Mbeya Golden city hotel - ogopa kabisa hii hoteli

Napenda kutoa tahadhari kwa mtu yoyote anayetaka kulala katika hii hotel iliyopo mbeya aogope sana kwani inashirikiana na wezi. Unaibiwa katika mazingira ya kutatanisha kwani hawana air condition na wana madirisha ya aluminium; ukiacha dirisha wazi tu ili upate hewa tu umekwisha unaibiwa bila kujijua...sasa nadhani wafanyakazi wanaita mwizi aje au wao wenyewe wanakuibia. Na uongozi ndio kabisa hauna ushirikiano nafikili na wao wanashirikiana na hao wezi. USIJARIBU KABISA KULALA KATIKA HII HOTELI MIMI YAMENIKUTA NA WAHUSIKA WA HOTELI HAWANA KABISA MSAADA

Mosi wewe ni mwongo, Kwa hali ya hewa ya MBY huitaji kiyoyozi, pia jengo la hoteli tajwa nl la Gorofa. Acha kuhara]ibo Biashara za watu umetumwa wewe.
 
Pole kaka kwa yaliyokusibu na shukrani kwa tahadhali uliyotoa na kwa nyongeza tu,wanajf msiziamini sana hata zile funguo zao za guest yaani guest yoyote ile kwani nikama huwa wankuwa na copy so ukifunga na kutoka wao wanafungua nakukupekua chochote cha thamani halali yao.
 
Mosi wewe ni mwongo, Kwa hali ya hewa ya MBY huitaji kiyoyozi, pia jengo la hoteli tajwa nl la Gorofa. Acha kuhara]ibo Biashara za watu umetumwa wewe.

Ww vipi issue sio kutaka a/c bali utafunga madirisha wkt hakuna any air supply..ukiwa ktk gari sehemu yenye barodi unazima ac na kufunga madirisha yote?..fahamu kwamba a/c ina condition hewa iwe baridi au hata joto na pia ina supply hewa kutokq nje

Hata mm nilishangaa kuibiwa kupitia dirishani wkt nililala ghorofa ya kwanza ndio maana nadhani wafanyakazi wanahusika
 
Ahsante kwa taarifa hii. Wakati fulani nilisafiri kwenda huko kwa mara ya kwanza, nilipoiona nilitamani nikae humo maana nilikuwa nakaa huko kwa wiki mbili. Kwenye seat nilikuwa na mabinti wawili ambao nilikuwa nimeshawajua si watanzania, ni wamalawi. Kwa vile tulikuwa tayari tuezoeana, nikawaeleza juu ya huo mpango wangu. Wakanisimulia walivyowahi kuibiwa humo Hotelini na hawakupata msaada wowote kutoka kwenye uongzi wa hoteli hiyo.
Baadae wakiwa wanajiandaa kuondoka, waliwakuta vijana waliowaibia maana waliwaona, wakiwa na mtu waliyejulishwa ndiye meneja wa hiyo hoteli wanaongea kwa vicheko.
Hivyo niliahirisha na kukaa Peter Safari Hotel, ni sehemu salama na ni wakarimu. Nimekuwa nikikaa hapo kila mara ninapoelekea huko.
 
Mimi sio mfanyabiashara..hivyo sina nia ya kuwachafulia. Nimeweka hapa ili wana jf muwe makini na hii hotel kwani najua humu ndani kuna watu wanasafiri kwa shughuli mbalimbali hivyo uwe makini.

Ni hatari sana kufunga madirisha kabisa hata kama nje kuna baridi; baridi haina uhusiano na hewa ndugu yangu. Unahitaji hewa ndio maana unaacha kidogo tu upate hewa.

Hiyo hotel vyumba vyake havina air condition wala any other air supply system hivyo itabidi ufungue tu dirisha hata wakati wa baridi; sasa hapo ndio wanapoita wezi waje kuiba. Yaani mwizi apande mpaka ghorofa ya kwanza bila mlinzi au wafanyakazi kujua na atajiaminisha vipi wakati wa kushuka?..yaani ni inside-job kabisa

HIVYO NAWAONYA VISITORS WA MBEYA YASIJE YAKAWAKUTA KAMA YALIYONIKUTA MIMI
Asante kwa kutujuza. Sasa nimemwamini jamaa yangu aliyenisimulia hadithi ya kuibiwa pesa nyingi tu huko huko Mbeya kwenye hoteli yenye jina kama hilo. Yeye aliripoti polisi lakini yaellekea hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kwani hakupewa feedback baada ya kuambiwa aache contacts zake na wangemjulisha matokeo ya upelelezi. Ilikula kwake maana sasa ni miezi kadhaa na tayari yuko nje ya nchi atatakokaa kwa miaka 2 hivi. Kama hakuna Hoteli nyingin yenye jina hilo hapo basi ni kweli hoteli hiyo imesheheni vibaka na haifai kabisa kufikia.
 
Kweli kabisa golden view moshi waliwahi kuniliza, nikitendo cha dk 3 tu.......


Pole kaka kwa yaliyokusibu na shukrani kwa tahadhali uliyotoa na kwa nyongeza tu,wanajf msiziamini sana hata zile funguo zao za guest yaani guest yoyote ile kwani nikama huwa wankuwa na copy so ukifunga na kutoka wao wanafungua nakukupekua chochote cha thamani halali yao.
 
Mosi wewe ni mwongo, Kwa hali ya hewa ya MBY huitaji kiyoyozi, pia jengo la hoteli tajwa nl la Gorofa. Acha kuhara]ibo Biashara za watu umetumwa wewe.
Bila shaka wewe ni mmoja wa wezi hao. Laiti nchi hii ingekuwa na vyombo bora vya upelelezi tungekutia mbaroni. Unatetea nini wakati hata humu kwenye JF tu wapo watu wengi wanaotoa ushuhuda wa uhalifu wa hawa jamaa?
Natamani serikali ingekuwa makini katika kutoa vibali vya kuendesha hoteli na nyumba za kufikia wageni kwa kuzingatia usalama wa afya na mali za wateja. Hata hili tu limewashinda?
 
poleni sana ninawashauri tu sio kwa Jiji la Mbeya tu sehemu yoyote wizi upo hivi sasa kuna makampuni ya simu yana huduma ya kuhifadhi fedha ni vizuri kutuweka katika makampuni hayo kwa tahadhari zaidi
 
Ni kweli kila sehemu unaweza kuibiwa, ndio sababu ya hii maada. Ni hatari sana sehemu iliyoaminiwa na kupewa dhamana ya kutoa huduma ya maradhi kwa watu ikageuka kuwa kijiwe cha wahuni wa kuwaibia wateja wao. Baada ya wizi, hata mauaji pia yanaweza kutokea.
Hii tabia ya kwamba kama una vitu vya thamani uvikabidhi mapokezi nayo ni hatari sana. Unapowakabidhi hela nyingi au vitu vya thamani sana, unawatamanisha hawa watu na hivyo ni rahisi kukufanyia chochote kibaya ili wabaki na vitu hivi. Ilitokea hotel moja, kijana mmoja alikabidhi Milioni tano mapokezi, usiku akiwa amelala, alishangaa kumkuta Meneja wa hotel na mlinzi wa hotel hiyo, wako ndani wameongozana na Vijana watatu, ambao walimteka kijana huyo na kutokomea naye.
Lengo la mpango wa utekaji huo lilikuwa kumuua kijana huyu na kumtupa mtoni. Alijiokoa kwa bahati sana, baada ya aliyekuwa anamlinda huku wakisubiri mpango wao ukamilike, kusinzia.
 
Asante kwa kutujuza. Sasa nimemwamini jamaa yangu aliyenisimulia hadithi ya kuibiwa pesa nyingi tu huko huko Mbeya kwenye hoteli yenye jina kama hilo. Yeye aliripoti polisi lakini yaellekea hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kwani hakupewa feedback baada ya kuambiwa aache contacts zake na wangemjulisha matokeo ya upelelezi. Ilikula kwake maana sasa ni miezi kadhaa na tayari yuko nje ya nchi atatakokaa kwa miaka 2 hivi. Kama hakuna Hoteli nyingin yenye jina hilo hapo basi ni kweli hoteli hiyo imesheheni vibaka na haifai kabisa kufikia.

Yaani itakua ni hotel hii hii ya mbeya golden city kwani hata mm ilitokea hivyo hivyo..na km kweli mwizi anatoka nje ya hotel its very simple kumkamata siku zote hotel kwa nn haijakamata..u leave the window open at nite, mlinzi anajifanya amelala na officers wanakaa ndani ya chumba wakisubiri..in several tries lazima atakuja kuiba then unamkamata..ila kwa sababu ni staff ndio wezi basi hawataki kumkatama mwizi

Halafu kwangu mm hata police walikua wanataka tusi-report eti wana utaratibu wao..shame on managemen n staff of this mbeya golden city hotel
 
Hii tabia ya kwamba kama una vitu vya thamani uvikabidhi mapokezi nayo ni hatari sana. Unapowakabidhi hela nyingi au vitu vya thamani sana, unawatamanisha hawa watu na ni rahisi kukufanyia chochote kibaya ili wabaki na vitu hivi.
.

Yaani hata mm nashangaa kwanini uweke reception na ww umelala chumbani kwahiyo ulinzi wa reception na chumbani ni tofauti ktk hotel...tatizo ni wezi ni wao wenyewe au wanawajua hasa hao wanaojifanya mameneja ndio wezi hasa
 
Ukiona vipi usiku ufungue mlango uwe wazi kabisa, vuta ka meza wekea mlango ili usijifunge, kama kuna net shusha kama hakuna basi panda kitandani lala. Hakikisha taa inawaka ili wapitao kwenye korido waone kituko ulichofanya cha kuacha mlango wazi.hakika hatoingia mtu kwako

mhh! Sio kwa wabongo, unakuwa umewarahisishia kazi.
 
Mimi niliwahi kulala hapo nikashangaa hotel nzuri lakini haina watu kabisa, yaani kama gofu tu. Basi usiku mlinzi akapita dirishani akagonga na kusema funga dirisha nikamshangaa kwani kulikua na joto. ASBH NIKAHAMA KABISA
 
Huo ni uzushi wa hali ya juu,mimi binafsi nilikuwa mby mwezi uliopita na nilifikia hapo mbeya golden city hotel ni hotel nzuri na ya kisasa kabisa na huduma zake ni nzuri sana,ishu ya wewe kuibiwa si sababu ya kuiponda hotel,hata kilimanjaro hotel watu wanaibiwa sembuse mby golden city?,muhimu ni wewe mwenyewe kuwa makini na mali (fedha) ulizonazo,kumbuka adam malima alilala kwenye hotel ya kifahari kabisa pale morogoro akiwa na siraha za moto kama smg lkn bado wezi walimwibia sembuse wewe ambaye hata panga hukuwa nalo?, nadhani kutokana na ushindani mkubwa wa hotel uliopo mby yawezekana ukawa unatumiwa uli kuharibu brand ya hotel hiyo. Mimi nawashauri kwa wanaokwenda mby wasiogope kwenda mby golden city hotel ni mahali pazuri na salama
 
Mzee wa busara

Inawezekana ww ndio una hisa katika hii hotel au ndo meneja..kuna watu watatu tofauti ktk hii thread ambao wameonyesha kujua vitendo vya uwizi vitavyotokea sasa unatetea nini. Na nimejibu several times sina hotel wala biashara mimi ni mfanyakazi tu. Ninaweza kuweka hapa namba ya kesi ambayo nilifungua na ukaangalie inahusu nini..usiwe na fikra finyu kiasi hicho wkt jina lako linataka uwe makini. Mimi sijakaza mtu kwenda hapo lkn ajue kuna uwizi.

Kuna makini na pesa we all agree lkn wewe unaibiwa wkt umelala chumbani kwako na unasema hotel ina ulinzi whats that..
 
Tunashukuru kwa taarifa achana na hao wenye hisa au ndio wezi wenyewe. Natumaini kungekua na post kama hii zamani na kuisoma usingelala hapo na kuibiwa

jf tunapeana taarifa za kila aina na hizi za kijamii ni muhimu kwani wengi wetu ni wasafiri mikoani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom