Mbeya: Madereva watakiwa kubadilika ili kuepuka ajali za barabarani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa, Aprili 20, 2023 amewataka madereva wa vyombo vya moto kubadilika kufuatana na hali ya kijiografia yam ilima, miteremko pamoja na hali ya hewa ya Mkoa wa Mbeya yenye mvua na ukungu kwa kuhakikisha wanafuata na kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.

1.JPG
Ameyasema hayo katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani Mkoa wa Mbeya yaliyofanyika katika Stendi ya kabwe Jijini Mbeya, ambapo Beno Malisa alikuwa mgeni rasmi akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Comrade Juma Zuberi Homera.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Malisa amelipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani kitaifa mkoani mwanza.

2.JPG

mbye.JPG

Aidha, amepongeza jitihada zinazofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na kamati ya usalama barabarani katika kuzuia na kudhibiti ajali za barabarani kwani kitakwimu ajali zimepungua ukilinganisha na mwaka 2022.

Sambamba na hilo, Malisa amempongeza na kumshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zaidi ya Bilioni mia moja kwa ajili ya ujenzi na utanuzi wa barabara ya TANZAM Jijini Mbeya.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamin Kuzaga ambaye pia ni mlezi wa kamati ya usalama barabarani Mkoa wa Mbeya ametoa onyo kwa watu wanaong'oa na kuharibu alama za usalama barabarani na kwenda kuuza kama vyuma chakavu kwani kuondoa alama hizo ni moja ya chanzo cha ajali za barabarani.

Uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoani Mbeya ulifanyika Aprili 12, 2023 ukiwa umebeba ujumbe unaosema, "Mbeya bila ajali, inawezekana, timiza wajibu wako"

Hafla ya maadhimisho hayo imekwenda sambamba na zoezi la ukaguzi wa magari chini ya wakaguzi wa magari wa Jeshi la Polisi, ubandikaji wa stika kwa magari yaliyokaguliwa, utoaji wa elimu na mafunzo kwa madereva wa vyombo vya moto.
 
Back
Top Bottom