikana Mbeya
Mkoa unaopakana na nchi zaidi ya moja Mbeya (na Kagera)
 
Jile79

Jile79

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2009
Messages
12,157
Likes
4,012
Points
280
Jile79

Jile79

JF-Expert Member
Joined May 28, 2009
12,157 4,012 280
Big four (feeder regions) mbeay namba one.
Kila kitu kinapatikana mbeya...
 
Next Level

Next Level

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2008
Messages
3,158
Likes
22
Points
135
Next Level

Next Level

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2008
3,158 22 135
Afu na weeee jiangalie....umekuwa edior siku hizi eeeh!!!
Mammmy.......just trying....ha!ha!ha!ha!ha!ha...umeona eeeeh?
 
Sipo

Sipo

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2008
Messages
2,146
Likes
41
Points
0
Sipo

Sipo

JF-Expert Member
Joined Jul 25, 2008
2,146 41 0
Big four (feeder regions) mbeay namba one.
Kila kitu kinapatikana mbeya...
I can agree with you, ni kweli kabisa hata wake wenye nidhamu na upendo wanapatikana Mbeya. I can prove this with evidence
 
babukijana

babukijana

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2009
Messages
5,512
Likes
2,006
Points
280
babukijana

babukijana

JF-Expert Member
Joined Jul 21, 2009
5,512 2,006 280
mkuu una kumbukumbu safi niliwahi kukaa nzovwe miaka ya 80 hayo uliyoeleza yalikuepo,kuna visa vingi sana niliviona,km mvua ikinyesha tulijipanga barabarani hapo nzovwe ilikua lazima ajali itokee,pia kulikua na kundi la washkaji zake jombi kina kibo nao walikua mtata,wababe huo mkoa usiulize sikumoja mdogo wao kibo alimninginiza mwanae nzovwe sokoni kataka kumchinja live mbele ya umati wa watu,fununu zikaja kwamba ndio alikua mkuu wa wachinjaji na wachunaji forest,mara ya mwisho nasikia kibo mwingine alitaka kulipua hicho kitongoji nzovwe kwa bomu akaghairi akajiua mwenyewe,na jombi alikuja kamatwa itigi huko kwa oda ya rais baada ya kupora mbeya,huko kote umetaja umesahau nzovwe mkuu pale ndo ilikua kitongoji cha uharamia,ukikusanya watoto wa sokolo,mbembela,kalongoti*hatari zaidi*,kibo,mwamwaja,tunyande,kina chande na jairo,yani ilikua baraa,jombi wafuasi wake wote alitoa nzovwe na walikua watu wa kazi kweli,lakini sidhani kama kuna mmojawapo aliishia pazuri
 
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined
Aug 3, 2008
Messages
12,673
Likes
5,076
Points
280
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined Aug 3, 2008
12,673 5,076 280
Wabe........! humo kny bold ....mmmmmmmhh???
athari za mshika mawili, napigana kumalizia thesis at the same time , nataka jukwaa liwe live! unawaza huku unaandika, inakuja point nyingine unaipandishia juu!!!, mara una click go! neeext thread!!ndio matokeo

thanks though
 
Next Level

Next Level

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2008
Messages
3,158
Likes
22
Points
135
Next Level

Next Level

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2008
3,158 22 135
athari za mshika mawili, napigana kumalizia thesis at the same time , nataka jukwaa liwe live! unawaza huku unaandika, inakuja point nyingine unaipandishia juu!!!, mara una click go! neeext thread!!ndio matokeo

thanks though
Don't worry Wabe......knew that mkuu!
 
Pretty

Pretty

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2009
Messages
2,581
Likes
53
Points
145
Pretty

Pretty

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2009
2,581 53 145
.......Vipodozi vingi vinapatikana Mbeya maeneno ya tunduma.
Kuna ndizi mbivu ndogo ndogo tamu sana zinapatikana Mbeya.
 
GM7

GM7

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2009
Messages
492
Likes
6
Points
35
GM7

GM7

JF-Expert Member
Joined Jun 26, 2009
492 6 35
Aisee Mbeya kuna hazina kubwa sana. Halafu ulisahau, kiwanda kikubwa cha bia na cha kisasa Afrika mashariki kinapatikana Mbeya, Viwanda vingine kama Cocacola, Pepsi n.k. vinapatikana Mbeya. Station nzuri ya garimoshi kama hii hapa kwenye picha na yenyewe inapatikana Mbeya.
 

Attachments:

Albedo

Albedo

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2008
Messages
5,565
Likes
25
Points
135
Albedo

Albedo

JF-Expert Member
Joined Feb 24, 2008
5,565 25 135
Ni mji ambao ifikapo saa mbili tu watu wanjifungia majumbani mwao sijui wanogopa Nondo au
 
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined
Aug 3, 2008
Messages
12,673
Likes
5,076
Points
280
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined Aug 3, 2008
12,673 5,076 280
Greenland!

Hii rutuba baraka tupu

 

Forum statistics

Threads 1,250,868
Members 481,514
Posts 29,748,830