Mazuri ya Edward Lowassa

Mazuri ya Edward Lowassa

Nilishawaambieni huko nyuma, malaria imeshampanda kichwani huyu mtu -- na sasa anatoa topic hovyo tu bila ya mantiki. Again twamuomba Moids a-do somnething on this man otherwise wachangiaji wengi wenye dhamira njema na JF watapotea mmoja mmoja. Hebu fikiria JF ibakiwe na watu kama hawa pekee. Mods, please?
 
Ni vema sana angerudi ili apate 'another fatal political accident' kuisha kabisa!!
 
Ni kweli tunahitaji mtu kama EL lakini si EL mwenyewe maana kishapoteza imani yetu kwake. Mtu kama EL asiyeogopa, aliye ambitious kwa watendaji wavivu. Watendaji wetu wanahitaji mtu mkorofi na asiyeogopa kuwaambia ukweli kama EL.

Laiti kama kungekuwa na TIME TRAVEL basi EL ningependa awe Rais wa 2005 mpaka 2007 kabla ya kujisiliba uchafu kwa Tamaa ya pesa na kuendekeza biashara zake na washirika wake badala ya maendeleo ya nchi. Nchi hii kwa sasa inahitaji mtu siyo tu kama EL bali aonekane kufanya mambo aliyokuwa anayafanya EL japo hata moyoni mwake si muumini wa yale anayoyafanya.
 
Wale wote ambao Mwalimu Nyerere alituonya kuwa hawafai tukamdharau au kujisahaulisha tukawapa uongozi wameumbuka hadharani. Bado haitoshi tu jamani...mnajaribu kuwasafisha watu ambao hawatobadilika tabia zao hata wabatizwe kwa maji ya moto.
 
Nilishawaambieni huko nyuma, malaria imeshampanda kichwani huyu mtu -- na sasa anatoa topic hovyo tu bila ya mantiki. Again twamuomba Moids a-do somnething on this man otherwise wachangiaji wengi wenye dhamira njema na JF watapotea mmoja mmoja. Hebu fikiria JF ibakiwe na watu kama hawa pekee. Mods, please?

Kama huna cha kuchangia si acha mbona unamfuatilia mwenzio mbona watu wengi tu weame respond? na wengi tu wamekaa kimya?
 
Namkubali sana mzee pinda, namkubali sana huyu kiongozi wangu wa nchi kwa kuwa ni mchapakazi.lkn ningalitamani waziri mkuu mstaafu El kurudi tena bungeni na kuwa waziri mkuu , kwani licha ya kuwa mkali kwa watumishi wabovu, lkn pia utendaji kazi wake hasa pale alipoamuru bandari ya dsm kufanya kazi masaa 24 pale nimemkubali na matunda yake tumeyaona
Unaonyesha jinsi usivyoipenda inji yako!
 
Lowassa arudi tena kama Waziri Mkuu? Is this a joke?

We may be desperate for good leadership in Tanzania -- but we are not that desperate. EL alilazimika kujiuzulu kutokana na kashfa ya Richmond, si kwa swala la accountability ni kwa kuwa alihusika moja kwa moja na kashfa hii. Yeye ndiye aliyeunda kamati kushuhulikia tenda nzima na aliisimamia kwa karibu sana.

Kamwe huwezi kumtenganisha EL na kashfa ya Richmond. Huyu mtu pamoja na kusifiwa eti kuwa mchapa kazi, amekaa ki biashara zaidi. Anapenda mali na utajiri, ni hodari kwa ujasiriamali. Tanzania haihitaji viongozi wajasiriamali. Nyerere alishawahi kusema, huwezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja -- yaani pesa na wananchi. Ni ukweli usiopingika kuwa serikali iliyopo imeshindwa kazi. Lakini sie Lowassa.

Ndani ya CCM kuna viongozi wengi waadilifu wanaofaa kuwa PM. Huyu mtu hafai kabisa kuongoza nchi. Kufanya kosa mara moja kwa kumfanya Lowassa Waziri Mkuu ni aibu tosha, tukirudia tena kosa hili itakuwa ni upumbavu wa hali ya juu. Mungu iepushe Tanzania ya Nyerere na kiama cha Lowassa kurudi madarakani.

Sijashangaa mada hii kuja hivi sasa. Huu ni mpango madhubuti wa kutaka kuleta mapinduzi haramu ya kurejesha Lowassa na timu yake serikalini. Watanzania tuwe macho na ujasiri huu wa kifisadi. Never again, never again, never again!
 
Ninyi. Mnaomfagilia huyu fisadi mnahitaji maombezi. Hakuna Mtanzania mwenye akili timamu atamfikiria mtu kama Lowassa kurejea kwenye uongozi. Nchi hii sasa inahitaji ukombozi baada ya kunyonywa na watawala dhalimu kwa muda mrefu na kukwamisha maendeleo yetu. Hata huyo rafiki yake, JK hastahili tena kipindi kingine cha miaka mitano. Hawa watu wameichezea sana nchi yetu na kuididimiza kwenye dimbwi la umaskini. Sehemu pekee wanayostajili kuwepo ni jela!
 
Nilishawaambieni huko nyuma, malaria imeshampanda kichwani huyu mtu -- na sasa anatoa topic hovyo tu bila ya mantiki. Again twamuomba Moids a-do somnething on this man otherwise wachangiaji wengi wenye dhamira njema na JF watapotea mmoja mmoja. Hebu fikiria JF ibakiwe na watu kama hawa pekee. Mods, please?
Hizi chuki binafsi! What is wrong with that thread? Is there any insult from that topic? He/she is speaking his/her mind! He like Lowasa and He would be very delighted to see him back as a PM. Well..... if you dont like Lowasa Im afraid you gt to live with it because some do like Him!
 
Ninyi. Mnaomfagilia huyu fisadi mnahitaji maombezi. Hakuna Mtanzania mwenye akili timamu atamfikiria mtu kama Lowassa kurejea kwenye uongozi. Nchi hii sasa inahitaji ukombozi baada ya kunyonywa na watawala dhalimu kwa muda mrefu na kukwamisha maendeleo yetu. Hata huyo rafiki yake, JK hastahili tena kipindi kingine cha miaka mitano. Hawa watu wameichezea sana nchi yetu na kuididimiza kwenye dimbwi la umaskini. Sehemu pekee wanayostajili kuwepo ni jela!
Mzee Punch,
Hili ni suala la mtizamo kati ya mtu mmoja na mwingine. Wakati wewe unampenda fulani mimi naweza nikawa simpendi kabisa.
Let people miss EL. Frankly speaking pamoja na udhaifu wake jamaa binafsi nammiss kwa sana.
Naamini binafsi tuki-trace Richmond JK utamweka wapi rafiki yangu?
Kama mshirika wake mkuu kisiasa kanasa kwa nini nae JK asiwemo? tunazugana hapa
 
Kama unampenda kiasi hicho hata baada ya kukuibia and you know it tena unawafahamu na wengine wengi walioiba naye! Then Mzee Puch is right Unahitaji maombi tena maombi ya kukesha mlimani!!!!
 
Maadam kuna watu wanaofikiria kwamba EL alikuwa kiongozi mzuri basi bila shaka tuna matatizo ya Kiakili...inabidi sisi wananchi wenyewe tukapimwe akili zetu. Na kama asemavyo yule mhindi...upo uwezekano mkubwa wa kupungukiwa IQ..
 
Binafsi nashangaa kuona watu wanamtaka Lowasa lol! Ama kweli Waafrika tuna matatizo makubwa ya akili na ufahamu. Ndo maana wazungu wanatuona kama mazezeta. Yaani mtu mwizi wa wazi wa mali ya umma, arudi kuiongoza nchi? No, no, no, no. Huo utendaji wake unaosifiwa na watu hapa kwanza ni kinyume na maadili ya uongozi. Utawaaibishaje viongozi mbele ya watu wanaowaongoza? Kwanini asikae nao na kuwakemea pembeni kama anaona kuna matatizo. Na kwa ujumla alikuwa anakemea viongozi wa chini sana akiwaacha wakubwa wenzake ambao walikuwa wanalididimiza taifa kiuchumi. Yeye mwenyewe ana hisa kwenye makampuni mengi yanayoinyonya nchi hii ikiwemo TICS.
 
Mtakumbuka kuwa wakati ule El akiwa waziri Mkuu, jamani kazi ilikuwa inafanyika. sio wakurugenzi, watendaji wa manispaa, Halmashauri, Kata, mpaka kijiji, kamati za ujenzi wa shule zetu za kata-- n.k. tulishaanza kupata morali ya uwajibikaji na kuondokana na mambo yetu yale ya kufanya kzai kwa mazoea...yote hayo sababu ya ufuatiliaji wa karibu wa Mh. EL. Ameondoka tu,unaona mambo yamezorota, watendaji wa serikali wakapata ahueni kuzembea na wametafuna fedha za umma, ndo haya tunayoyaona kufikishana mahakamani kila kukicha...zile shule zetu za kata zimejengwa mpaka lenta nas wananchi...kumaliziwa na Serikali sijui itakuwa lini?. Namuombea |Mungu amjalie achaguliwe tena kwenda Bungeni na pengine apate nafasi ile au zaidi.
 
jamaa, aliteleka akaanguka. Kama ni utendaji huwezi kumlinganisha na yeyote ktk serikali hata wa juu kabisa. aangukaye husimama. Na tukubali kuwa amesimama.
 
Sorry, Maovu yake yamefunika mazuri yote, hilo hata watu wa Mondulu wanalifahamu. Mhuni huyo!
 
Back
Top Bottom