Kiwanda kipo ZNZ. Wanaimport maziwa unga wanaprocess. Jiulize kwanini kiwanda hakikuwekwa bara ambako kuna maziwa mengi ya ngombe na walaji pia ni wengi?
By the way kwa Tanzania hiiiii maziwa ya ngombe ninayo trust siyo ya kutoka kiiwandani.
niongeze kwa kuwahabarisha kuwa: kwa wale mnaonunua maziwa fresh toka kwa wafugaji kuna umuhimu ujiridhishe kuwa hayajachakachuliwa. wauzaji wa maziwa wanaongeza maji kufanya yawe mengi kupata faida zaidi. ili kuficha huu ujanja huwa wanaweka vitu vya ajabu kama unga wa ngano, blue band etc kuyafanya yaendelee kuwa mazito. But ni hatari kwa afya hasa ya mtoto mchanga. Mtoto aweza kuharisha, kudumaa kwa kukosa virutubisho muhimu vya hayo maziwa na pia long term impact kwenye ini na figo. Hivyo basi namna rahisi ya kubaini kama maziwa fresh yamechakachuliwa ni: i. chovya njiti ya kiberiti halafu iwashe, isipowaka yametiwa maji
ii. mwaga kijiko kimoja cha maziwa kwenye sakafu, kama yameongezwa maji yatajitenga
iii. chukua glass weka maziwa fresh kiasi halafu kamulia ndimu au tone la alcohol (bia, konyagi) yasipokatika ni dalili pia yameongezwa maji.
Maziwa ni muhimu sana kwa afya ya inadamu hasa watoto na wazee. Tuingatie haya kwa afya bora za watanzania.