Mazishi ya Maalim Seif nilisikia mambo 3 muhimu Ibada, Madeni na Msamaha, Wakristo wanajikita kwenye Wasifu na Mashada

UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
12,876
2,000
Kwani wewe unayojua yote ushawahi kuyapitia?

Unapomuamkia Baba yako ushawahi kupitia hali ya kuwa Baba yako na kujua kwamba yupo kweli na si hologram tu?

Unapojibizana na mimi hapa ushawahi kuwa mimi na kujua nipo na si mfumo wa Artificial Intelligence wa computer unakujibu?
Nimeuliza umejuaje? hilo ndio swali langu la msingi nimetaka kujua umejuaje.
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,352
2,000
Nimeuliza umejuaje? hilo ndio swali langu la msingi nimetaka kujua umejuaje.
Nimejua kwa mantiki ya kisayansi.

Wewe una ushahidi gani wa kimantiki kwamba mtu akifa anaweza kuelewa kinachoendelea?
 
Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
12,481
2,000
Akina nani
Kuna watu wanadai ukifa na lako limeisha?? Kuna haja ya kutoa elimu KWA wenzetu hawa. Huenda tunawalaumu bure na kuwasimanga chini KWA chini ila kiukweli kuna vitu vingi mno hawavijui
 
chokodari

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
765
1,000
Inawezekana ikawa labda sababu waislamu ni wengi na ndio maana unaona waislamu wengi ni masikini hasa ukizingatia siku zote matajiri huwa ni wachache.
[/QUOTE
Wazo lako tu waislam wengi ni magomen, temeke na kinchi ni pwani tu
 
UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
12,876
2,000
Nimejua kwa mantiki ya kisayansi.

Wewe una ushahidi gani wa kimantiki kwamba mtu akifa anaweza kuelewa kinachoendelea?
Mimi sijasema chochote, ila nataka kujua tu kutoka kwako hebu nielezee ni kwa vp mtu akifa anakuwa haelewi kinachoendelea?
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,352
2,000
Mimi sijasema chochote, ila nataka kujua tu kutoka kwako hebu nielezee ni kwa vp mtu akifa anakuwa haelewi kinachoendelea?
Kwa sababu uelewa unahitai ubongo na moyo vifanye kazi. Mtu akifa ubongo na moyo havifanyi kazi.

Hivyo, hawezi kuelewa kinachoendelea.

Wewe una ushahidi kwamba mtu anaweza kuelewa kinachoendelea bila ubongo na moyo kufanya kazi?
 
UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
12,876
2,000
Kwa sababu uelewa unahitai ubongo na moyo vifanye kazi. Mtu akifa ubongo na moyo havifanyi kazi.

Hivyo, hawezi kuelewa kinachoendelea.

Wewe una ushahidi kwamba mtu anaweza kuelewa kinachoendelea bila ubongo na moyo kufanya kazi?
Kufa ni nini?
 
sysafiri

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
1,038
2,000
Kama hakulipa madeni au kuomba msamaha wakati yuko hai,hata angelipa nani madeni yake au mtu angeomba msamaha kwa ajili yake,mbele za Mungu haisadii! Ndiyo maana kadiri inavyowezekana omba msamaha kila siku kwa sababu hujui siku wala saaa!
 
GIRITA

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
2,981
2,000
Dini zinagawanya watu tu.

Wewe hapo pia umetunyanyapaa tusio Waislamu kwa kusema tumemshambulia.

Mimi si Muislamu na sijamshambulia mtu.

Tafadhali kuwa specific.

Ama kama unataka nianze kushambulia naweza.
ukweli ni kwamba wasio waislamu ndio wamemshambulia mwenzao......sasa kama huku mshambulia vipi unaanza kujitoa wakati sijakutaja kama mshambulizi?
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,352
2,000
ukweli ni kwamba wasio waislamu ndio wamemshambulia mwenzao......sasa kama huku mshambulia vipi unaanza kujitoa wakati sijakutaja kama mshambulizi?

That is simplistic collectivization in a world that needs specificity and nuance.

Wasio waislamu ni wengi. Hata mimi si Muislamu.

Kama John kamshambulia, sema John kamshambulia. Usiseme wasio Waislamu wamemshambulia. Na mimi sijamshambulia Maalim.

Ukisema wasio Waislamu wamemshambulia, unatulundika wengine tusio Waislamu ambao hatujamshambulia.

Tumia mantiki kidogo tu ku make sense usisababishe rabsha zisizo na sababu.

Mimi nikisema Waislamu ni magaidi kwa sababu kuna Waislamu magaidi utaona sawa?
 
omtiti

JF-Expert Member
Jun 19, 2019
870
1,000
Ukifa mambo yameisha hakuna kutakiana heri wala kumuombea msamaha marehemu bwashehe..

Mbona mambo madogo yanakupiga knockouts bwashee au ndio umebakia na akili za kumsifia mjomba tu
Kwahiyo wasifu na ukaribu na late ndio sawa?
 
kindigiwa

Member
Apr 5, 2020
82
150
Imani ya waislam ina wataka wapate mali kwa njia halali ( means should justfy the ends)japo wapo waislam walio amua kuchuma mali kwa njia za haramu( ends justfy the means) kutokana na hilo ndipo unapo ona wengi wao wame ridhika na wakipatacho!
 
Ralph Tyler

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
2,514
2,000
Ukiacha mambo mengine ya itikadi, nadharia na falsafa ambazo nabishanabishana na waislamu, NAKUBALIANA nao kabisa katika mambo mawili kwamba wanayatenda vizuri sana, na kama siyo vizingiti vya kiimani, haya yanapaswa kuigwa:
Utaratibu na miongozo yao ya:
  1. Ndoa
  2. Mazishi
 
Vp ibada zao au utaratibu wao wa ibada?
 
Ralph Tyler

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
2,514
2,000
Vp ibada zao au utaratibu wao wa ibada?
Huko sijawahi kuingia kwa hiyo sina maoni yoyote. Lakini nafahamu kuwa kuna mambo katika itikadi, nadharia na falsafa zao ambayo tunapishana kabisa. Hata hivyo ni ndugu zetu jirani zetu tunaishi wote mitaani humu tukiheshimiana katika tofauti hizo, kila mmoja akiamini kuwa ndiye yuko sahihi mbele za Mungu. Maadam hakuna miongoni mwetu atakayemhukumu mwenzie siku ya kiama, bado hapajaharibika neno.
 
AGITATOR

JF-Expert Member
Apr 7, 2019
1,972
2,000
Nilifuatilia kwa karibu shughuli za mazishi ya maalim Seif kuanzia msikitini pale Upanga hadi mazishi kule Mtambwe Pemba kupitia luninga ya Channel ten.

Kitu kikubwa nilichojifunza waislamu kwenye mazishi wanamjali zaidi marehemu kuliko wao wanaobaki.

Kwa mfano pale msikitini Upanga swala haikuchukua zaidi ya robo saa ( Ibada) kisha mwakilishi wa familia akatangaza kama kuna mtu anamdai maalim Seif basi deni hilo linahamishwa kutoka kwa marehemu kwenda kwa mwanafamilia ambaye alitambulishwa kwa wote (madeni) na mwisho mwakilishi wa familia akamuombea msamaha marehemu kwa wale wote wenye kinyongo naye ( msamaha)

Hii ni tofauti na misiba ya kikristo ambayo kama kule Kenya hutumika kisiasa na hapa nyumbani ratiba ya mazishi hutawaliwa na salamu, wasifu na mashada ya maua.

Kwenye salamu kila mtu hujielezea zaidi yeye binafsi alivyokuwa karibu na marehemu badala ya kutumia muda huo kumtakia heri mwendazake huko aendako.

Katika hili waislamu nimewakubali.

Maendeleo hayana vyama.
Mwanadamu amepewa kuishi mara moja, baada ya kufa hukumu. Hata kufanyike sarakasi za aina gani, haziwezi badili kilichomo kwenye file lako kule uendako. Mengine ni kufarijiana tu.
 
luangalila

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
3,778
2,000
Nilifuatilia kwa karibu shughuli za mazishi ya maalim Seif kuanzia msikitini pale Upanga hadi mazishi kule Mtambwe Pemba kupitia luninga ya Channel ten.

Kitu kikubwa nilichojifunza waislamu kwenye mazishi wanamjali zaidi marehemu kuliko wao wanaobaki.

Kwa mfano pale msikitini Upanga swala haikuchukua zaidi ya robo saa ( Ibada) kisha mwakilishi wa familia akatangaza kama kuna mtu anamdai maalim Seif basi deni hilo linahamishwa kutoka kwa marehemu kwenda kwa mwanafamilia ambaye alitambulishwa kwa wote (madeni) na mwisho mwakilishi wa familia akamuombea msamaha marehemu kwa wale wote wenye kinyongo naye ( msamaha)

Hii ni tofauti na misiba ya kikristo ambayo kama kule Kenya hutumika kisiasa na hapa nyumbani ratiba ya mazishi hutawaliwa na salamu, wasifu na mashada ya maua.

Kwenye salamu kila mtu hujielezea zaidi yeye binafsi alivyokuwa karibu na marehemu badala ya kutumia muda huo kumtakia heri mwendazake huko aendako.

Katika hili waislamu nimewakubali.

Maendeleo hayana vyama.
Moja kati ya UZI wa kipuuzi mwaka 2021
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom