Mbeya long time kitambo

Mbeya long time kitambo

Kambosonic na mwenzie muradix ilikua cha mtoto kwa majaa furani walikua olevel pale sangu nimesahau majina yao,wakitoka darasani kwenda toilet wanapanga mstari mmoja huku wakidunda balaa!
 
HII NDIO ILIKUWA MBEYA BWANA

1. Enzi hizo alikuwepo mtu anaitwa Jombi, kudhihirisha ubabe kwa wenzako lazima uwaambie Mimi ni "Jombi"

2. Kulikuwa na basi zinaitwa Kiswele..engine nyuma, Dar - Mby faster, Mafegi hii ilikuwa na vijihoni vya Ukweli,usisahau Mv Saratoga, Tunyande bus service, Zainabus

3. Kulikuwa na wavuta petroli, hawa jamaa walikuwa km 5 hivi, wachafu wanatembea pamoja mitaa ya BP uhindini wakiwa na makopo na vitambaa vilivyoloa petrol wanavuta.

4. kiwanja ngoma, hapa Soka lilipigwa bwana, timu yangu ya Mtaa Snow White chini ya Key, kina Baba Jeni. Basket ball ilikuwa pale Centre, tulikuwa na chama letu Mbeya Flames.

5. Town pale palikuwa na vichaa hatari kuna "Tiotio" huyu alikuwa anachapa ngeli balaa, Merry Kichaa alikuwa na alergy na watu weupe, akikuotea atakukimbizaa na stick utakula. Pale Mbeya Recto ndio ilikuwa km Makao makuu ya vichaa walikuwa kibao

5.Pale Bomani palikuwa na Mzee mmoja mfupi nakumbuka jina moja la Mwakifuna,nilifanya jitihada ili kumuona tu maana kutokumjua na kumuona ilikuwa ni weakness kubwa.

6. Kipindi hicho Disco lilikuwa Mount Livingstone na Rift valley, Soggy doggy enzi hizo akiitwa Wasape na Sugu- 2 Proud, hipop ilinoga bwana.

7. Mtakumbuka Mbeya tulikuwa na ukumbi Wa Sinema pale opposite na Ofisi za Posta Town, Muvy ya Hatya ilifunika sana enzi zile.

8. Miaka ile bwana mvua ilikuwa inapiga km gharika,sometimes ilikuwa inamwagwa barafu km ulaya,mlima Loleza ulikuwa ukifunikwa theluji kwa siku kadhaa. Radi sasa, hatariii mpaka nyumba ina Shake.

9. Siku ya Jumamosi ilikuwa ya kuosha mbwa,mbwa wote walikuwa wanapelekwa josho pale Mifugo,nyuma ya Kanisa la Roman,mkishamaliza kuogesha mnaanza kugombanisha Mbwa,mbwa Wa kizungu walikuwa wanaogopwa kupambanishwa na Wa kienyeji ikiaminika wananguvu balaa.

10. Uzunguni enzi hizo kulikuwa na matunda ya aina mbalimbali,watoto walikuwa wanatoka maeneo kadhaa ikiwemo Isanga kuja kuchuma maparachichi,mang'ang'a,mafyulizi,mapohora,mapera nk.

11. Mwanjelwa.enzi hizo iliitwa Doksi au Njelii, mitumba viwango,raba Kali,msela ukitupia vya doksi umemaliza.

12.Enzi zile ukisoma Sisimba na Azimio unafunika,Shule ya International ilikuwa Umoja primary school, waliosoma hapo hata kupishana nao unaogopa

13. Kuruka ukuta Wa Uwanja Wa Sokoine au kuingia uwanjani kupitia Bomba la maji ya mvua wakati Wa mechi ilikuwa ujanja balaa.

14. Ukisikia Shule za Sekondari Iyunga, Sangu, Loleza, Mbeya Day zilikuwa na kila aina ya sifa.Sangu kulikuwa na vichwa lazima uvitambue wababe km Simply na Kambosonic waliogopwa.

15. UMISETA sasa, dah, achaa..hapa Lutengano hapa Mwakaleli, boli lilitandazwa,kikinuka uwanjani ilikuwa km vita,makwanja na fimbo hujui vilipotokea,ukizubaa utakula mkono balaa

16. Kuna mdada walikuwa hatari alikuwa anatembeza kichapo kwa wanaume balaa walikuwa anatokea ilemi alifahamika kwa jina la Jeni.

17 Kuna jamaa alikuwa mtata sana mtaa Wa mafiati, makunguru, juakali alifahamika kwa jina la Daudi Masoke. Walikuwa balaa alikuwa anaiba Nyumba nzima hadi kitanda ulicholalia.

18. Ukisia mtaani Dunda, Kwendi, Shaban wanatembea mtaani wanaume wote kimya walikuwa hawaoni shida kukupiga dispiss ya tumbo. Wakitaka kupora walikuwa hawapati shida wanakuzunguka baada ya muda unaporwa ukipiga kelele hakuna Wa kukusaidia maana hadi wazazi wao walikuwa wanawaogopa.

19. Ukisikia obamka yaani ilikuwa full kwa watoto Wa mafiati, sinde, ilemi, isanga, ilolo ni sehemu ya kuchomea viazi mtoto walikuwa radhi asile nyumbani aende njelii kuokota viazi ili akachome obamka.

20. Uswahili tabu fresh food iligeuzwa jina na kuitwa Chakula barafu kiss vyakula vinahifadhiwa kwenye friiza. Expire date ya chakula hasa maziwa ilikuwa furaha kwa watoto Wa uswahili. Zaidi panaitwa city pub/century plaza.

21. Doxi waliwauzia wanyia blauzi na kuwaambia mashati. Ndio kisasi kikarudishwa unyiani na kuwaambia wamachinga Wa nguo Tumugoge tumuleshe...(tumuue tumuache).

NAIKUMBUKA MBEYA YA ZAMANI..
Mbona Wane hujamtaja mkuu? au wewe ulikua humkimbilii na mangongoti yake? Dah kitambo enzi hzo Sugu anavalia suruali matako nje
 
Kulikuwa na pusher wa bangi huko Nonde. Ukitaka kuvuta bangi kwake utavuta bure hata gunia. Take away ndio unalipia. Jamaa alikuwa anaitwa Mswanga na alikuwa na stock ya kutosha kuvutisha vijana wote wa Mbeya kwa miaka minne bila kutetereka
"mswanga " alikuwa ni wa kimataifa!
 
Kuna dogo alikuwa anacheza sana sarakasi alikuwa anaitwa PINDU alikuwa mara kwa mara anazunguka mji akionyesha michezo
 
Kuna jamaa alikuwa anaitwa Bob G alikuwa mzee wa magendo kutoka nchi mbalimbali hasa malawi. Alikuwa na cruiser wakati kipindi hicho polisi wana hyundai. Aisee Hatari mno. Nasikia jamaa alikuwa anafukuzwa na polisi akamwagaga rambo ya shilingi mia mia pale uyole watu wakaingia barabarani polisi wakashindwa kupita.
Kuna jamaa walikua wanaiba ng'ombe hata 30 na wanawaswaga barabani wakiwa na gobole na polisi wanagwaya. I miss that Mbeya
ni kweli aiseh huyo Bob G mtoto wake mmoja ni rafiki yangu.....Jamaa alikuwa hatari sana kwa magendo huyo.
 
kuna jamaa alikuwa anaitwa JAPIPO alikuwa giant fulani hivi, na mchezaji wa timu ya Stand Uyole pale,,,,,Jamaa alisifika kwa kuwa na mashuti sana uwanjani. Alikuwa beki matata sana
 
Kweli umekaa mby .....watoto wa malakasuka na bebby shangazi walisumbua sana .....pia kulikuwa na mtemi mmoja anatokea Isanga akiitwa brigadia mwakayugu .....by the way uwanja ngoma nimecheza soka nikichezea timu ya forest .....mambo yalikuwa mswano kipindi hicho
Forest.Jitambulishe.Wewe ni nani?
 
Forest.Jitambulishe.Wewe ni nani?
Nilichomoka longtime kitambo miaka kumi na tano sijarudi huko .....by the way utambulisho ndio hilo rass jeff kapita....hiyo timu ya forest nimecheza na akina robyo mwasalemba,hamis chepe chepelino.....maja,zungu,abuu kasanga
etc,etc ...niambie ww unatokea angle ipi ......ama ww ni mtoto wa mzee nani nitakuelewa
 
Back
Top Bottom