Mazito ripoti ya CAG - Janeth Rithe: Matrilioni yatumika ‘juu kwa juu’... Serikali hoi kwa madeni! Ahofia ‘EPA’ nyingine BoT

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,551
2,000
Zitto aibua mazito ripoti ya CAG

• Matrilioni yatumika ‘juu kwa juu’
• Serikali hoi kwa madeni
• Aifananisha na mchana
• Ahofia ‘EPA’ nyingine BoT

SERIKALI ya Tanzania imevunja Katiba kwa kutumia kiasi cha shilingi trilioni 1.7 bila ya kupitia Mfuko Mkuu ambao hukaguliwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amewaambia waandishi wa habari jana.

Katika mkutano na waandishi wa habari alioufanya jijini Dar es Salaam jana kuhusu uchambuzi wa chama chake kwenye Ripoti ya CAG ya mwaka 2018/2019, iliyowasilishwa bungeni wiki iliyopita, Zitto alisema jambo hilo ni baya kwa sababu linaruhusu fedha za Watanzania kutumika pasipo kukaguliwa.

Alisema kwa kutambua umuhimu wa kulinda fedha za umma, Katiba iliweka ofisi ya CAG iwe inakagua mapato na matumizi yote ya serikali lakini uchambuzi wao umebaini matumizi ya shilingi trilioni 1.7 ambayo hayajakaguliwa na ofisi hiyo.
“Katika mwaka wa fedha wa 2018/2019, serikali ilitumia shilingi trilioni 1.7 bila kwanza kupitia kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali. Baadhi ya fedha hizi zinatokana na mikopo kutoka nje.
“Hizi shilingi trilioni 1.7 zinazotokana na mikopo kutoka nje zimelipwa hukohuko; kwa mfano kununua ndege za ATCL na zinaweza pia kuwa zimetumika kuwekwa kwenye akaunti za watu binafsi huko nje. Utaratibu huu ni kichaka cha kukwepa kukaguliwa na CAG ili kufanya ubadhirifu,” alisema Zitto.

Zitto ambaye kitaaluma ni mchumi na amewahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (PAC) kwa takribani miaka minane, alifanya uchambuzi wake kwa kuangalia ripoti hiyo yam waka huu lakini akaangalia kwa ujumla rekodi ya serikali tangu kuingia madarakani kwa Rais John Magufuli.

Uchambuzi wa ACT Wazalendo uliangazia maeneo makubwa kumi ambayo uchambuzi umeonyesha serikali ndiyo chanzo cha hali ngumu ya uchumi –maarufu kwa jina la “vyuma kukaza” kwa sababu ya kufanya mambo yanayochangia hali hii.
Kwa mfano, Zitto aliwaambia waandishi wa habari kwamba kiwango cha serikali kudaiwa na wazabuni, kulipa deni kubwa la taifa na kukopa kupita kiasi ni mambo ambayo yamesababisha kunyausha uchumi wa Tanzania.

Akizungumza kwa takwimu, mbunge huyo wa Kigoma Mjini, alisema katika miaka mitatu ya kwanza ya utawala wa Rais Magufuli, wastani wa kiwango cha kutofikia lengo la makusanyo kilikuwa ni asilimia 16.

Alisema Deni la Taifa sasa limefikia kiasi cha shilingi trilioni 53 na mzigo wa kulihudumia umekuwa mkubwa kwa sababu sasa zinahitajika shilingi trilioni 10 kulihudumia kulinganisha na shilingi trilioni 6.3 wakati anaingia madarakani.

Kiwango hicho, mujibu wa Zitto, kinamaanisha kwamba sasa zaidi ya nusu ya makusanyo yote ya ndani ya Mamlaka ta Mapato Tanzania (TRA) yanatumika kwenye kulipia deni hilo pekee.

Uchambuzi wa ACT Wazalendo uliotangazwa na Zitto jana umeonyesha pia namna wafanyabiashara wanavyokwepa kodi kupitia bandari ya Dar es Salaam; ambapo bidhaa zenye thamani ya shilingi bilioni 312 zilidaiwa kupitishwa bandarini kama zinakwenda nje ya nchi lakini hakuna ushahidi kwamba kweli ziliondoka.

Kwa takwimu, Zitto alisema katika mwaka wa fedha wa 2018/209, ongezeko la kiwango cha ukwepaji kodi umefikia kiwango cha asilimia 742; na kusema hali hiyo inatisha kwa uchumi wa nchi.

“ Inawezekana kwamba tatizo hili linatokana na udhaifu katika udhibiti lakini pia inawezekana kuna watu wanaachwa wafaidike na hali hii kwa makusudi.
“ Kwa serikali ambayo imejipambanua kwa kupambana na rushwa na kudhibiti matumizi ya fedha za umma, hali hii inatisha. Hii nchi sasa inaliwa kwa kiwango ambacho hakijawahi kuonekana. Hawa ni sawa na mchwa wanaotafuna uchumi wetu,” alisema.
Katika hatua nyingine, Zitto alieleza hofu yake kuhusu ukaguzi wa Benki Kuu ya Tanzania kuendelea kufanywa na CAG ilhali CAG aliyepita, Profesa Mussa Assad, alipendekeza kazi hiyo ifanywe na wakaguzi wa kimataifa.

Uchambuzi wa ACT Wazalendo umeeleza hofu yake kwamba fedha kutoka BoT zilienda kununua korosho kwa wakulima na hazijarudishwa bado na huku kukiwa na taarifa kuwa fedha nyingine zilitoka BoT kwenda kufanya manunuzi ya serikali nje ya nchi.

“ Kwa kuzingatia historia ya mambo yaliyowahi kutokea huko nyuma, ni wazi kwamba BoT inatakiwa kufanyiwa ukaguzi na taasisi ya kimataifa inayoheshimika. Kitendo cha serikali kutofuata ushauri wa CAG aliyepita uliotolewa kwa njia ya maandishi, kinaonyesha serikali inataka kuficha kinachoendelea BoT,” alisema.

Janeth Joel Rithe @JaneRithe
Naibu Katibu Uenezi @actwazalendo

Simu: 0713556704
Email:riterite20@gmail
 

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
1,668
2,000
Hii taarifa kaiandika Zitto mwenyewe ila huyo naibu katibu mkuu uenezi ni kivuli tu. Swali, kwa nini uandike ujifanye imeandikwa na mwingine?

Unataka kucheza na akili za watanzania baada ya watu kugundua data zako za uongo hivyo hutaki kujitokeza Kama wewe. Una nafasi kubwa ya kurudisha Imani watanzania waliyonayo kwako, ujanja ujanja sio mzuri.
 

Capt Tamar

JF-Expert Member
Dec 15, 2011
10,667
2,000
Hii taarifa kaiandika Zitto mwenyewe ila huyo naibu katibu mkuu uenezi ni kivuli tu. Swali, kwa nini uandike ujifanye imeandikwa na mwingine?

Unataka kucheza na akili za watanzania baada ya watu kugundua data zako za uongo hivyo hutaki kujitokeza Kama wewe. Una nafasi kubwa ya kurudisha Imani watanzania waliyonayo kwako, ujanja ujanja sio mzuri.
Ni kweli au si kweli?hilo ndilo la msingi

Sent using Jamii Forums mobile app
 

HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
7,125
2,000
Hii taarifa kaiandika Zitto mwenyewe ila huyo naibu katibu mkuu uenezi ni kivuli tu. Swali, kwa nini uandike ujifanye imeandikwa na mwingine?

Unataka kucheza na akili za watanzania baada ya watu kugundua data zako za uongo hivyo hutaki kujitokeza Kama wewe. Una nafasi kubwa ya kurudisha Imani watanzania waliyonayo kwako, ujanja ujanja sio mzuri.
Binafsi nimeshindwa kuelewa kwanini amemtumia huyo Bidada badala ya kusimama yeye kama yeye!!!
 

Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,942
2,000
Utapeli huu ni zaidi ya corona.Jiwe anapiga mipunga hatari.....trn 1.5+trn 1.7=Huyu jamaa amevunja record ya dunia kwa upigaji tena peke yake huku akitoa kafara za kisanii kwa asiowapenda.
Yafaa apewe tuzo ya kuitia nchi hasara ndie aongozae tangu akiwa waziri kuanzia meli ya samaki,mv kigamboni,kituo cha mafuta mwanza,barabara ya bagamoyo nk.Kila agusacho ni hasara kwa taifa tena kubwa tu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom