Mbeya Golden city hotel - ogopa kabisa hii hoteli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbeya Golden city hotel - ogopa kabisa hii hoteli

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by sparrow, Apr 20, 2012.

 1. s

  sparrow Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napenda kutoa tahadhari kwa mtu yoyote anayetaka kulala katika hii hotel iliyopo mbeya aogope sana kwani inashirikiana na wezi. Unaibiwa katika mazingira ya kutatanisha kwani hawana air condition na wana madirisha ya aluminium; ukiacha dirisha wazi tu ili upate hewa tu umekwisha unaibiwa bila kujijua...sasa nadhani wafanyakazi wanaita mwizi aje au wao wenyewe wanakuibia. Na uongozi ndio kabisa hauna ushirikiano nafikili na wao wanashirikiana na hao wezi. USIJARIBU KABISA KULALA KATIKA HII HOTELI MIMI YAMENIKUTA NA WAHUSIKA WA HOTELI HAWANA KABISA MSAADA
   
 2. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ungetupa kisa chako kuthibitisha maneno yako
  Vinginevyo itabaki kuwa kama jelous tu
  OTIS
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Ajira million moja hizo.
   
 4. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Adam Malima ndio atakuwa anakuja kulala hapo... ha ha haaaaaaaaa
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Isije ikawa wewe ni mpinzan wao?
  Baridi lote la mbeya wewe wataka kufungua dirisha?
   
 6. s

  sparrow Member

  #6
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilikua nimelala usiku na kuacha dirisha wazi kidogo..tena ni ghorofa ya kwanza na ina fence na mlinzi yupo; basi kama saa 10 asbh hivi nikashtuka baridi kali na dirisha limefunguliwa zaidi halafu suruali ambayo ilikua na pochi nili-hang ndani zilikua zimetupwa kwa nje ya dirisha..tukaita receptionist na mlinzi wakawa wanasema wezi wameiba tena..inaelekea wanajua kuna uwizi sana na cha kushangaza walichukua hela tu lkn kadi za bank...kifupi hao wezi au wafanyakazi walivuta suruali kwa kutumia mti..

  baadae wanasema eti ingebidi niache hela reception halafu ndio nikalale chumbani kwani wanajua vyumbani hakuna usalama kabisa. Na wakawa hawataki nilipoti polisi eti wana utaratibu wao wa kushughulikia wezi kwani wanawajua kumbe wajanja tu wanajua umetoka Dar na hutakaa siku nyingi..

  OGOPA SANA HII HOTEL INAJIFANYA INA HUDUMA NZURI KUMBE WEZI SANA.
   
 7. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 2,042
  Likes Received: 383
  Trophy Points: 180
  Pole sana. Mimi nilikuwa na kawaida ya kufikia hapo. Kuna siku nikaenda hapo kama saa 12 hivi nikitokea Dar Kwa Sumry nikaambiwa mmiliki wake alipata ajali na kufariki siku hiyo saa 9.00 Mchana. Hivyo nikaenda kukaa ktk hotel inaitwa Paradise bahati mbaya nilikuwa nimepoteza kadi ya Benki hivyo nilikuwa na fedha taslimu kwa ajili ya Semina. Nilikuwa natoka nazo siku zote (mbili)zikiwa kwenye mfuko wa laptop hadi nikalipa na kubakiwa na Tsh 1,500,000/= basi kukawa na onyesho la Makhirikiri karibu na hapo nikaenda na kufanya kosa la kuacha zile fedha kwenye Begi (wanaziita Pilot Bag)

  Nilivyorudi kitu cha kwanza nikaangalia nikakuta pesa iko nikalala na hiyo begi haijafunguliwa iko kama nilivyoiacha. Kuamka asubuhi nikalipe nikakuta kila fungu la laki moja inapungua elfu 30,000/=. Nikafanya uhakiki nikakuta kumbe nililizwa pia soksi mpya kama pea mbili, na underwear mpya kama mbili hivi. Hapo ndipo nilipowaaminia.

  Nikashuka chini kuripoti nikakutana na bango kuwa vitu vyote vya thamani ikiwa ni pamoja na PESA vikabidhiwe mapokezi!! Upotevu wowote Hoteli haitasikiliza hata kidogo.
  Hivyo nikaghairi kuripoti hilo tukio.

  Hata hivyo ni hatari sana kukabidhi fedha kiasi kikubwa kwani kuna jamaa yangu alifanya hivyo siku anaondoka akakutana na vijana wenye piki piki pale tu nje ( Siyo Paradise) wakimtaka awakabidhi haraka kiasi hicho bila kuchelewa kwani walikuwa wanawahi kumwua jamaa mwingine hapo mbele

  Hivyo wizi upo sehemu nyingi cha kufanya ni kuchukua tahadhari ya hali ya juu, ikiwa ni pamoja na kutokabidhi pesa kaunta.
   
 8. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Watu wengine wakilala huzalisha gesi zinazotakiwa kutoka nje
   
 9. s

  sparrow Member

  #9
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi sio mfanyabiashara..hivyo sina nia ya kuwachafulia. Nimeweka hapa ili wana jf muwe makini na hii hotel kwani najua humu ndani kuna watu wanasafiri kwa shughuli mbalimbali hivyo uwe makini.

  Ni hatari sana kufunga madirisha kabisa hata kama nje kuna baridi; baridi haina uhusiano na hewa ndugu yangu. Unahitaji hewa ndio maana unaacha kidogo tu upate hewa.

  Hiyo hotel vyumba vyake havina air condition wala any other air supply system hivyo itabidi ufungue tu dirisha hata wakati wa baridi; sasa hapo ndio wanapoita wezi waje kuiba. Yaani mwizi apande mpaka ghorofa ya kwanza bila mlinzi au wafanyakazi kujua na atajiaminisha vipi wakati wa kushuka?..yaani ni inside-job kabisa

  HIVYO NAWAONYA VISITORS WA MBEYA YASIJE YAKAWAKUTA KAMA YALIYONIKUTA MIMI
   
 10. s

  sparrow Member

  #10
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Sina jealous nao kabisa ila nimeweka hapa wana jf tuwe makini na hizi hotel ambazo zina kazi mbilimbili; hasa kuwaibia wateja wao.
   
 11. Mhoja

  Mhoja JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2012
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mi nadhani ni jambo la bahati mbaya tu, mi nimekuwa nikilala hapo haijawahi kutokea, wahudumu wake ni wakarimu na ina full ulinzi. Kwa mazingira ya hotel zote za kisasa hawaweki grill za nondo na vyuma hata ukienda kilimanjaro hotel. Uwe na amani, usitembee na fedha nyingi.
   
 12. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,159
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Pole mkuu, haukuwa na SMG? Inaweza ikawa ulikuwa una Malima CD akaku time, tueleweshane kaka
   
 13. s

  sparrow Member

  #13
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mimi nilidhani hivyo lakini wewe lala hapo floor ya kwanza uone; im sure wanajua suala la uwizi kwani mlinzi alisema imekua ikitokea..tatizo wanajua kuna uwizi lkn hawasemi au kutahadharisha..
   
 14. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Poleni kwa mlokutwa na hayo maswaiba!
  Fine next time usilale apo as Mbeya kuna hotel nyingi tuu za kulala tena standard kuliko iyo walikuliza.
  Alafu pia nawashukuru kwa kushare izi info maana tungeweza kuwa next Victims na maisha yalivyo magumu unaweza faint
   
 15. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Shukuru Mungu walikuibia pesa na wakakuachia hizo kadi zako ; huko Mbeya si ndiko wanakochuna watu ngozi kwa imani za kishirikina!!! You could have been a victim; hawa wanyambala ni watu wa vituko!!
   
 16. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  poleni sana na mikasa hiyo mikubwa mliyoipata. pia tunashukuru sana kwa taarifa ambazo ni vizuri tu kuzipokea na kuzifanyia kazi manake ni heri kinga kuliko tiba.
   
 17. s

  sparrow Member

  #17
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mimi nashukuru sana kwa hilo ila nimetahadharisha kwa sababu next victim katika hiyo hotel anaweza akawa mwana jf nimeona nilete taarifa kwani inawezekana hoteli inahusika katika uwizi huu. Nitaweka picha ya hotel muione.
   
 18. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #18
  Apr 20, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Napafahamu vizuri sana hapo ila nashangaa ni kahoteli kazuri lakini wanashindwa kukaendesha au kwasababu mwenye nayo alishafikisha miaka10 akatangulia mbele za haki??
   
 19. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #19
  Apr 20, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,909
  Likes Received: 2,336
  Trophy Points: 280
  Asante kwa taarifa mkuu.
  Hii Hotel iko sehemu gani tuiepuke?
  Tena kesho naelekea Mbeya
   
 20. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #20
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Da hivi wana JF mtu huwezi kwenda kulala kituo cha polisi maana hawa ndio walinzi wa raia na mali zao,i believe ukulala hapo utakuwa safe side
   
Loading...