hotuba ya rais siku ya kuchaguliwa dodoma namnukuu
ndugu zanguni napenda uwaambia na kuwaonya wale woote walio mstari wambele kulitenganisha taifa hili kwa njia moja ama nyingine hakika ntadili nao...nawaambia kweli waulizeni waliojaribu wako wapi sasa..nasema hili nikiwatahadharisha ndugu zangu kama kitu nikisema no hata uende mahakamani,,uende sijui haki za binadamu itabaki no tu..usijaribu kutafuta umaarufu kwenye seriakli yangu ukaja kujutia milele namnkuu.....waliona rekodi wamsome vizuri mh sana...dk wetu naona kaamua kuanza na maprof...
Mungu amlaze pema peponi
Hii kauli inaniumiza sana. Maneno haya hayakupaswa kusemwa na Rais wa nchi inayoendeshwa kwa misingi ya democrasia na sheria. Maana ilivyokaa ni dhahiri kwamba miaka hii mitano itakuwa ni ya kuua kila atakayejaribu kupinga au kukosoa utawala wake. Lakini Mungu anajua, maana hakuna muuaji hata mmoja ambaye hatakufa au akifa atazikwa angani. Their days are underway! Sina ushahidi wowote kwamba serikali imeshiriki katika kifo cha prof Jwani, but kama ni kweli kuna viongozi wa serikali ambao wanawaua wenzao ili kujipatia ulaji zaidi, naamini Mungu hatawaacha.
Alikuwepo Mfalme Nebukadneza aliyejiona yupo juu ya kila kitu, aliwategemea waganga na wachawi wamtabirie uelekeo wa uongozi wake na ndoto zake, kama CCM na Kikwete wanavyomtegemea Sheik Yahya, lakini mwisho wa siku alikula nyasi na kukaa porini na kunyeshewa na mvua kwa vipindi saba. Kila mtu atalipwa sawasawa na matendo yake. Nyie tuueni tu, lakini siku ya siku tutakuwa wote kaburini na tutaoza sawasawa kati ya aliyeua na kuuawa.
Laiti binadamu angekuwa anatambua kinachokuja mbele yake hata dk moja ya baadaye, angejitahidi kila wakati kutenda mema na kuwapenda na kuwalinda wenzake. Lakini kwa kuwa hajui, matokeo yake yanakuwa ndo kama hayo. Unaua tu, wewe unajua utaishi hadi lini? Inatia uchungu sana. Ndiyo maana kwenye signature yangu nasema binadamu ni kiumbe mjinga kuwashinda viumbe wote waliowahi kuishi duniani milele ne milele. Wakati wanyama wengine wanaofanana huungana kujilinda na mnyama tofauti na wao, binadamu wanauana wao kwa wao. wanatengeneza silaha nzitonzito kwa ajili ya kuulia binadamu wenzao. Ni kiumbe wa ajabu kabisa binadamu.
Lakini nawaambieni watanzania wenzangu Mungu wetu ni mwaminifu, kama hii kazi ya kumwaga damu zisizo na hatia inafanywa na CCM (ninasema kama inafanywa na CCM), basi miaka mitano hii haitaisha. Najua hamtaniamini kwa kuwa mnamwamini zaidi sheik Yahya, lakini mtaamini yatakapotokea. Najua mtaitafuta hii post hapo yatakapokuwa yamejiri.