Mbeya kwarindima kwa Mabomu, risasi!

Mhoja

JF-Expert Member
Aug 13, 2010
207
24
Wadau risasi na mabomu yanarindima mwanjelwa mbeya kati ya polisi na vijana. Barabara ya kibiashara ilifungwa. Ni hatari
 
Sababu kubwa ni kwamba machinga wamegoma kuhama maeneo ya mwanjerwa kama walivyoagizwa na mkurugenzi,mana hakuna sehemu waliyoandaliwa,wapo wanaimba peoples power na kuonyesha vidole viwili juu,wanarusha mawe,hari ni hatari kwa kweli wanasema uonevu basi unaofanywa na serikali ya CCM.
 
poleni sana wana mbeya ndo tujue serikali yetu ilivyolegelege maana haya yote yalihitaji maandalizi mapema na yakajengewa mazingira mazuri haya yasingetokea tuombe Mungu asife mtu hapo.
 
Tatizo lao hawa CCM hawataki kuwasikiliza na kufata ushauri wa Chadema,haya majimbo ya chadema watu wameelekezwa sana haki zao na siku soko la Sido lilipoungua hapa Mbeya, mda si mrefu Mh sugu na Mbowe walifika na kuongea na wananchi na kuwapa pole na kuwaelekeza haki zao.

Sasa cha kushangaza mpaka muda hu mabomu yanaendelea na machinga na vijana wengine wameungana kupambana polisi wanaimba peoples power hali ni hatari ndugu zangu mi nipo huku maeneo ya oil com, na nawa maji usoni, na tangia jana hawa vijana walikuwa na hamu na mandamano ya Chadema!
 
Huku ni noma maomu ya machozi yanarindima kwa kasi.Vijana wameziba barabara kwa mawe mitaa ya isanga,ilemi na vitongoji vinavyozunguka Mwanjelwa.Lakini hivi mabomu na risasi vinaleta maisha bora au serikali imeshindwa kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya vijana? JK na magamba wenzako Mbeya inaweza kuwa Homs maana Bengazi ni A town.Makinika.
 
acha wadai haki zao maana wanyonge hawa wananyanyasika tanzania nzima utazani walipenda kufanya shughuli hiyo ngumu.Maisha tu ndo yanawafanya wafanye hivyo ila serekali badala ya kuwapa support inawaharibia.sijui lini kipato cha mnyonge kitakuwa.
 
dar fujo kila mahali siku hizi, huko tunakoelekea huko si kwema

Nahisi ndo wanachokitaka ccm wanapofika wakati badala yakupunguza matatizo ya mnyonge ndo wanazidi kuyaongeza, je ujambazi ukishamiri watamlaumu nani?
 
Back
Top Bottom