Mbeya na mambo yao

sasa JOMBI ALIFUNGWA , YUko hai ama ? hii stori ya Jombi imeniacha kinywa wazi

Said Abinala a.k.a Jombi alifungwa baadaye akatoka,jamaa laishindikana kabisa huyu Mbeya na nadhani katika maisha yake hatamsahai Ex RPC wa Mbeya Laurian Sanya...Jombi aliishika sana Mbeya jamani nakumbuka Ex RPC wa Mbeya mzee Yohana Mapunda alistaafishwa kwa manufaa ya umma mojawapo ya sababu ikiwa ni kumkumbatia huyu Jombi
 
Kiwanda cha beer pale iyunga ie TBL tena ni state of the art techn
Vile vile daraja na chungu cha mungu kule kiwila
Volcanic mt ie Rungwe na Matema beach ie the only beautiful beach in southern highlands
 
........Kuna kijiji fulani huko Mbeya Ndolezi miaka hiyo ya zamani kimombo au nyota kilianguka pale, hadi leo watalii wengi huwa wanakwenda kukiona.
 
Watu wasiokua na huruma wanapatikana Mbeya, mfano waliokufa kwenye ajali ya mlipuko wa mafuta , badala ya kuwasaidia waliopata ajali wakawa wanachukua mafuta. Mbeya kuna kila kitu jamaniii
 
Jombi ni mzima kabisa na yuko pale Soweto (Mbeya). Ana gereji yake pale, ina jina la VETA, nadhani wanafunzi wa VETA wa auto mechanics wanajifunzia pale. Nilimkuta tarehe 26/12/2009 nilipokwenda kukarabati gari langu pale, yuko fiti kinoma.
Hata mie nilikuwa simfahamu hadi nilipooneshwa na watu kwamba ndio yeye, na wala sikujua kwamba ile gereji ni ya kwake.
bado nasisimka na hadithi za JOMBI, ANGALAU AMEKUA rAIA MWEMA, ukute Ufundi alijifunzia Mbeya, nikitoka Mpwapwa nataraji kwenda Mbeya, bila shaka nitamtafuta huko SOWETO.
 
bado nasisimka na hadithi za JOMBI, ANGALAU AMEKUA rAIA MWEMA, ukute Ufundi alijifunzia Mbeya, nikitoka Mpwapwa nataraji kwenda Mbeya, bila shaka nitamtafuta huko SOWETO.

Ukifika tu pale Soweto uliza gereji ya Jombi, utamkuta na yeye hapo hapo, yupo almost muda wote. Gereji yake iko mkabala na njia ya kwena Moondust Hotel! Kashakuwa mtu mzima sana na ni mpole sana, hata katika maongezi yake. Huwezi kumdhania kwamba ndiye eliyekuwa anautikisa mkoa kwa matukio ya ujambazi na utekaji magari. Anaitwa Saidi Abinala, ndio jina lake halisi!
 
Lawlence Mwalusako, Godwin Aswile, Ezekiel Greyson (Jujuman) .... go on, kocha maarufu enzi hizo kufundisha mpira kama wa brazil Dan Korosso anatoka Mbeya.
 
kingine muhimu sana ni kuwa Wazee wa Mbeya na hasa wanyakyusa wana busara sana. huwa makini sana katika maamuzi mengi sana hasa yanayohusu jamii. Na ukiangalia sana vijana wa Mbeya wanawaheshimu na kuwasikiliza watu waliowazidi umri. Hicho kinanikosha sana.
 
BARIDI kali kama la Europe lipo huko Mbeya.Jamani watu huwa hawaogi Mbeya kwa ajili ya baridi.Hasa mwezi wa 5 mpaka 7,usirogwe ukaenda Mbeya.Nasikia eti ndio chanzo kimojawapo cha ukimwi? sijui ni kweli.
 
Endapo marafiki na watu wa Mbeya wako wengi naomba mshike habari za maeneo ya mkoa huu. Enendeni wikipedia ya Kiswahili ambako makala fupi sana ("mbegu") zimeandaliwa kwa kila kata ya Mkoa wa Mbeya.
[ame]http://sw.wikipedia.org/wiki/Jamii:Mbegu_za_jiografia_ya_Mkoa_wa_Mbeya[/ame]
Hapa chagua mahala unapojua makala itafunguka.
Bofya tu "hariri" halafu ingiza habari za mahali na watu wake!
(Anza kuandika kabla ya ==Marejeo==)
 
_wsb_368x274_Mbeya+Peak+am+Morgen_85_1.JPG

Mitaa ya soko Matola... nyuma ni Mlima Mbeya.
 
Jamani mmesahau kitu kimoja pale tukuyu kuna sehemu kuna daraja la mungu lipo mto kiwira lipo kimaajabu sana nani amewahi kusikia?
 
Daraja la Mungu Mbeya
Maporomoko mazuri yenye mandhari safi - utafikiri "sitting room" KAPOROGWE Mbeya
Wanawake wenye vitambi Mbeya
Miguu ya Chupa Mbeya
Ulevi Mbeya............
Vyakula, matunda ya kila aina Mbeya
AAAAAAA Mbeya naipenda
 
Kuna mzungu alioa mwanamke wa kinyakyusa yule mzungu alimnunulia mkewe gari basi yule mama alishukuru kwa kilugha: ndanga fijo, mzungu akajua mkewe anamwambia anataka pijo akamnunulia pijo yele mama akasema ndanga fijo na loli: mzungu alibaki ameduaaa kuwa anataka na loli?
 
Msisahau hata ukimwi uliiingilia huko pia!

Enzi hizo ukiitwa Kizambia! teh teh teh by the way asili yangu ni pale Isange Mwakaleli, Tukuyu(inatamkwa TOKYO) ; Mbeya
 
Back
Top Bottom