Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,568
Jeshi la Polisi Mkoani Pwani limekamata noti za fedha zenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 13 za bandia pamoja na Mtambo wa kutengeneza pesa hizo Maeneo ya Goba jijini Dar es salaam ambapo baadhi ya noti hizo zilishaanza kutumika mitaani ikiwemo Msata, Chalinze Mkoani Pwani
Tukio hilo limekwenda sambamba na kuwakamata watu wanne wanaotuhumiwa kuhusika na mnyororo wa matumizi na uzalishaji wa noti hizo bandia.
Baadhi ya wakazi mjini Kibaha wamesema hawajui noti bandia ni ipi na halali ni ipi kutokana na kutojua utofauti wake kirahisi machoni.