Mazito ripoti ya CAG - Janeth Rithe: Matrilioni yatumika ‘juu kwa juu’... Serikali hoi kwa madeni! Ahofia ‘EPA’ nyingine BoT

Mie ngoja nimwamini zitto, kwanza maelezo yake yanaonyesha hakuna ubadhilifu Ila kasoro katika uwekaji hesabu na kimsingi sio kasoro Ni upotoshaji wake tu kwani hakuna taratibu zilizokiukwa.

Kuhusu budget na makusanyo anaongelea tofauti za asilimia Kati ya jk na JPM lakini hasemi tofauti ya fedha,

Kusema kuwa mizigo haijavuka mipaka haimaanishi imeibiwa, hasemi Ni mizigo mingapi iliyotolewa lakini iko kwenye ma godown au kwenye mafuso kuelekea mpakani
Unatuletea story za LUGOLA na unifomu za Polisi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
¶ Mbinu ya Jiwe a.k.a Meko likely itakuwa ni ile ile kama ya 1.5trn ya kuitisha kikao kingine cha "makinikia" ili kujijitetea akiwa na serikali yake yote;

• Mawaziri wake wote
• IGP
• CDF
• Spika
• Jaji Mkuu
• Gavana - BoT
• Na mtu kati atakuwa CAG Kicheere na vijana wake

¶ SWALI KWA CAG Kicheere litakuwa lile lile "chakavu" la;

"....eti, CAG kuna ufisadi wa trillion 1.7 serikalini au hakuna....🤓🤓🤓🤓!!!??"

"....na eti wizara ya maliasili na utalii kuna ufisadi au hakuna....:oops::oops::oops:

😃😃😃!!!??"

Zito Kabwe ni mwanasiasa very technical sana....

Kwa hoja hizi, kwa hakika kabisa lazima serikali yote iamke na kukimbia mbwito mbwito kujaribu kufunika kombe ili mwana haramu spite....

Lakini this time sina hakika kama mwanaharamu huyo atapata mlango was kupitia...!!
 
Zitto aibua mazito ripoti ya CAG

• Matrilioni yatumika ‘juu kwa juu’
• Serikali hoi kwa madeni
• Aifananisha na mchana
• Ahofia ‘EPA’ nyingine BoT

SERIKALI ya Tanzania imevunja Katiba kwa kutumia kiasi cha shilingi trilioni 1.7 bila ya kupitia Mfuko Mkuu ambao hukaguliwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amewaambia waandishi wa habari jana.

Katika mkutano na waandishi wa habari alioufanya jijini Dar es Salaam jana kuhusu uchambuzi wa chama chake kwenye Ripoti ya CAG ya mwaka 2018/2019, iliyowasilishwa bungeni wiki iliyopita, Zitto alisema jambo hilo ni baya kwa sababu linaruhusu fedha za Watanzania kutumika pasipo kukaguliwa.

Alisema kwa kutambua umuhimu wa kulinda fedha za umma, Katiba iliweka ofisi ya CAG iwe inakagua mapato na matumizi yote ya serikali lakini uchambuzi wao umebaini matumizi ya shilingi trilioni 1.7 ambayo hayajakaguliwa na ofisi hiyo.
“Katika mwaka wa fedha wa 2018/2019, serikali ilitumia shilingi trilioni 1.7 bila kwanza kupitia kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali. Baadhi ya fedha hizi zinatokana na mikopo kutoka nje.
“Hizi shilingi trilioni 1.7 zinazotokana na mikopo kutoka nje zimelipwa hukohuko; kwa mfano kununua ndege za ATCL na zinaweza pia kuwa zimetumika kuwekwa kwenye akaunti za watu binafsi huko nje. Utaratibu huu ni kichaka cha kukwepa kukaguliwa na CAG ili kufanya ubadhirifu,” alisema Zitto.

Zitto ambaye kitaaluma ni mchumi na amewahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (PAC) kwa takribani miaka minane, alifanya uchambuzi wake kwa kuangalia ripoti hiyo yam waka huu lakini akaangalia kwa ujumla rekodi ya serikali tangu kuingia madarakani kwa Rais John Magufuli.

Uchambuzi wa ACT Wazalendo uliangazia maeneo makubwa kumi ambayo uchambuzi umeonyesha serikali ndiyo chanzo cha hali ngumu ya uchumi –maarufu kwa jina la “vyuma kukaza” kwa sababu ya kufanya mambo yanayochangia hali hii.
Kwa mfano, Zitto aliwaambia waandishi wa habari kwamba kiwango cha serikali kudaiwa na wazabuni, kulipa deni kubwa la taifa na kukopa kupita kiasi ni mambo ambayo yamesababisha kunyausha uchumi wa Tanzania.

Akizungumza kwa takwimu, mbunge huyo wa Kigoma Mjini, alisema katika miaka mitatu ya kwanza ya utawala wa Rais Magufuli, wastani wa kiwango cha kutofikia lengo la makusanyo kilikuwa ni asilimia 16.

Alisema Deni la Taifa sasa limefikia kiasi cha shilingi trilioni 53 na mzigo wa kulihudumia umekuwa mkubwa kwa sababu sasa zinahitajika shilingi trilioni 10 kulihudumia kulinganisha na shilingi trilioni 6.3 wakati anaingia madarakani.

Kiwango hicho, mujibu wa Zitto, kinamaanisha kwamba sasa zaidi ya nusu ya makusanyo yote ya ndani ya Mamlaka ta Mapato Tanzania (TRA) yanatumika kwenye kulipia deni hilo pekee.

Uchambuzi wa ACT Wazalendo uliotangazwa na Zitto jana umeonyesha pia namna wafanyabiashara wanavyokwepa kodi kupitia bandari ya Dar es Salaam; ambapo bidhaa zenye thamani ya shilingi bilioni 312 zilidaiwa kupitishwa bandarini kama zinakwenda nje ya nchi lakini hakuna ushahidi kwamba kweli ziliondoka.

Kwa takwimu, Zitto alisema katika mwaka wa fedha wa 2018/209, ongezeko la kiwango cha ukwepaji kodi umefikia kiwango cha asilimia 742; na kusema hali hiyo inatisha kwa uchumi wa nchi.

“ Inawezekana kwamba tatizo hili linatokana na udhaifu katika udhibiti lakini pia inawezekana kuna watu wanaachwa wafaidike na hali hii kwa makusudi.
“ Kwa serikali ambayo imejipambanua kwa kupambana na rushwa na kudhibiti matumizi ya fedha za umma, hali hii inatisha. Hii nchi sasa inaliwa kwa kiwango ambacho hakijawahi kuonekana. Hawa ni sawa na mchwa wanaotafuna uchumi wetu,” alisema.
Katika hatua nyingine, Zitto alieleza hofu yake kuhusu ukaguzi wa Benki Kuu ya Tanzania kuendelea kufanywa na CAG ilhali CAG aliyepita, Profesa Mussa Assad, alipendekeza kazi hiyo ifanywe na wakaguzi wa kimataifa.

Uchambuzi wa ACT Wazalendo umeeleza hofu yake kwamba fedha kutoka BoT zilienda kununua korosho kwa wakulima na hazijarudishwa bado na huku kukiwa na taarifa kuwa fedha nyingine zilitoka BoT kwenda kufanya manunuzi ya serikali nje ya nchi.

“ Kwa kuzingatia historia ya mambo yaliyowahi kutokea huko nyuma, ni wazi kwamba BoT inatakiwa kufanyiwa ukaguzi na taasisi ya kimataifa inayoheshimika. Kitendo cha serikali kutofuata ushauri wa CAG aliyepita uliotolewa kwa njia ya maandishi, kinaonyesha serikali inataka kuficha kinachoendelea BoT,” alisema.

Janeth Joel Rithe @JaneRithe
Naibu Katibu Uenezi @actwazalendo

Simu: 0713556704
Email:riterite20@gmail
Mtaarifu Zitto kuwa Serikali ya Awamu ya 5 inachapakazi kama kawaida propaganda zake hazimzui Tembo kunywa maji na mwisho wa ubunge wake ni Juni 30 2020 wananchi wa Kigoma wamemchoka na ulaghai wake!
 
295 likes
mwigulunchemba Bwana @zittokabwe , MBONA UNATESEKA Sana, Unateseka bure, Ngoja tukusaidie,
Moja ungetwambia (84.9% ya shilingi NGAPI, 91.1% ya shilingi NGAPI) na (66.5% ya Shilingi NGAPI, 64.5% ya shilingi NGAPI). Unajua FIKA percentage na absolute figures vina uzito tofauti kiuchumi.
Pili, Fedha hizo kwa asilimia hizo za awamu hizo unazolinganisha zilikwenda wapi, Kwa watu wangu hizi asilimia sio mhimu, Mhimu kwao ni KWAMBA TARAFA TATU HAZIKUWA NA HOSPITALI, SASA ZOTE ZIMEPOKEA ZAIDI YA 400M na Sasa MAPORI YAMEKUWA MIJI, MAJENGO YA HOSPITALI. NA HII NI KWA NCHI NZIMA.
Mjinga mwingine huyu. Kwa hiyo kama vituo vya afya vinajengwa kwa hiyo ni halali kuiba? Wewe baki unarusha mateke ya mwisho maana jimbo keshapewa Kitila.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua awamu zilizopita ni watu walikua wanaiibia serikali, sasa hivi ni serikali inajiibia yenyewe . halafu inabiga matrilioni. Hizi tarakimu ni kubwa kuliko ufisadi wowote tangu tupate uhuru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
¶ Mbinu ya Jiwe a.k.a Meko likely itakuwa ni ile ile kama ya 1.5trn ya kuitisha kikao kingine cha "makinikia" ili kujijitetea akiwa na serikali yake yote;

• Mawaziri wake wote
• IGP
• CDF
• Spika
• Jaji Mkuu
• Gavana - BoT
• Na mtu kati atakuwa CAG Kicheere na vijana wake

¶ SWALI KWA CAG Kicheere litakuwa lile lile "chakavu" la;

"....eti, CAG kuna ufisadi wa trillion 1.7 serikalini au hakuna....🤓🤓🤓🤓!!!??"

"....na eti wizara ya maliasili na utalii kuna ufisadi au hakuna....:oops::oops::oops:

😃😃😃!!!??"

Zito Kabwe ni mwanasiasa very technical sana....

Kwa hoja hizi, kwa hakika kabisa lazima serikali yote iamke na kukimbia mbwito mbwito kujaribu kufunika kombe ili mwana haramu spite....

Lakini this time sina hakika kama mwanaharamu huyo atapata mlango was kupitia...!!
Zitto saa hizi anatapatapa tu alijaribu kwa Accacia akashindwa sasa Accacia amepotea hapa TZ akaja na issue ya CAG mstaafu Assad naye pia amepotelea mbali akaja na issue ya mkopo wa World Bank pia amefeli. Hivyo Zitto hana cha maana katika propaganda zake yupo yupo tu lakini atawapata wasiojitambua ambao wengi wao hawana madhara yoyote kwenye Serikali na Watanzania kwa ujumla.
 
Hii taarifa kaiandika Zitto mwenyewe ila huyo naibu katibu mkuu uenezi ni kivuli tu. Swali, kwa nini uandike ujifanye imeandikwa na mwingine?

Unataka kucheza na akili za watanzania baada ya watu kugundua data zako za uongo hivyo hutaki kujitokeza Kama wewe. Una nafasi kubwa ya kurudisha Imani watanzania waliyonayo kwako, ujanja ujanja sio mzuri.
Akili ndogo na ngumu hujadiri watu while wengine wakijikita kwenye content au hoja.Ccm mna haki ya kuiba na kuteteana, sasa mtu mwenye akili Kama hii zaidi ya kazi ya kuteuliwa anaweza kufanya nini zaidi? Huyu hata ukimpa mtaji lazima afeli
 
Zitto saa hizi anatapatapa tu alijaribu kwa Accacia akashindwa sasa Accacia amepotea hapa TZ akaja na issue ya CAG mstaafu Assad naye pia amepotelea mbali akaja na issue ya mkopo wa World Bank pia amefeli. Hivyo Zitto hana cha maana katika propaganda zake yupo yupo tu lakini atawapata wasiojitambua ambao wengi wao hawana madhara yoyote kwenye Serikali na Watanzania kwa ujumla.
Chama keshauza kwa wapemba, soon wanamtupa nje
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Zitto saa hizi anatapatapa tu alijaribu kwa Accacia akashindwa sasa Accacia amepotea hapa TZ akaja na issue ya CAG mstaafu Assad naye pia amepotelea mbali akaja na issue ya mkopo wa World Bank pia amefeli. Hivyo Zitto hana cha maana katika propaganda zake yupo yupo tu lakini atawapata wasiojitambua ambao wengi wao hawana madhara yoyote kwenye Serikali na Watanzania kwa ujumla.
Mwingine huyu hapa,mr Bashite
 
Hata hueleweki unasimamia nini, Mbinguni haupo ahera pamefungwa. Alicholeta Zitto ni kutoka ripoti ya CAG na wewe unasema huamini aliyosema Zitto unaamini ripoti ya CAG!! Uwe na kumbukumbu, alichopinga Zitto siyo uwepo wa CAG Bali Kichere kuwa head of office kwa vile hana sifa za kuwapo alipowekwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu asante vile umenielewa, Mimi nitaiamini tarifa hii ya Zitto iwapo itathibitishwa na Mwingine, Kwa sababu Kwa sasa, Zitto amekuwa kama ni mtu wa jinsia moja hivi ktk Imani furani, akisimama atoe ushahidi wa Yeye peke yake hautakubalika, ushahidi wa jinsia hiyo hukubalika tu pindi watoa ushahidi watakapokuwa ni zaidi ya mmoja, ni Sawa na alivyo Mh Zitto Kwa sasa, haaminiki na hawezi kuaminiwa

Tangu alipokisaliti Chama chake kilichompa umarufu, amekuwa haeleweki na hatokuja kuaminika ni Hadi atubu,

Uteuzi wa CAG ulimsikia alichokisema mkuu? Sasa Iweje leo ripoti za CAG ambaye yeye alimzodoa huku akisema ni Magufuli wa pili, eti leo aanze kuona ni za Moto Kwa Magufuli kweli?

Mimi simwamini, Iweje leo hii Kwa ripoti hii aone inamtenganisha Magufuli na CAG?

Mwamini wewe mkuu
 
Chama Cha Mapinduzi hakina ubunifu wa kuleta viongozi bora ni dalili tosha kuwa kimeishiwa
Tatizo na upinzani wa bongo hauna umoja. Maslahi binafsi yamewekwa mbele sana. Hadi sasa sijaona umuhimu wa kuwa na utiriri wa vyama vya upinzani.
 
Zitto aibua mazito ripoti ya CAG

• Matrilioni yatumika ‘juu kwa juu’
• Serikali hoi kwa madeni
• Aifananisha na mchana
• Ahofia ‘EPA’ nyingine BoT

SERIKALI ya Tanzania imevunja Katiba kwa kutumia kiasi cha shilingi trilioni 1.7 bila ya kupitia Mfuko Mkuu ambao hukaguliwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amewaambia waandishi wa habari jana.

Katika mkutano na waandishi wa habari alioufanya jijini Dar es Salaam jana kuhusu uchambuzi wa chama chake kwenye Ripoti ya CAG ya mwaka 2018/2019, iliyowasilishwa bungeni wiki iliyopita, Zitto alisema jambo hilo ni baya kwa sababu linaruhusu fedha za Watanzania kutumika pasipo kukaguliwa.

Alisema kwa kutambua umuhimu wa kulinda fedha za umma, Katiba iliweka ofisi ya CAG iwe inakagua mapato na matumizi yote ya serikali lakini uchambuzi wao umebaini matumizi ya shilingi trilioni 1.7 ambayo hayajakaguliwa na ofisi hiyo.
“Katika mwaka wa fedha wa 2018/2019, serikali ilitumia shilingi trilioni 1.7 bila kwanza kupitia kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali. Baadhi ya fedha hizi zinatokana na mikopo kutoka nje.
“Hizi shilingi trilioni 1.7 zinazotokana na mikopo kutoka nje zimelipwa hukohuko; kwa mfano kununua ndege za ATCL na zinaweza pia kuwa zimetumika kuwekwa kwenye akaunti za watu binafsi huko nje. Utaratibu huu ni kichaka cha kukwepa kukaguliwa na CAG ili kufanya ubadhirifu,” alisema Zitto.

Zitto ambaye kitaaluma ni mchumi na amewahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (PAC) kwa takribani miaka minane, alifanya uchambuzi wake kwa kuangalia ripoti hiyo yam waka huu lakini akaangalia kwa ujumla rekodi ya serikali tangu kuingia madarakani kwa Rais John Magufuli.

Uchambuzi wa ACT Wazalendo uliangazia maeneo makubwa kumi ambayo uchambuzi umeonyesha serikali ndiyo chanzo cha hali ngumu ya uchumi –maarufu kwa jina la “vyuma kukaza” kwa sababu ya kufanya mambo yanayochangia hali hii.
Kwa mfano, Zitto aliwaambia waandishi wa habari kwamba kiwango cha serikali kudaiwa na wazabuni, kulipa deni kubwa la taifa na kukopa kupita kiasi ni mambo ambayo yamesababisha kunyausha uchumi wa Tanzania.

Akizungumza kwa takwimu, mbunge huyo wa Kigoma Mjini, alisema katika miaka mitatu ya kwanza ya utawala wa Rais Magufuli, wastani wa kiwango cha kutofikia lengo la makusanyo kilikuwa ni asilimia 16.

Alisema Deni la Taifa sasa limefikia kiasi cha shilingi trilioni 53 na mzigo wa kulihudumia umekuwa mkubwa kwa sababu sasa zinahitajika shilingi trilioni 10 kulihudumia kulinganisha na shilingi trilioni 6.3 wakati anaingia madarakani.

Kiwango hicho, mujibu wa Zitto, kinamaanisha kwamba sasa zaidi ya nusu ya makusanyo yote ya ndani ya Mamlaka ta Mapato Tanzania (TRA) yanatumika kwenye kulipia deni hilo pekee.

Uchambuzi wa ACT Wazalendo uliotangazwa na Zitto jana umeonyesha pia namna wafanyabiashara wanavyokwepa kodi kupitia bandari ya Dar es Salaam; ambapo bidhaa zenye thamani ya shilingi bilioni 312 zilidaiwa kupitishwa bandarini kama zinakwenda nje ya nchi lakini hakuna ushahidi kwamba kweli ziliondoka.

Kwa takwimu, Zitto alisema katika mwaka wa fedha wa 2018/209, ongezeko la kiwango cha ukwepaji kodi umefikia kiwango cha asilimia 742; na kusema hali hiyo inatisha kwa uchumi wa nchi.

“ Inawezekana kwamba tatizo hili linatokana na udhaifu katika udhibiti lakini pia inawezekana kuna watu wanaachwa wafaidike na hali hii kwa makusudi.
“ Kwa serikali ambayo imejipambanua kwa kupambana na rushwa na kudhibiti matumizi ya fedha za umma, hali hii inatisha. Hii nchi sasa inaliwa kwa kiwango ambacho hakijawahi kuonekana. Hawa ni sawa na mchwa wanaotafuna uchumi wetu,” alisema.
Katika hatua nyingine, Zitto alieleza hofu yake kuhusu ukaguzi wa Benki Kuu ya Tanzania kuendelea kufanywa na CAG ilhali CAG aliyepita, Profesa Mussa Assad, alipendekeza kazi hiyo ifanywe na wakaguzi wa kimataifa.

Uchambuzi wa ACT Wazalendo umeeleza hofu yake kwamba fedha kutoka BoT zilienda kununua korosho kwa wakulima na hazijarudishwa bado na huku kukiwa na taarifa kuwa fedha nyingine zilitoka BoT kwenda kufanya manunuzi ya serikali nje ya nchi.

“ Kwa kuzingatia historia ya mambo yaliyowahi kutokea huko nyuma, ni wazi kwamba BoT inatakiwa kufanyiwa ukaguzi na taasisi ya kimataifa inayoheshimika. Kitendo cha serikali kutofuata ushauri wa CAG aliyepita uliotolewa kwa njia ya maandishi, kinaonyesha serikali inataka kuficha kinachoendelea BoT,” alisema.

Janeth Joel Rithe @JaneRithe
Naibu Katibu Uenezi @actwazalendo

Simu: 0713556704
Email:riterite20@gmail
Well
 
Atukuzwe zwazwa wa uchumi, mtafuta kiki ya kisiasa.

Ripoti ya CAG imewasilishwa ikisubiri kujadiliwa na bunge. Pamoja na hilo, Rais ameagiza wahusika waanze kuchukua hatua. Zitto kama Mbunge, angefanya subira ndipo atoke hadharani.

Anajiaibisha na kudharilisha taaluma yake.
 
Back
Top Bottom