Mbeya: Magari yanateketea kwa moto kijiji cha mwale Chimala

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Moto mkubwa unawaka muda huu kijiji cha mwale Chimala mkoani Mbeya malori ya mafuta yanateketea na moto chanzo cha ajali bado hakijulikani. Malori ya mafuta yanawaka moto ni balaa

Ni pale hapo stendi mpya karibu na dukani kwa Mama Pipo.

=====

MOTO WATEKETEZA MAGARI 6 NA NYUMBA 4 MBEYA

Taarifa iliyothibitishwa na Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Ayoub Sanga, imeelezwa kuwa Magari 6, Pikipiki 2 na Nyumba 4 zimeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo huko Chimala Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya

Diwani wa Kata hiyo, Charles Komba amesema moto huo ulianza majira ya saa nne usiku kutoka kwenye Lori lililokuwa limeegeshwa katika kituo maalumu cha magari maarufu kama Mama People

Zimamoto lilifika saa 6 usiku na kufanikiwa kuzima moto huyo ambao chanzo chake kimetajwa kuwa ni biashara holela ya mafuta ya Petroli na Dizeli iliyokuwa ikifanywa na madereva katika eneo hilo.

#JamiiForums #JFMatukio
 
Naona ni mtindo mpya sasa,wiki tatu zimepita gari ya mafuta ilichomwa inyala wanakijiji waliacha vitanda wakalala mtoni
 
Hiyo itakuwa kwamba alikuwa anaiba temperature akajisahau akawasha fegi.

Dhana tu.
 
Back
Top Bottom