Mbeya long time kitambo

Mbeya long time kitambo

Nakumbuka enzi hizo Uncle Ngwisa Mapugilo,alikuwa mbabe hasa Mbeya manispaa walikataza kuchunga n'gombe pale makuburi ya Loleza,yeye akapeleka n'gombe,kuchunga akatumiwa polisi hii issue Nilishuhudia live aliwapiga na akaenda kuchukua shoka kufuata mifugo yake siku kadhaa mbele wakamkamata baada ya kupiga bomu la machozi sokomatola hiyo
Issue ya Ngwisa na Polisi ilikuwa hivi, marehemu Mapugilo alikuwa na wake wa Tatu. Mama yake Ngwisa ndio alikuwa Bi mdogo. Ngwisa akamfukuza Stella ambaye ni mtoto wa dada yake ila mama tofauti na Ngwisa. Pia baadae akawatimua na ndugu zake wengine. Wakaenda Polisi. Mamwela wakaja na 110 Lao akawapiga sana, ndipo wakaenda kuleta ma bunduki na mabomu ya machozi. Manjagu walipiga mabomu kuanzia saa tisa Alasiri hadi kesho yake asubuhi, Ngwisa alikuwa akizidiwa na Moshi wa mabomu anatoka na shoka lake anawatimua Polisi ndipo wataanza kumlenga kwa risasi. Kesho yake akaja RPC akambembeleza Ngwisa aende Polisi ndio hicho kisa cha Ngwisa
 
Pia kulikuwa na Bisso Ntepa, alisha fungwa mara kadhaa kwa ujambazi baadae akaokoka na kufungua kanisa lake DSM. Baadae akaachana na kanisa na kujiunga na bongo movie. Miaka minne nyuma nilimuona anaendesha daladala kubwaa
 
Pia kulikuwa na Bisso Ntepa, alisha fungwa mara kadhaa kwa ujambazi baadae akaokoka na kufungua kanisa lake DSM. Baadae akaachana na kanisa na kujiunga na bongo movie. Miaka minne nyuma nilimuona anaendesha daladala kubwaa
Bisso Ntepa ni mlokole tena, ana kanisa lake hapo Dar. Nilikuwa naye hapa mbeya last week.
 
12 inanihusu direct shule ya katikati ya jiji iliyopo mlimani, wale wa Sisimba wapite tufahamiane
 
Mimi naikumbuka Mbeya ya 1975/1977. Reli ya Tazara inazinduliwa 1976 tulipanda train iliyotoka Kapiri Mposhi tukashuka Makambako tukarudi Mbeya kwa gari VW combi. Nilikuwa na viwanja vya golf kabla ya kugeuzwa matumizi ili ujengwe uwanja mkubwa wa michezo. Tulishiriki katika Ujenzi wa Uwanja wa Mapinduzi ( Sokoine) tukitokea Majengo primary school tukishirikiana na wanafunzi wa Sisimba, Mbaya, Azimio hiyo ilikuwa 1976 etc. Mwalimu Mkuu Malengo alikuwa Mwl Mwangomile na Mbaya alikuwa Mwakang'ata.
Nakumbuka kulikuwa na kikundi cha Sanaa kilichoitwa Chamnambe kikiongozwa na Mzee Ryoba. Kulikuwa na shule inaitwa Muungano ilikuwa msituni njia ya Mwanjelwa sijui kama bado ipo. Pia nakumbuka Pareto ya uyole. Those old good days.

Pia nakumbuka 1976 ilitokea ajali kubwa ya basi likiitwa Mwambipile Bus Service ilipinduka huko Mwakaleli ikaua watu wengi sana.
Sijafika Mbeya Tangu Dec. 1977, nasikia imebadilika mno.
Karibu sana Mbeya, Pareto ya Uyole ipo mkuu.
 
12 inanihusu direct shule ya katikati ya jiji iliyopo mlimani, wale wa Sisimba wapite tufahamiane
Nilisoma Sisimba ya Msuya, akahama akaja Mtawa.
Mwalimu Matthew alikuwa anafundisha darasa la kwanza.
Kasela na Mwaisaka ndio walikuwa Mabitozi
 
Aisee. Kuna nyumba ya kina Kajigili pale karibu na Moravian jirani yao. Nakumbuka kuna jamaa yangu alikuwa anaitwa Amini na kina Mwaikakile. Kwenye zile kota kulikuwa kuna mtu anaitwa Mfula Mohamed.
Mkakile, Amini alifariki
 
Kuna jamaa white hivi rafikiye Mkakile alikuwa anaishi Jacaranda baba yake alikuwa anavaa kaptura tu akiitwa "makaptura"
 
Hakika hii ndo mbeya bwanaa enzi hizo alikuwepo mzee mmoja mchawi alitoka malawi aliitwa "CHAKUDONOLA"aliwaliza sana makondakta yaani alikuwa akitoa nauli konda akichanganya tu hela yake na zingine basi anavuta kichawi hela zote akashtukiwa makonda wakawa hawachukui hela zake...
Nakumbuka daladala langu liliitwa 'MTAMBO' ngoma ilikuwa bedford hatari hadi leo dereva babu na gari ni boza la maji..
Sitasahau tuliandamana toka sangu hadi mama john nyumbani kwa mzee MWAMKINGA kupinga asihamishwe..!
Ruanda nzovwe primary kiboko ya sisimba kitaaluma namkumbuka mkuu wangu KAMASHO bila kusahau mboko za mwalimu KURUSHA apumnzike kwa Amani.
 
Bujibuji umenikumbusha mbali sana Mkuu umesahau FAT ya isanga ilikua inatengeneza Tiketi feki za uwanjani na Disco nakumbuka kuna siku walitengeneza tiketi za Disco livingstone ikaonekana watu wengi kuliko mauzo ya tiketi zao ikabidi tutolewe wote disco jamaa yule baunsa akawa akimtambua wa isanga,docks au Nonde hata kama ulilipa tiketi harali haurudi ndani..Kambosonic nilimuona mara ya mwisho Cape Town 2003,Rossebank katulia sana huyo Simply nasikia alikua Jozi sijapata kumuona karibuni..isanga kulikua na Brigedia Mwakayugu na ATU JANDE kwa sasa marehemu..maisha ya kibabe utadhani soweto ya south sasa hivi..
 
Kanji Lalji, Dhandho na Bhanji ndio ma transporters wazito wa kipindi hicho!
 
Wale wa Muungano Primary kulikuwa na mwalimu Mwailima,Mecky,John David,Mamkwe etc bila kumsahau Ester David
Mamkwe amenifundisha muungano ....Mwailima pia amenifundisha hesabu ....amenifundisha hesabu za maumbo .....mzingo ....pia kulikuwa na mwalimu flani kilema Yessaya wa yessaya kanifundisha historia .....huyu mwalimu ilikuwa usipoandika notisi zake za darasani lazima uchezee fimbo .....lakini pia alikuwa akipokea hongo ya shilingi ishirini ili asikuchape .....
 
Mamkwe amenifundisha muungano ....Mwailima pia amenifundisha hesabu ....amenifundisha hesabu za maumbo .....mzingo ....pia kulikuwa na mwalimu flani kilema Yessaya wa yessaya kanifundisha historia .....huyu mwalimu ilikuwa usipoandika notisi zake za darasani lazima uchezee fimbo .....lakini pia alikuwa akipokea hongo ya shilingi ishirini ili asikuchape .....
Mamkwe kanifundisha hesabu na Mwailima kanifundisha Science Kilimo. Mwailima alikuwa anapiga bakora mpaka 20
 
Nimemkumbuka mzee remmy wa kule sokomatola alikuwa mwanamziki na mchezaji mzuri sana wa drafti, wakina Devi, mzee wa kuholamaka, mzee ramadhani. Nimemkumbuka pia dr. Kasimbazi, dr. Salehe n.k.
daah kitambo sanaaa!! dr. Kasimbazi saiz kachakaa,kawa kama mwehu,pombe zimeshamuharibu
 
Back
Top Bottom