johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 84,035
- 142,137
Nilifuatilia kwa karibu shughuli za mazishi ya maalim Seif kuanzia msikitini pale Upanga hadi mazishi kule Mtambwe Pemba kupitia luninga ya Channel ten.
Kitu kikubwa nilichojifunza waislamu kwenye mazishi wanamjali zaidi marehemu kuliko wao wanaobaki.
Kwa mfano pale msikitini Upanga swala haikuchukua zaidi ya robo saa ( Ibada) kisha mwakilishi wa familia akatangaza kama kuna mtu anamdai maalim Seif basi deni hilo linahamishwa kutoka kwa marehemu kwenda kwa mwanafamilia ambaye alitambulishwa kwa wote (madeni) na mwisho mwakilishi wa familia akamuombea msamaha marehemu kwa wale wote wenye kinyongo naye ( msamaha)
Hii ni tofauti na misiba ya kikristo ambayo kama kule Kenya hutumika kisiasa na hapa nyumbani ratiba ya mazishi hutawaliwa na salamu, wasifu na mashada ya maua.
Kwenye salamu kila mtu hujielezea zaidi yeye binafsi alivyokuwa karibu na marehemu badala ya kutumia muda huo kumtakia heri mwendazake huko aendako.
Katika hili waislamu nimewakubali.
Maendeleo hayana vyama.