Narudia tena kusema hakuna mtu mwenye akili timamu atakubali kushirikiana na upinzani au chama kikuu cha upinzani chini ya Mbowe. Hayupo na hatakuwepo atakayebaki .
Ni bora mtu aungane na dikteta aliyeshika dola kuliko kuungana na dikteta asiye na kitu chochote zaidi ya SACCO'S.
Mbowe alikosea sana kuandaa vijana wavuta bangi kuandamana ili achukue tena uenyekiti na yeye asivyo na maarifa ya siasa za Karne hii akaingia mkenge akang'ang'ania uongozi.
Ameua upinzani chini ya Ukawa mana wote walikua wanategemea kubebwa na Harakati za Chama Cha Damokrasia na Maendeleo. Watu walitegemea kujifunza Demokrasia kupitia Chadema.
Leo hii utamshawishi nani apiganie Demokrasia kupitia Chadema.
Nani yupo tayari kutoka yeye na Mke wake na kuvunjwa miguu kama enzi za Dr.Slaa?
Nani yupo tayari kupigania Demokrasia inayoongozwa na Mbowe Tajiri mpenda madaraka asiyejali maslahi ya wanyonge zaidi ya Uenyekiti wake?
Watanzania wanataka Mabadiliko ,Watanzania wanataka Demokrasia ! Wasipoipata ndani ya Chadema wataipata nje ya Chadema.
Nenda Mbatia Jembe letu la taifa.
Tunahitaji maendeleo ya mama Tanzania sio Maeneleo ya mfuko na uenyekiti wa Mbowe na genge lake wanaotukana watu mitandaoni. Tuliona walivyokua wanamzomea Mzee wa Busara John Shibuda siku ya uchaguzi wa Chama chao. Mbowe ameshindwa kujenga siasa za kistarabu na kidemokrasia ndani ya Chadema kwa miaka 16 lakini wanataka Mh. Magufuli ajenge Demokrasia ndani ya miaka mitano.
Chadema wametanguliza Mkokoteni wakamweka Farasi Nyuma.
Angalieni mikakati ya Zito Kabwe ya kujenga Chama chake ; alistahili sana kuiongoza Chadema kwa mika sita iliyopita leo hii nguvu ya Chadema isingodhoofika kama ilivyo sasa. Waliopo ACT ndio waliokua wapinzani wa kweli. Waliokua wameandaliawa na Zito kabwe wakati akiwa Chadema . Walioandaliwa na kupewa madaraka na Mbowe wote wamekimbilia CCM kwa kununuliwa . Mbowe ameua upinzani nchini kwa kusababisha Watanzania wasiamini tena siasa za kupinga serikali kuhusu Demokrasia.
Mbowe analinda maslahi yake ndani ya Chadema kwa hiyo tumuache Mbatia aangalie kesho yake.
Ni vyema tukapata madiwani na Wabunge wa upinzani lakini Rais abaki Mh. Magufuli. Hilo halina Ubishi hakuna chama kilichojiandaa kushika dola lenye misingi ya Demokrasia. Bora CCM mana kimejipambanua kwa muda mrefu kuwa ni Chama cha Kijamaa na kinatumia dola kuendesha siasa zake. Hao wengine wajiandae kwanza na watuletee serikali iliyoiva kidemokrasia kuanzania ndani ya vyama vyao. Ni bora ACT wanaonyesha kujiandaa na wakiongeza ujuzi watachukua Dola kule Zanzibar.
Hatutaki Chama kitakachokuja kuitawala nchi hii kwa Misingi hii hii na mbinu hizi hizi za CCM.
Hatutaki chama chenye Wenyeviti miungu watu tena kiingie madarakani na kushika dola. Chadema ikiingia madarakani chini ya uenyekiti wa Mbowe nchi haitatawalika.
Tunataka Demokrasia ijengwe kuanzia chini ili tuwe na Taifa la watu wastarabu.
Mtu kuhama chama haiwezi kuwa ni uadui . Kama amenunuliwa kwa nini nyie msiwanunue kama ndio siasa za Watanzania wapenda madaraka na wabinafsi?
Bado Selesini naye namshauri tuu kiroho safi kabisa bunge likiivunjwa mwezi wa sita asipoteze muda ndani ya Chadema ya mpalestima mmoja Mbowe. Kukijenga Chadema kwa kujitolea maisha ni kumpa Mbowe umiliki halali wa Chadema.
Chadema ni chama cha mtu mmoja tuu. Anaamua anachotaka yeye na ukoo wake.
Wengine wote ni wasindikizaji tuu.October mwaka huu ndio utakua mwisho wa Siasa za Chadema na Mbowe kama mmiliki na hakuna mwenye jeuri ya kumtoa pale wala kumwajibisha kwa uzembe na ujinga alioufanya kwa kushindwa kujua kuwa watu wa ndani kabisa kwenye chama chake hawamtaki kabisa na hawapo tayari kuongozwa naye kwa sasa ndio maana wanaamua kusepa zao.
Kaka yangu Komu naye ajitafakari kama kweli alikua na ndoto ya kulikomboa Taifa hili kwa kutumia Elimu na kipaji alicho nacho basi hana Budi kutafuta chama kingine na kuachana na Dikteta asiye na Dola ,ikiwezekana ajiunge na CCM awaongoze wananchi kutafuta maendeleo ya nchi.
Hata Kileo yule aliyejaribu kule jimbo la Mwanga aachane kabisa na siasa za Mbowe na Chadema aangalie maisha yake mana Mbowe naye anaangalia maisha yake ndio maana hataki kuwa nje ya Uenyekiti wa kamapuni yake ya Chadema. Kileo asipoteze muda wake kupigania chama cha ukoo wa Mbowe kule Hai.
Watanzania wanataka Demokrasia wasipoipata ndani ya Chadema wataipata nje ya Chadema.
Sent using
Jamii Forums mobile app