Tindo
Platinum Member
- Sep 28, 2011
- 71,206
- 127,213
Siyo propaganda ni uhalisia watu walinunuliwa na wataendelea kununuliwa. Ndiyo maana nimekwambia vyama vya upinzani vyote sawa vinazidiana ma fan base tu Chadema wana fan base kubwa hasa kwenye miji na ma fan base ni ndiyo mzee ndiyo maana CCM inaiongelea zaidi Chadema kwasababu ina fan base kubwa.
Mimi siyo ndiyo mzee ndiyo maana ninahoji baadhi ya vitu na hilo linanifanya nionekane kama naipenda CCM ila kama kweli tunataka mabadiriko yaliyo ya kweli siyo mabadiriko ya eti leo kulikuwa na CCM kesho kuna CHADEMA lakini mambo ni yale yale, nina mashaka sana kama hayo mabadiriko yataletwa na CHADEMA chini ya uongozi uliopo
Kwa taarifa yako mimi ni mshabiki wa cdm tena kindakindaki, pitia post zangu toka 2011 nilipojiunga hapa jukwaani kama nimebadilika kwenye hilo. Nilipinga ujio wa Lowassa ndani ya cdm, na ninakubaliana wazi wazi kuwa kwa Lowassa cdm walichemka, na hata hivi majuzi nimepinga na ninaendelea kupinga Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm, kwani muda wake umeisha na hana jipya. Haya maoni yangu yako wazi peupe hapa jukwaani, na hata hao cdm damu damu wanajua msimamo wangu huu. Mbona mimi sionekani ni ccm? Au mimi na ww tunatolea maoni sehemu tofauti kisha tunakutana hapa jukwaani? Ninajua ninachozungumza na ninachotetea, nimegundua kama nilivyosema, ww una nongwa na cdm, bendera fuata upepo au vyote kwa pamoja, ndio maana unaishia kujichanganya tu humu kwenye mjadala.