Mazito ripoti ya CAG - Janeth Rithe: Matrilioni yatumika ‘juu kwa juu’... Serikali hoi kwa madeni! Ahofia ‘EPA’ nyingine BoT

Mkuu asante vile umenielewa, Mimi nitaiamini tarifa hii ya Zitto iwapo itathibitishwa na Mwingine, Kwa sababu Kwa sasa, Zitto amekuwa kama ni mtu wa jinsia moja hivi ktk Imani furani, akisimama atoe ushahidi wa Yeye peke yake hautakubalika, ushahidi wa jinsia hiyo hukubalika tu pindi watoa ushahidi watakapokuwa ni zaidi ya mmoja, ni Sawa na alivyo Mh Zitto Kwa sasa, haaminiki na hawezi kuaminiwa

Tangu alipokisaliti Chama chake kilichompa umarufu, amekuwa haeleweki na hatokuja kuaminika ni Hadi atubu,

Uteuzi wa CAG ulimsikia alichokisema mkuu? Sasa Iweje leo ripoti za CAG ambaye yeye alimzodoa huku akisema ni Magufuli wa pili, eti leo aanze kuona ni za Moto Kwa Magufuli kweli?

Mimi simwamini, Iweje leo hii Kwa ripoti hii aone inamtenganisha Magufuli na CAG?

Mwamini wewe mkuu
Humuamini Zitto , Sawa. Je taarifa za CAG unaziamini ?!. Kama waziamini lete ripoti inayopingana na taarifa za Zitto.

Odhis *
 
Mbona kuna hoja za msingi ambazo kazitolea ufafanuzi mnaaza kuzikimbia hoja mapema hivi?
Unajua nini Mkuu, omba Sana Mungu akupe kuaminika Kwa watu na istokee ukawa msaliti Kwa vitu vile ambavyo vimekufanya uaminike Kwa watu

Mkuu huyo mwanasiasa ni Mzuuri haswaaa, na kiukweli kabisa ukimwondoa Tundu Lisu Kwa upinzani pengine anayefuata ni Yeye, Tatizo alilonalo na huenda likagharimu mwenendo wa Siasa zake ni Uwongo uwongo mdogomdogo, unamshushia Sana Heshima huyu mwanasiasa Machachari na makini, Rejea kuvumisha kupotea hewani Kwa aliyekuwa CAG wa enzi hizo, Rejea agenda zake za kukiuza Chama chake Cha zamani!!!
 
Unajua nini Mkuu, omba Sana Mungu akupe kuaminika Kwa watu na istokee ukawa msaliti Kwa vitu vile ambavyo vimekufanya ukaaminika,

Mkuu huyo mwanasiasa ni Mzuuri haswaaa, na kiukweli kabisa ukimwondoa Tundu Lisu Kwa upinzani pengine anayefuata ni Yeye, Tatizo alilonalo na huenda likagharimu mwenendo wa Siasa zake ni Uwongo uwongo mdogomdogo, unamshushia Sana Heshima huyu mwanasiasa Machachari na makini, Rejea kuvumisha kupotea hewani Kwa aliyekuwa CAG wa enzi hizo, Rejea agenda zake za kukiuza Chama chake Cha zamani!!!
Ninachompendea Zitto ni pale anapowanyima ccm usingizi wa pono anajua haswa kuwavuruga
 
Tz ni chama kipi tunaweza kiko purely opposition.
Mimi nilikuwa ccm kwa muda mrefu kabla ya kukihama
Trust me ccm inakiogopa sana sana chama cha demokrasia na maendeleo hadi kufikia kukubali kuwa bila kucheza rafu chadema kitawang'oa madarakani

Kwa muktadha huo ninaweza kusema bila wasiwasi kuwa CHADEMA ni chama cha Upinzani tena kinachokuwa kwa kasi
 
ZITTO AJIBIWA KWA MIKWAJU 10 YA KAFULILA.soma iyo!

NATOFAUTIANA NA ZITTO KUHUSU RIPOTI ZA CAG NA MWENENDO WA UCHUMI

Na David Kafulila!
Aprili 12,2020-SONGWE

Aliyekuwa Rais wa Marekani, George W.Bush alipata kusema kwamba uongo ukirudiwa una nafasi ya kugeuka kuwa ukweli wa watu! Pengine ni sababu hiyo, pamoja na kupongeza uamuzi wa Mhe. Zitto Kabwe kama Kiongozi wa Chama Cha Upinzani kuchambua mwenendo wa awamu ya tano katika muktadha wa uchumi na utendaji kwa kurejea ripoti za CAG, napenda kutoa maoni yangu binafsi katika mafungu10 kutofautiana na uchambuzi wake kwa lengo la kuwekana sawa kwa faida yetu sote kama watanzania!

1. Hoja kwamba Serikali ya JPM imeshindwa kukusanya mapato kulinganisha na awamu ya nne ina matobo matatu;

Kwanza Zitto ametoa ulinganisho wa miaka3 ya mwisho wa awamu ya nne na miaka 3 ya kwanza ya JPM kwa kutaja kiasi na asilimia ya makadirio( estimates)na makusanyo(actual collections)kwa upande wa awamu ya 5 lakini akaishia kutaja asilimia ya kutofikiwa lengo bila kutaja kiasi halisi kilichokusanywa katika miaka hiyo 3 ya mwisho wa awamu ya nne.Najua alivokuwa anakwepa!

Zitto kafanya hivyo kwa makusudi kwasababu alijua kwamba kwa mujibu wa ripoti hizo za CAG, makusanyo ya miaka3 kamili ya mwisho ya awamu ya nne( 2012/13, 2013/14 na 2014/15) yalikuwa sawa na jumla ya TZS.28trilioni karibu sawa na makusanyo ya mwaka 1 tu wa 2017/18 chini ya JPM yaliyofikia TZS.27.7Trilion.

Kwa ufafanuzi zaidi ni kwamba, makusanyo ya miaka ya 2012/13 (TZS.8Trilion), 2013/14( TZS.9.28Trilion.) , na Mwaka 2014/15 ( TZS.10.77Trilion) sawa na jumla ya (TZS.28Trilioni) ambayo ni sawa na makusanyo ya kodi ya mwaka mmoja tu (2017/18) chini ya JPM.

Kifupi kulinganisha uwezo wa kukusanya kodi kati ya awamu ya4 na awamu ya 5 inahitaji kuwa na nia OVU kupotosha au chuki binafsi kwani hizo awamu mbili ni mlima na kichuguu katika eneo hilo.

Kifupi makusanyo ya awamu ya nne kwa mwezi yalikuwa wastani wa TZS. 850bn, kiasi ambacho hakikutosha hata kumudu malipo ya deni la Taifa kwa mwezi na mshahara. Malipo ya deni kwa mwezi yalikuwa wastani wa 650bn, na Mshahara kwa mwezi ilikuwa wastani 550bn sawa na 1100bn. Hivyo ilibidi kukopa kuweza kumudu kulipa mshahara.

Pengine ndio msingi wa kejeli za Rais Uhuru Kenyatta miaka hiyo kwamba ilikuwa Kenya peke yake katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyoweza kumudu kulipa mshahara watumishi wake bila kukopa.

Wastani wa makusanyo ya sasa ya kodi tu kwa mwezi yanatosha kumudu deni na mshahara na hivyo Serikali haikopi tena kulipa mshahara watumishi wake.

2. Hoja kwamba Serikali inakopa sana ndani na hivyo kuathiri fursa ya sekta binafsi. Hoja hii ina matobo ya aina mbili;

Kwanza inafahamika sura ya deni la Taifa mpaka sasa asilimia 75% ni la nje na hivyo deni la ndani ni asilimia25%. Katika mazingira ya kawaida inashauriwa Serikali ikope zaidi ndani ili inapolipa fedha hiyo sehemu kubwa ibaki kwenye uchumi ndani badala ya kwenda nje.

Pili, Serikali ingeathiri sekta binafsi kama ingekopa kwa riba kubwa kwani kwa kufanya hivyo ingesababisha riba za benki za biashara kwa sekta binafsi kupanda kwani moja ya kigezo cha kiwango cha riba za benki ni kiasi cha riba katika soko la hatifungani( TBs auctions).

Aidha Serikali ingekuwa inakopa kwa riba kubwa ingesababisha watu binafsi wenye ukwasi kukopesha zaidi Serikali kuliko kuweka bank au kuwekeza maeneo mengine ya uzalishaji.

Kwa mujibu wa ripoti za Benki Kuu kuhusu minada hiyo, Mwaka 2020, Serikali inakopa soko la ndani kwa riba isiozidi asilimia 5% kwa mikopo ya siku365 kulinganisha na riba ya silimia 17% mwaka 2015.

Kutokana na Serikali kukopa soko la ndani kwa riba chini ya asilimia 5% kulinganisha na asilimia17% mwaka 2015, ni moja ya sababu ya riba za bank za biashara kushuka kutoka asilimia 24% mwaka 2015 mpaka asilimia 16%.

3. Hoja kwamba Serikali inaficha madeni ya mifuko ya hifadhi. Hii ina matobo ya aina tatu;

Kwanza ni changamoto ya madeni yenyewe kwa namna yalivyopatikana. Sio siri kwamba kabla ya JPM, mifuko ya hifadhi iligeuzwa shamba la bibi na mali ya genge fulani.Huu ni ukweli unaothibitishwa na taarifa ya taasisi ya kimataifa ya ukaguzi ya E& Y ya Disemba2015, habari za uchunguzi za majarida makubwa ya kimataifa kama Africa Confidential na Africa Research Institute.

Kwa mfano, Ujenzi wa Chuo Kikuu UDOM, mifuko ilikuwa ikidai jumla ya TZS 5.3Trilioni lakini baada ya ukaguzi deni halali likakutwa TZS.3.2Trilion sawa na deni hewa la zaidi ya TZS.2.1Trilion.

Sielewi Kiongozi anaesisitiza deni lilipwe kama lilivyo kama kweli ana mapenzi na watanzania walipa kodi? Hata kama hana mapenzi na walipa kodi wa nchi hii vema awe japo na huruma basi!

4. Hoja kwamba Serikali ya JPM ina kesi nyingi kwa kuvunja mikataba.
Hapa ni vema ikaeleweka kwamba;

Kwanza kesi hizo ni matokeo ya mikataba mibovu ya zamani ambayo JPM amerithi kutokana na udhaifu mkubwa huko tulikotoka na sio mikataba ndani ya awamu ya tano

Mfano, uamuzi wa Serikali kufuta mkataba wa kampuni ya kufua umeme ya Symbion iliyorithi mitambo ya Dowans/ Richmond, imepunguza mzigo wa kinachoitwa tozo ya gharama ya uwekezaji (capacity charges) kwa mwezi kutoka dola milioni 16.35 (zaidi ya bilioni 37.6) mpaka dola milioni 9.75 (sawa na bilioni 22.4) kwa mwezi( Rejea CAG report 2017).

Inahitaji ukatili sana kwa Taifa lako kumlalamikia JPM kufuta mikataba mibovu kama Symbion kwani kinachoitwa tozo ya ya gharama za uwekezaji ni mfano wa mbaya wa mikataba ya hovyo ambapo mwekezaji analipwa bila kujali amezalisha umeme au la eti kufidia gharama alizotumia kuwekeza.

Vema kufahamu kwamba zama za Serikali kulipa madeni ya mikataba mibovu tumeshavuka. Huko tulikotoka Serikali iliwahi kulipa deni la Dowans kinyemela kiasi cha dola milioni 94 (zaidi ya bilioni 200 wakati huo). Hakika inahitaji roho kutamani zama hizo, ni Taifa la 'wapumbavu' linaloweza kupigania Serikali yao ilipe madeni ya aina hii!

5. Kwamba Serikali ya JPM ni ya ufujaji! Labda nikubaliane kwamba vita dhidi ya Ufisadi ni endelevu duniani kote na inaendelea Tanzania. Hata hivyo inahitaji upofu kusema Serikali hii inatatizo hilo kuliko tulikotoka. Unaweza ukabaki peke yako kwani hali halisi na Tafiti zote kitaifa na kimataifa zinathibitisha mapinduzi makubwa eneo hili;

Mwaka 2019, Serikali ya Tanzania ilitangazwa kuwa ya 28 duniani kwa usimamizi madhubuti wa fedha za Umma( World Economic Forum,Executive Opinion Survey 2019).Kwa mujibu wa Ripoti hiyo, nchi za Kenya ilishika nafasi ya 70, Uganda 100, Ethiopia 48, Malawi 106, Msumbiji 118 , Ghana 61, Zambia 68 na Botswana 37.

6. Hoja kwamba Serikali imeshindwa usimamizi wa uchumi, Hapa nisiguse mapinduzi makubwa sekta za miundombinu, maji, Elimu na Afya..twende na ripoti za Tafiti tu;

Mwaka 2017, kwa mara ya kwanza katika historia, ilifanyiwa uhakiki kuhusu uthabiti wa kiuchumi kuweza kukopesheka (Credit rating), kazi hii ilifanywa na Taasisi ya Moody's ambayo ni ya kwanza kwa ukubwa duniani katika kazi hizi (inamiliki asilimia 45% ya soko), ilitoa matokeo yake mwezi Machi2017, kuonesha kwamba Tanzania ina daraja la B1 juu ya Kenya, Uganda ambazo zilikuwa na B2. Ripoti hii ilizua mjadala mkali sana Kenya (Business Daily, 4th, March2017).

Mwaka 2018, Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa uchumi jumuifu( Inclusive Economy), na ya tatu kwa bara zima ikitanguliwa na Algeria na Tunisia (World Economic Forum 2018). Sikatai kwamba kuna mengi ya kufanyia kazi zaidi, lakini rekodi hizi ni kubwa na fahari kwetu kama Taifa kwamba tunakwenda vizuri katika maeneo mengi kuhusu ujenzi wa uchumi

Mwaka 2017, IMF, iliitaja Tanzania kuwa miongoni mwa Mataifa manne ya Afrika yanayoelekea safari ya Vietnam katika ujenzi wa uchumi wa viwanda. Nchi zingine ni Nigeria, Kenya na Ethiopia. Rejea mahojiano ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi Christine Lagarde, alipohojiwa na Jarida la Quartz akiwa Addis nchini Ethiopia alipotembelea Tume ya Umoja wa Mataifa kwa Uchumi wa Afrika (UN- Economic Commission for Africa).

7. Hoja za Mhe. Zitto kutaka watanzania wapoteze imani na Serikali kwa hoja za kuokoteza ni kupoteza muda. Tazama ripoti hizi;

Mwaka 2019, Tanzania ilitajwa kuwa nchi ya 96 kati ya nchi 186 duniani katika vigezo vya kupambana na rushwa. Mwaka 2015 kabla ya JPM, Tanzania ilikuwa ya 119. (Rejea Ripoti ya Transparency Internation 2019).

Mwaka 2019, Tanzania ilitajwa kuongoza Afrika katika nchi 35 zilizofanyiwa utafiti kuhusu imani ya wananchi kwa Serikali katika vita dhidi ya rushwa. (Transparency International, Global Corruption Barometer 2019 report).

Ripoti hiyo hiyo ya kimataifa imeonesha kwamba asilimia 72% ya watanzania mwaka 2019 wanaamini kuwa Serikali yao inapambana na rushwa kulinganisha na asilimia 13% mwaka 2015.

8. Mapinduzi makubwa Sekta ya miundombinu na rasilimali watu yanaonekana bayana kwa kila mtanzania. Naamini kasi ya sasa ingekuwepo miaka 30 nyuma, ni wazi leo tungekuwa washindani wa Mataifa kama Vietnam.

Kwa mujibu wa Benk ya dunia,kufikia mwaka 1990, uchumi wa Tanzania ulikuwa dola 4.5bn nyuma ya Vietnam ikiwa na dola 6.5bn huku Kenya ikiwa mbele ya Vietnam kwa uchumi wa dola 8.4bn. Leo mwaka 2020, ikiwa ni miaka30, Uchumi wa Vietnam ni dola 260bn, ikiipita Kenya yenye dola bilion 90 na Tanzania dola 60bn.

Ujenzi wa miradi mikubwa kimkakati kama Stirglers Gorge utakaozalisha umeme zaidi ya 2100MW na Ujenzi wa Reli ya kati ya sanjari na kufufua shirika la ndege ndio majibu kuelekea huko.

Ni sisi watanzania tuliopiga kelele Serikali kumiliki ndege1 tena mbovu na wakati mwingine kukodi ndege kwa gharama kubwa kuliko gharama ya kununua (CAG report 2015/16). Nisisi tuliopiga kelele reli iliyozeeka kutoka uwezo wa tani milioni 5 mpaka tani laki4.

Nisisi tuliopiga kelele kuhusu sekta ya umeme ilivyonyonga uchumi wetu kwa biashara za mitambo ya kukodi ambayo imekamua uchumi na kuacha nchi mifupa mitupu.

Kinachofanyika sasa ndio safari kuelekea vietnam japo ilipaswa tuanze zamani.Mikopo kwa miradi ya kimkakati kama hii ina uhalali kulinganisha na tulikotoka ambapo tulikopa kulipa mishahara na kuendesha Serikali (Recurrent Expenditure)

9. Hoja ya ujenzi wa rasilimali watu. Haihitaji miwani kuona mapinduzi makubwa haya. Sekta ya Elimu, Afya na Maji zimepiga hatua kubwa. Tafiti zinaonesha kwamba kila dola1 inayowekezwa kwenye maji inaokoa dola 4.2 ambazo zingewekezwa kwenye dawa ambazo ni matokeo ya tatizo la maji safi. Kuna mafanikio makubwa lakini changamoto za sekta hii kwa kiasi kikubwa ni miradi ya kurithi tulikotoka.

Kuongeza mikopo elimu ya juu kutoka 360bn mwaka 2015 mpaka 450bn ni juhudi zilizo bayana. Kupeleka 23bn kila mwezi kuhakikisha Elimu- bure ni ndoto iliyogeuka kweli na kusababisha takribani watoto 1m waliokuwa wakikosa shule kila mwaka sasa wanasoma.Changamoto za ubora ni suala endelevu kuhakikisha tunazalisha nguvu kazi yenye uwezo wa kuhimili ushindani wa soko la ajira.

Aidha mapinduzi ya Sekta ya afya nayo ni bayana. Ripoti za NHIF zinaonesha mwamko mkubwa kwa watanzania kuwa na bima ya afya kutoka milioni 9 kabla ya awamu ya tano mpaka zaidi ya milioni16.

Ongezeko la fedha za dawa na vifaa na tiba kutoka 31bn mwaka 2015 mpaka 269bn sawa na ongezeko la zaidi ya asilimia 700% ni mafanikio ya mfano.

Ripoti ya Shirika la Afya duniani (WHO) zinaonesha kasi ya maambukizi ya malaria kushuka kutoka asilimia 14% mwaka 2015 mpaka asilimia7%.

Hii msingi wake pamoja na mambo mengine, ni ongezeko la upatikanaji dawa kiasi kwamba mtu mwenye malaria haimchukui muda mrefu kupona hata kuambukiza wengine kabla hajapata matibabu kutokana na ukaribu wa huduma za Afya kuanzia ngazi ya Zahanati mpaka Hospital ya Mkoa.

10. Nihitimishe kwa kurudia kauli ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Bi.Thereza May na falsafa yake ya kuendesha Serikali inayozingatia maslahi ya wote ikiwemo wasio na sauti (Government works for all).

Alisema kwamba ni kiu ya waingereza kuona Serikali ya namna hiyo, lakini sio jambo jepesi kulitimiza kwa muda mfupi, linahusu kuyakabili maslahi ya wachache ambao kwa muda mrefu walifanya Serikali iendeshwe kwa maslahi yao. Naye aliyekuwa Rais wa Marekani JF. Kennedy alipata kusema kuwa Kiongozi bora ni yule anayesimamia maslahi ya Umma hata kama kwa kufanya hivyo atachukiwa na jamaa zake na hata makada wa chama chake.

Kifupi haya mawili ndio nayatazama kama mapito ya JPM. Anajenga msingi wa Taifa ambalo tuendako kijana hatokosa fursa ya elimu bora kwasababu ya umasikini wa wazazi wake, wala mama hatokosa huduma ya afya sababu ya umasikini wa familia yake au mume wake!

Kufumua na kusuka upya Taifa lilodumu kitambo katika uchumi wa 'missiontown' kuna changamoto nyingi ingawa tupo kwenye mstari sahihi!
 
Mimi nilikuwa ccm kwa muda mrefu kabla ya kukihama
Trust me ccm inakiogopa sana sana chama cha demokrasia na maendeleo hadi kufikia kukubali kuwa bila kucheza rafu chadema kitawang'oa madarakani

Kwa muktadha huo ninaweza kusema bila wasiwasi kuwa CHADEMA ni chama cha Upinzani tena kinachokuwa kwa kasi
Holy shit. Kumbe CDM ni wakali kiasi hicho

My life is mine to remember
 
Binafsi nimeshindwa kuelewa kwanini amemtumia huyo Bidada badala ya kusimama yeye kama yeye!!!
Kafulila kamvua nguu kwenye uongo wa jana. Sasa kaona aje kivingine ili akiumbuliwa ionekane si yeye
 
Zile habari kwamba Magufuli kadhibiti upigaji, karudisha nidhamu serikalini, zinatetewaje kwa ripoti kama hii?

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Uli
Ni huyu huyu Zitto ambaye aliapa kwamba CAG aliyepo sasa ni Magufuli mwingine, hawezi kumwamini na hatomwamnini imekuweje leo atuletee habari hizi?

Ripoti ya CAG naiamini Ila haya yaliyoletwa na Zitto siyaamini kama ambavyo yeye alitangaza kutomwamini CAG
Acha kukaa ndani ya chupa! Ulifuatilia alichopresent au ndo umeishia kusoma hiki kiduchu humu!!! Mbona ameongelea na mambo ambayo CAG hakugusa kabisa kama mikopo ya sirikali kwenye mashirika ya umma!!!
 
Back
Top Bottom