Mbeya kwarindima kwa Mabomu, risasi!

Mbeya kwarindima kwa Mabomu, risasi!

Haki ya kufanya biashara maeneo ambayo hayajatengwa kwa ajili hiyo?

Mkubwa, tatizo la Wamachinga wa Mbeya linatokana na kuunguliwa na masoko mfululizo, hawana pahala pa kuweka bidhaa zao baada ya masoko kama 7 hivi kuungua tangu mwaka 2006, na mpaka sasa hakuna soko hata moja ambalo limejengwa na kutumika, tangu yameungua (Mbalizi, Mwanjelwa, Uhindini, Sido n.k). Kandoro na watawala wenzake waliahidi kutafuta na kutenga mahali pa kufanyia baiashara kwa ajili ya Watanzania hawa, lakini mpaka jana ambayo ndo ilikuwa deadline hawajatekeleza chochote. Hayo ndo madhara ya kuingiza longolongo za kisiasa katika masuala ya kiutendaji. Ni makosa makubwa. Ikumbukwe kwamba Mbeya mjini wapinzani wana nguvu, si kama miaka ya nyuma. Hakuna haki inayopatikana bila kuifanyia kazi, ndo sababu unaona leo Watanzania wenzetu wanapodai haki yao wanapigwa mabomu. Yana mwisho haya.
 
hawa CCM wameshindwa kufikiri hata kwa tumbo sasa wanatumia masaburi.Nadhani huu ndio mwisho wa mwisho wa CCCCCCCM
 
Tnawashukuru sana Beghazi ya Tanzania aka KILIMANJARO......
Mwanzoni tuliona kama wangeshindwa lakini Uthubutu wao na elimu waliyoitoa kwa watanzania ni kubwa
Na sasa DEMOCRASIA IMEEJULIKANA MAANA YAKE KUANZIA KILIMANJARO, ARUSHA, MWANZA, SHINYANGA, MARA(RIP CHACHA WANGWE), MBEYA, RUKWA...........................NA BADO TUNASONGA MBELE!!!!!!!!!!!! HADI TUFIKE SIRTE YA BAG'MOYO
 
hivi jk anaona taabu gani kuacha uraisi ampishe mtu mwingine ..hivi kwanza nasikia hazina hakuna hela wanafanyia nini hela hawa au wanaweka vocha kwenye simu na kunywa azama kola
 
Jamani nasikia kuna vurugu kubwa mjini mbeya...eneo la mwanjelwa kati ya wafanyabiashara ndogondogo na Polisi....Wakuu mwenye taarifa zaidi atujuze sisi tulio mbali.
 
Wenzangu wa Dox(Mwanjelwa) poleni sana.

Tatizo la ukosefu wa ajira Mbeya ni kubwa sana, kiasi kwamba vijana wengi wameamua kujiajiri kwa biashara ndogo ndogo. Miaka ya karibuni, masoko mengi sana mbeya yameungua na kuna soko moja la makunguru lilibadilishwa kuwa shule ya english medium eneo ambalo halifai kuwa shule kabisa, hali iiliyopelekea watu kukosa sehemu rasmi za kufanyia biashara. Serikali makini ilikuwa na wajibu wa kutenga maeneo ya muda kama suluhisho la muda mfupi huku ikiendelea na ujenzi ya masoko yaliyoungua. Mfano soko la mwanjelwa peke yake lilikuwa linaajiri vijana zaidi ya 10,000 ambao wana familia zao zinazo wategemea.

Vijana wa mbeya si watu wanaopenda vurugu na serikali. Ni watu waoga sana ukilinganisha na mikoa kama Mara, Arusha na Kilimanjaro. Ukiona wamefikia hatua hiyo ujue serikali imegusa maslahi yao sana kiasi kwamba inatishia uhaio wao.

USHAURI

Busara zitumike. Kandoro aache ubabe aliotoka nao Dar na Mwanza. Abadilike kidogo,hali ya mbeya ni tofauti sana. Ahakikishe halmashauri inatenga maeneo mapya kwa ajili ya biashara ndogo ndogo huku watu wakisubiri kujengwa kwa masoko mapya. Serikali isitumie mkono wa chuma kwa mambo hata madogo sana huku ikilaumu upinzani kwa kila maandamano. Watu wanaacha kazi kwenda barabarani wana sababu zao za msingi.
 
Hadi ivi sasa ninapo ingia mtamboni mabomu yanaendelea kurindima baina ya wamachinga na polisi wa jiji la Mbeya, ni katika eneo la Mwanjelwa.lakini tatizo nini serikali inashindwa kuwatambua na kuwaheshimu wamACHINGA.
 
Maandamano yameisha watu wanachechemea kurudi makwao chapwa mbaya polisi wanapiga jaramba wanaomba wapi kwingine waende vijana wanpendeza hawa wanapendeza sana hawa wameiva ...Tanzania hakika tuko imara
 
watu wanapigwa risasi za moto watu wamekufa magari yamechomwa polisi wameiishiwa risasi wameenda kuwachukua wanajeshi kitu ka somalia hivi i wish kinuke nchi nzima
 
mkuu kuna thread ya mbeya.
Mods please move hii thred kule inajaza server bule
 
intelijensia haikufanya kazi huko Mbeya nini?? Tatizo wanafikiri haya matatizo yanaletwa na CDM na ndiyo maana wanaconcrate nao bila kujua kuwa matatizo yako kwa Wananchi wa chini!!
 
Police kumbuka cc ni ndugu! Mnamuogopa jk lakini ngojeni hacra yangu ifike 100% kweli patakuwa tunisia! Mi mwenyewe nmehitim udsm hamna ajira alafu mabomu! Kulaaleki!
 
Maandamano yameisha watu wanachechemea kurudi makwao chapwa mbaya polisi wanapiga jaramba wanaomba wapi kwingine waende vijana wanpendeza hawa wanapendeza sana hawa wameiva ...Tanzania hakika tuko imara
hata kama unalipwa kwa kuwa Jf,toa vtu vya maana,ACHA UJINGA,hii issue haihusian na Chadema wala ccm,MTU MZIMA OVYOO!
 
Back
Top Bottom