Uchaguzi 2020 Mbeya Mjini kazi ipo kubwa

Oct 7, 2019
51
156
Leo DR Tulia ambaye Ni naibu Spika alikula Chakula Cha mchana kwa mamaNtilie Jijini Mb
eya. Kabla ya kuhitimisha vikao vya bunge alisema atagombea mwaka huu sisi HATUJUI ni Jimbo gani lakini niliwahi kuandika kuwa Sugu ASIMBEZE DR TULIA.... Niwakumbushe kidogo, bado msimamo wangu na analysis yangu katika Jimbo hili Kama watakutana Sugu na Dr Tulia unabaki vile vile.

Uchaguzi uliopita CCM tulitandikwa hapa kisawasawa mgombea wetu SAMBWEE Mwalyego Shitambala alipata kura 54,296 huku Mgombea wa Chadema Sugu akipata Mara mbili ya kura 108,566 karibia Mara mbili ya mgombea wa CCM.

Sugu 2015 alibebwa na vitu viwili vikubwa Moja uimara wa mgombea urais waliyekuwa naye Lowassa lakini cha pili Ni hulka ya majimbo ya mjini huwa yanatutesa Sana CCM.

2020
Vita ya kipindi hiki Ni ngumu kidogo kwa Sugu kutokana na aina ya Mgombea anayejipitisha pitisha jimboni. Dr Tulia uwezo wake Ni mkubwa na ana mvuto wa kisiasa kuliko mgombea wa CCM 2015. Mambo kadhaa yanayombeba Tulia Elimu yake, Kuna future mbele ya kuwa kiongozi mkubwa ukiachana na Ubunge anaweza kuukwaa uwaziri au hata Uspika kabisa hili Lina faida kwa wanambeya mnapopata mtoto wa kuingia kwenye Baraza la mawaziri si nafasi ya kuchezea, ground work kaifanya vizuri sana, kwa namna flan naye Ni mbishi kwenye Siasa sio mlaini Kama mgombea wetu wa 2015, Nguvu ingine ya Tulia Ni jinsia yake, Kama atacheza na mahitaji ya wanawake vizuri watambeba Sana kwenye uchaguzi.

Akiweza kuwaunganisha kundi hili atashinda kirahisi Sana mbeya. Mwisho kitakachombeba Ni Mgombea urais wetu Dr Magufuli, Dr Magufuli kwa Sasa kwa ukanda huu wa Afica mashariki amekuwa na Siasa za aina yake tutakuja kulichambua hili baadaye.

Kinachoweza kumwangusha kikubwa Ni kura za maoni hata Kama atapenya CCM Ina tabia ya kupasuka baada ya kura za maoni. Cha pili Ni Jimbo analogombea nimesema toka awali kuwa majimbo ya mjini sio Rafiki Sana kwa CCM.

Sugu yeye Ubora wake upo kwenye uanaharakati, tukumbuke huyu kiasili Ni mwanaharakati, Siasa za harakati zinapendwa Sana na Vijana. Kama vijana watajiandikisha wengi Mbeya CCM itapata wakati mgumu, Jambo la pili kwa sugu Ni kwamba yeye kizingiti cha Kura za maoni ameshakivuka huu Ni utaratibu wao kwenye chama, anaonekana hatashindanishwa na Mtu kutokana na maneno yake. Jambo la tatu Ni ulevi wa majimbo ya mjini katika Siasa za Upinzani hapa kutamnufaisha kuliko CCM.

UDHAIFU wake Ni ahadi alizotoa hajazikamilisha, yaani ukiacha maneno mengi anayoongea Sugu hakuna Mambo makubwa Sana aliyoyafanya atakayokumbukwa nayo. Pili Ni tabia ya vijana kutokupenda kupiga kura, anaweza kuwa nao wengi wa kumshabikia lakini siku ya kura wakakosa sifa ya kupiga kura, aina ya mgombea anayekutana naye mwaka huu Kama akipita Tulia ana nguvu kuliko yule aliyekutana naye 2015, kitu kingine ambacho atakutana nacho na kitamuathiri Ni Siasa za propaganda, Tukumbuke Sugu kwa Sasa kajiendeleza Sana kiuchumi ana vitega uchumi vingi mpaka hotel, maisha yake hayalingani na ya wamachinga wa pale Mbeya kwa Sasa hili CCM lazima walitumie na Tukumbuke hakuna urafiki Kati ya maskini na tajiri. Mwisho kabisa Ni nguvu aliyonayo Rais Magufuli kwenye Medan za kisiasa.
Sugu asichukulie Poa hili Jimbo la Mbeya litamponyoka Mambo sio marahisi Kama 2015. Ni tahira tu anayeweza kusema Sugu atashinda kwa asilimia au Tulia atashinda kwa asilimia. Kila mtu ana nafasi sawa ya kushinda hili Jimbo kwa Sasa (Equal chance).
Naelekea Mbeya....
 
Binafsi naamini mbeya ilistahili kuwa mbele sana kimaendeleo na hata kimuonrkano! Kuna mahali kitu hakiko sawa kwa viongozi. Labda huyu mheshimiwa apewe jimbo miaka mitano kama atalisogeza maana ana konection na juu, anaweza badili mji maana hata sio jiji. Sugu kashindwa, alichoweza ni kuwafanya baadhi ya wanambeya kuwa rebellion basi!
 
Uchaguzi uliopita CCM tulitandikwa hapa kisawasawa mgombea wetu SAMBWEE Mwalyego Shitambala alipata kura 54,296 huku Mgombea wa Chadema Sugu akipata Mara mbili ya kura 108,566 karibia Mara mbili ya mgombea wa CCM.
ANALYSIS YAKO NI NZURI, 54,296 SIYO NDOGO PAMOJA NA KUWA IKO CHINI, SUGU AKAZE BUTI SANA. ASIBWETEKE HATA KIDOGO, TUKO NA CHADEMA MPAKA KUFA
 
Chipesi Namisuku, nakutamani wewe!! Lakini huyu dada asiyekuwa na nyama huyu mwambieni aangalie asije akakimbia na pichu mkononi, mziki wa Sugu siyo wa polepole!
 
Tulia kushinda Mbeya Mjini anahitaji kubebwa wazi wazi na Magufuli na polisi, vinginevyo hana chochote cha kumshinda Sugu.
Mkuu Sugu alishawatangazia mapema kabisa kwamba mtiti utakaopigwa pale ni hatari! Wasije wakarogwa kuiba kura mchana kweupe, Mbeya siyo Shinyanga mjini ile àu siyo Muleba Kusini!
 
Watu wa Mbeya msirudi nyuma mmeshaonesha umma kuwa nyie ni watu imara na wapinzania wa siasa chafu za ccm. Mkirudia tena ccm tunawaondoa kati ya watu wa maana nchi hii.
 
Tulia hawezi shida, tusubiri uone, Kwanza Sugu still anapendwa sana Mbeya, watu sasa hivi sio wajinga hivyo, yaani uje miezi michache uanze kuwapa maneno matamu au vitu vichache kisha upate ubunge labda wananchi wangekuwa hawamtaki Sugu, ni ngumu sana kushinda Mbeya. Ukweli uko hivyo.
 
“Hulka ya majimbo ya mjini huwa yanatutesa Sana CCM” Mtu mwenye upeo kidogo tu hawezi kuchagua CCM huu ndio ukweli mchungu linchi Lina kila kitu lakini masikini kama Burundi aaahh
 
Binafsi naamini mbeya ilistahili kuwa mbele sana kimaendeleo na hata kimuonrkano! Kuna mahali kitu hakiko sawa kwa viongozi. Labda huyu mheshimiwa apewe jimbo miaka mitano kama atalisogeza maana ana konection na juu, anaweza badili mji maana hata sio jiji. Sugu kashindwa, alichoweza ni kuwafanya baadhi ya wanambeya kuwa rebellion basi!
Alikuwepo Prof.Mwandosa ambaye amekuwa Mbunge na Waziri! Vipi kuna maendeleo gani aliyoleta mkoa wa Mbeya?
 
Back
Top Bottom