Mbeya long time kitambo

Mbeya long time kitambo

nimefatilia kwa ukaribu uzi huu. naona maneno yaliyotawala zaidi ni haya: bob (marley), ganja, ubabe, jombi, kukaba, kubaka, vitisho, utemi, uchawi, doksi, pusha, magendo, kanitandika, kipigo, rushwa, machata etc. duuh. bado tuna kazi kubwa ya kukomboa taifa hili.
Kukurupuka ni ugonjwa mbaya sana
Ulitaka wadanganye historia au?
 
Mimi naikumbuka Mbeya ya 1975/1977. Reli ya Tazara inazinduliwa 1976 tulipanda train iliyotoka Kapiri Mposhi tukashuka Makambako tukarudi Mbeya kwa gari VW combi. Nilikuwa na viwanja vya golf kabla ya kugeuzwa matumizi ili ujengwe uwanja mkubwa wa michezo. Tulishiriki katika Ujenzi wa Uwanja wa Mapinduzi ( Sokoine) tukitokea Majengo primary school tukishirikiana na wanafunzi wa Sisimba, Mbaya, Azimio hiyo ilikuwa 1976 etc. Mwalimu Mkuu Malengo alikuwa Mwl Mwangomile na Mbaya alikuwa Mwakang'ata.
Nakumbuka kulikuwa na kikundi cha Sanaa kilichoitwa Chamnambe kikiongozwa na Mzee Ryoba. Kulikuwa na shule inaitwa Muungano ilikuwa msituni njia ya Mwanjelwa sijui kama bado ipo. Pia nakumbuka Pareto ya uyole. Those old good days.

Pia nakumbuka 1976 ilitokea ajali kubwa ya basi likiitwa Mwambipile Bus Service ilipinduka huko Mwakaleli ikaua watu wengi sana.
Sijafika Mbeya Tangu Dec. 1977, nasikia imebadilika mno.
nimetoka mbeya mwka 70 nasoma st francis naona mimi ndiye mzee kuliko wote humu. nimepita pale kuwaona wale ma sista wa kizungu miaka ya 90 sijui kama wako
 
Yaani niliwahi kuwa na boyfriend wa MTC,kipindi nasoma Mwakaleli high school,lkn masikani ilikuwa Mbeya Block T. Vurugu zake nilikoma,alikuwa akinitembezea kichapo popote hata anikute tu nimekaa na mtu wa jinsia tofauti hata kama ni ndugu yangu. MTC walikuwa washenzi bwana,makondakta na madereva walikuwa wanakiona.

Iyunga boys na MTC walikuwa paka na panya likija suala la Loleza girls. Ila ilikuwa poa sana
Mwakaleli ipi private au Government??
 
Da! Umenikumbusha mbali sana mkuu. Enzi za "jesus" na "Shetani" pale juakali.
Kuna mbabe tenende mlima nyoka na kulikuwa na gari moja ina sura mbaya sana iliandikwa "kisonzo".
Enzi za kutizama sarakasi za kina wanne star na kiingilio cha shillingi 20 baada ya masomo.
Ilikuwa kama kuna mashindano ya mpira, watoto wa isanga ilikuwa tishio sana.
Mbeya....home sweet home.
That was life.
Tenende yupo kazeeka saiz
 
Kuna ma dj wakali wa enzi hizo.
Dj Emma alikuwa mlemavu
Robert Cool, J4, Boomler (Lenny Makaya), Lugax, BBG yaani enzi ni turn table za LP na deck za Kanda
 
Nilimsahau dj Ayeya na wimbo wake wa akandu
 
Jiwegangi kwa miaka hiyo Itiji bila shaka walimu wafutao utakuwa unawakumbuka vizuri Bwalya, Mwakajila, Ndowa, Kyusa, Kalinga, Manase, Mwanakaya n.k.
Yes Mkuu, nawakumbuka sana hasa mwl Ndowa coz ndo alinifundisha std 1 enzi hizo ndo naanza kusoma A, E, I, O hadi U mwaka 1987!!!Nawakumbuka pia walimu wengine km Kilumbi, Mbega, Kaaya, Bwire, Kasiba, Yarabi, Mwasyoke, Mgase, Manase duh kwa uchache!
 
Jiwegangi kwa miaka hiyo Itiji bila shaka walimu wafutao utakuwa unawakumbuka vizuri Bwalya, Mwakajila, Ndowa, Kyusa, Kalinga, Manase, Mwanakaya n.k.
Yes Mkuu, nawakumbuka sana hasa mwl Ndowa coz ndo alinifundisha std 1 enzi hizo ndo naanza kusoma A, E, I, O hadi U mwaka 1987!!!Nawakumbuka pia walimu wengine km Kilumbi, Mbega, Kaaya, Bwire, Kasiba, Yarabi, Mwasyoke, Mgase, Manase duh kwa uchache!
 
Marappa wakali walikuwa Sunday Jackson (Sun Jacko) Musa Mwaiposa (Chancellor Wise/ Dr. Wise) Dika Chakudika (Dika Sharp), Kwaherini King, GILLBIZ, Uswahilini Matola, Cave dwellers, Adili, Isanga family, 2proud etc
 
Mbeya kulikuwa na timu ya Tiger inatoka Tunduma. Pia kulikuwa na rasta chotara wa kizungu Henry Mwambopo tulikuwa tunamuita Henule
 
Unamkumbuka mzee mwasyanguti wa forest?[/Q

Huyu mzee alikuwa anaitwa Mwansyunguti.Mzee alikuwa mbabe acha tu,ngumi mkononi! Nakumbuka alikuwa ana gari yake aina ya Pijoti kwenye bodi kaandika 'Kikusya farm'!Kuna siku mitaa ya Sokomatola alizichapa kavux2 na mzee mwenzie aliyejulikana kwa jina la Seme ambaye alikuwa mtumishi wa zimamoto enzi hizo. Ngumi zilipigwa km nusu saa hivi hadi watu walipofanikiwa kuachanisha ugomvi .
Pia mzee Mwansyunguti alikuwa na mtoto wake kwa jina la Ally. Jamaa alikuwa mtu wa kuvuta bangi plus mkorofi km baba yake!Huyu mshikaji na baba yake walikuwa wasumbufu sana mjini Mbeya!
 
Back
Top Bottom