Naona kama pumzi imekata. Hebu tuache huku kwenye siasa nyepesi, twende kwenye siasa za hoja nzito. Katiba yetu na ccm wanaamini kuwa nchi yetu ni ya ujamaa na kujitegemea, je ni kweli nchi yetu kwa sasa inafuata siasa hiyo? Kabla ya Magufuli kuingia madarakani Kikwete pamoja na chama chake walikuwa wanatuimbisha wimbo wa uchumi wa gasi kama wendawazimu, huku Magufuli akiwa kimya kabisa tena waziri. Leo hii kaingia madarakani anasema gas sio yetu, na yeye kaingia kwenye mkopo wa ujenzi wa umeme wa maji! Je inakuwaje ccm waendelee kuaminiwa huku kauli zao zikipishana kuhusu eneo la nishati na sera ya ujamaa kutokutekelezwa, lakini utake kutuaminisha cdm hawawezi kuaminiwa kwa kusema Lowassa ni fisadi kisha kumpokea? Mwanzoni nilikuwa nakuona kama we ni mjengaji mzuri wa hoja, lakini kwa hizi hoja za siasa nyepesi nimegundua kuwa we aidha una nongwa na cdm, au ni bendera fuata upepo, ama vyote kwa pamoja. Nilikuoverate bure kumbe ni bogus fulani.