Ngoja kwanza nikuulize isije ikawa hatuna uelewa wa pamoja katika neno kuchafuana, tukaishia kubishana wakati nakuona dhahiri umeshachoka kwenye hoja. Kuchafuana ni kitendo cha kutweza haiba, heshima ama wajihi wa mtu. Kila mtu anaweza kusimama kwa angle yake kuona ni matusi, dhihaka, kejeli ama dharau, lakini lengo zima la kuchafuana ni ili kumshusha mtu hadhi yake. Kama unataka tuamini kuwa musukuma kusema Lowassa kajinyea ni matusi na sio kuchafuana, tungeona akichukuliwa hatua. Lengo la kusema siku ile kuwa Lowassa kajinyea, ilikuwa ni kuonyesha kuwa afya yake ni mbovu na hafai kuwa rais, ndio maana Magufuli alipiga pushup kuonyesha kuwa afya yake ni njema hivyo anafaa kuwa rais. Nakushauri acha kutetea siasa chafu kisha unakuja hapa jukwaani kuzijengea hoja. Hiyo unayoambiwa kuwa cdm inakufa sio kwasababu ya mapungufu yake kama taasisi, bali ni kwa sababu ya siasa chafu unazozifumbia macho.
Jitahidi kutoka kwenye hilo box uliloingia au kuingizwa ili ujue cdm imekufa au itakufa kwa sababu gani. 90% ya kinachofanyika hivi sasa dhidi ya cdm ni nongwa na chuki binafsi za Magufuli dhidi ya cdm, ila kwakuwa yuko juu ya katiba, anaweza kutumia madaraka yake kufanya lolote na kusiwepo wa kumfanya lolote kutokana na kinga yake kwenye katiba. Nyinyi wengine wote mmejikuta mnashabikia jambo la hatari kwa kujua au kutokujua, hasa kwa huu udhibiti wa vyama vingine kufanya siasa, na vyombo vya habari kudhibitiwa, hivyo mnalishwa taarifa za upande mmoja hatimaye mnaishia kujichanganya tu huku kwenye mijadala huru. Ndio maana unaona huku mitandaoni kuna mijadala tofauti kabisa na wananchi wanacholishwa na watawala, maana humu ndani kuna mawazo huru na kinachoongelewa huku ni uhalisia, au upande wa pili ambacho watawala hawataki watu wasikie.