UHURU JR
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 18,149
- 9,562
Kumwita mtu msaliti kwa kubadili mtazamo wake ni tabia ya kutokuheshimu uamuzi wake na ni ishara ya kutokukubali kutofautiana mawazo. Lowassa alipohamia chadema hakuitwa msaliti,ila mtu anapotofautiana mawazo na chadema tu ndipo hapo utaanza kusikia akiitwa msaliti hii si sawa.Ni wapi mtu anatoka imani au chama fulani akasifiwa na watu wote? Wakati Lowassa katoka ccm kwenda cdm alikuwa anasifiwa na wanaccm wote, au waliheshimu huo uamuzi wake? Kuna kosa gani watu kuonyesha hisia zao kwa mtu asiye na msimamo?
Chadema waliacha msimamo wao waliyokuwa nao juu ya Lowassa na kumpa fisadi(Lowassa) nafasi ya kugombea urais ila hatukusikia kuitwa wasaliti kwa kuwa ni wao ndio waliyofanya ila wenzao tu ndio huwa wasaliti.