Mbatia anawazaje kuiuza NCCR Mageuzi?

Mbatia anawazaje kuiuza NCCR Mageuzi?

Rahisi mbona, Kwani CHADEMA ilinunuliwaje na Lowassa? Kila kitu kina bei yake tu mbona ukifika bei unanunua
Ya Lowasa kuinunua chadema ilikuwa propaganda za CCM tu, lawama hakuwa na haja ya kununua chochote kwani alikuwa ana watu wengi popote angepokelewa, lakini mbatia kaona hali tete chama kilishapotea pesa za kukiendesha hakuna bora achukue pesa za bure CCM ahamie huko agombee ubunge azawadiwe uwaziri wa ujenzi apige pesa azeeke vizuri maisha yaendelee.
 
Kwa jinsi nikivyomsikia na kumsoma Mbatia amechanganyikiwa baada ya mwaliko wa ikulu. Ameanxisha uadui usiokuepo na vyama vya upinzani especially Cdm. Sijui wasomi wetu kwanini wanaingia mtego huu wa CCM ?! Nasema sijui.

Wapinzani wa kweli wampuuze Mbatia. Itakuwa Jambo jema . Kwa kadiri wanavyomjibu anapata umaarufu asiokuwa nao. Cdm wafanye nini na madhila yote wanayofanyiwa na utawala huu katili. Wameuawa, Wana kesi za uchochez karibu kila mahali, wameharibiwa mali zao etc !!
Mi nasema Mbatia apuuzwe

Sent using Jamii Forums mobile app
Na uzuri hakuna kauli yoyote ya Chadema iliyotolewa kumsema Mbatia, yeye anajishuku tu kwani siku zote wenye hatia wanakuwa waoga. Kama haya ya mitandaoni hata wanaccm wanamnanga kwa nia ya kuchochea moto. Yeye ale tu mafungu yake ya usaliti kimya kimya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikutaka kuharibu ngome ya kaskazini hasa kilimanjaro tutasikia mengi bado yule Hamsini
Huko ndipo kwenye upinzani ulipo ota mizizi
 
Inavyo onekana mbatia na chama chake wamesha fika bei kuwa sehemu ya chama cha kijani.

Sijui kama mrema na mbatia wana uhusiano wowote, tusishangae mbati kuhamia ccm mazima mazima na pengine kuchaguliwa kuwa waziri pamoja na kwamba atatoka nccr kama ilivyo kua kwa mrema.

Tatizo la mambo haya ni kwamba mwisho wake huwa u akua aibu.

Huwezi weka rekodi kwa kujiuza. Kuna watu kama kina kambona walikataa kujipendekeza, wakashikilia misimamo yenye maslahi lakini hadi leo wanakumbukwa.

Matatizo tunayo yapata leo, ni yale yale ambayo tiliyapata wakati wa kutafuta uhuru.

Kuna watu walinunuliwa na wakoloni ili wawasemee kwamba wamejenga reli, soko la kariakoo, barabara hivyo wanahaki ya kuendelea kutawala.

Pamoja na hao kulikua na kundi la werevu ambao bila kujali vitisho walisimamia wanacho kiamini na leo tunafurahia matunda ya uhuru ambao wasio itakia mema nchi hii wanataka kuturudisha kwenye ukoloni.

Mbatia unaonekana hata kwa sura umenunuliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kitu kimoja ni dhahiri kwa Mbatia ubinafsi. Alimtosa Lyatonga ili yeye awe. Anawatosa Ukawa ili yeye awe. Kwa kumwangalia mwonekano wake na afya yake hana future. Anabutua liwalo na liwe kabla ya kufika mwisho. Inasikitisha. Utavuna laana yake mbele ya macho yetu.
 
Rahisi mbona, Kwani CHADEMA ilinunuliwaje na Lowassa? Kila kitu kina bei yake tu mbona ukifika bei unanunua

Lowassa hakuinunua cdm bali aliikodisha ili imfikishe kwenye urais. Angekuwa ameinunua angekimbia?
 
Ya Lowasa kuinunua chadema ilikuwa propaganda za CCM tu, lawama hakuwa na haja ya kununua chochote kwani alikuwa ana watu wengi popote angepokelewa, lakini mbatia kaona hali tete chama kilishapotea pesa za kukiendesha hakuna bora achukue pesa za bure CCM ahamie huko agombee ubunge azawadiwe uwaziri wa ujenzi apige pesa azeeke vizuri maisha yaendelee.
Aliinunua kwasababu we hujiullizi ilikuaje Chadema kwa miaka zaidi ya 4 wanamtangaza Lowassa kwamba ni fisadi, llist of shame wanasema wana ushahidi hadi wanasema hasafishiki, wanasema anayesema Lowassa ni msafi akapimwe akili... Halafu ndani ya siku moja tu wanampa kijiti cha kuwa mgombea wa uraisi na kusema mwenye ushahidi aupeleke mahakamani. Kama hawakununuliwa walifanyaje? Kila mwanasiasa ni mchumia tumbo acha na Mbatia aangalie tumbo lake litakapopata msosi maana hakuna anayeaminika.
 
Lowassa hakuinunua cdm bali aliikodisha ili imfikishe kwenye urais. Angekuwa ameinunua angekimbia?
OOOh kumbe kwahiyo ukiwa na pesa hata ama fisadi CHADEMA inakodishwa? Kumbe la msingi uwe na pesa? Basi haina tofauti na Mbatia maana naye anatafuta ulaji sa kwanini wamsumbue au kunya anye kuku akinya bata kaharisha?
 
Wabongo wanashughlishwa sana wanasiasa,hao ni wanasiasa na wanafanya siasa sie kila siku tutabaki kuwaita wasaliti mara wamenunuliwa.
 
OOOh kumbe kwahiyo ukiwa na pesa hata ama fisadi CHADEMA inakodishwa? Kumbe la msingi uwe na pesa? Basi haina tofauti na Mbatia maana naye anatafuta ulaji sa kwanini wamsumbue au kunya anye kuku akinya bata kaharisha?

Kwani hao cdm walivyomkodishia huyo mzee tapeli la kisiasa chama watu wote waliwasifia? Huyo Mbatia anapewa ukweli wake huku mitandaoni, anaishia kujishuku. Kuna popote cdm kama chama wamesema lolote kumuhusu huyo Mbatiwa? Kama kaolewa kwingine, asianze kumnanga mume wa zamani kwa maneno ya wapambe. Amtumikie mume wake mpya bila aibu, kwani hakuna asiyejua kuwa tumbo halina adabu.
 
Alafu anakuja na mikwara mbuzi eti wakiendelea kuniita msaliti nitawataja waliokua wafadhili wa ukawa na washirika wao. Ukishawataja? Msaliti mkubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani hao cdm walivyomkodishia huyo mzee tapeli la kisiasa chama watu wote waliwasifia? Huyo Mbatia anapewa ukweli wake huku mitandaoni, anaishia kujishuku. Kuna popote cdm kama chama wamesema lolote kumuhusu huyo Mbatiwa? Kama kaolewa kwingine, asianze kumnanga mume wa zamani kwa maneno ya wapambe. Amtumikie mume wake mpya bila aibu, kwani hakuna asiyejua kuwa tumbo halina adabu.
Mimi nimejibu swali la mbandika thread kuwa ni rahisi kuuza chama tu kama CHADEMA walivyouza/kukodisha kwa Lowassa. Ni simple as that...
 
Mimi nimejibu swali la mbandika thread kuwa ni rahisi kuuza chama tu kama CHADEMA walivyouza/kukodisha kwa Lowassa. Ni simple as that...

Na mimi nimekazia ulichojibu, as simpe as that.
 
Back
Top Bottom