Mazingaombwe (Jugglery) ni Sayansi au Uchawi?

Mwiyuzi

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
849
500
Enzi zile nasoma shule ya msingi kulikuwa na vijana waliokuwa wakija shule kwa ajili ya mazingombwe. Walikuwa wakifika shuleni mara kwa mara kwa ajili ya maonyesho hayo.

Walikuwa wakipewa kibali na mwl mkuu/mwl wa michezo pamoja na kupewa darasa la kufanyia mazingambwe yao kama ukumbi. Pia kulikuwa kiingilio ili kuweza kuingia ukumbini (darasani) kwa ajili ya kuangalia mazingaombwe hayo.

Ndani ya ukumbi, wanaofanyia mazingaombwe walikuwa wakifanya vituko mbalimbali ambavyo baada ya kuvikumbuka nikaamua kuleta uzi huu kwenye hili jamvi la chitchat ili tukumbushane. Nakumbuka:

• Kuna siku walimuita mvulana mmoja wakampasua tumbo hadi utumbo ukawa unaonekana kwa nje, baadae wakaongea maneno fulani yule mtu akazinduka na hakuwa na kovu lolote lile
• Siku nyingine wilimuita mtoto aliyekuwa mdogo kuliko wote darasani wakamuweka ndani ya gunia lililokuwa tupu mara baada ya dakika kadhaa... pipi na biskut zikajaa kwenye lile gunia...
Naombeni tukumbushane vituko vyilivyokuwa vikifanyika kwenye mazingaombwe

Vilevile nimejiuliza maswali yafuatayo:
1. Nini kilikuwa kinasababisha tuone mtu aliyepasuliwa tumbo hana hata kovu eneo lililopasuliwa?
2. Mazingaombwe bado yanafanyika mashuleni mpaka sasa?
3. Je Wizara ya Elimu ilikuwa inakuridhia mazingaombwe kufanyika mashuleni?
Mtazamo wako ukoje katika haya?

Amyner

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
2,398
2,000
Nilishawahi kuangalia show moja inaitwa "The secrets of the magicians!" inaonesha how magicians perform their tricks and at times fool u! Inshort mazingaombwe ni maujanja flani huwa yanafanyika without the audience having a slightest idea o clue of what is taking place behind the scene!

TONGONI

JF-Expert Member
Feb 18, 2011
1,038
1,500
Nilishawahi kuangalia show moja inaitwa "The secrets of the magicians!" inaonesha how magicians perform their tricks and at times fool u! Inshort mazingaombwe ni maujanja flani huwa yanafanyika without the audience having a slightest idea o clue of what is taking place behind the scene!
Na hayo maujanja flani ndio ufundi wenyewe,ndio maana sio kila mtu anaweza.kuna watu kama David Copperfield,Lance Burton..wanajulikana kimataifa kwa haya maujanja flani.

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
59,015
2,000
Kuna siku nilienda kufanya mazingaombwe kule Sumbawanga. Nilikuwa na uwezo wa kumgeuza binadamu kuwa panya kisha nikamrudisha tena na kuwa binadamu.
Basi nikaenda sokoni nikawakusanya watu, nikamgeuza jamaa kuwa panya.
Kulikuwa na mama mmoja pembeni akajigeuza na kuwa paka, kisha akammeza yule panya, na baada ya hapo akarudi kwenye umbo lake la ubinadamu.
Nilijuta kuzaliwa, sitaki kukuelezea kilichotokea baada ya hapo.

tindikalikali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,858
1,195

mh ishu ni kwamba wanawezaje kumgeuza binadamu kuwa panya?

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
6,799
2,000
Kuna siku nilienda kufanya mazingaombwe kule Sumbawanga. Nilikuwa na uwezo wa kumgeuza binadamu kuwa panya kisha nikamrudisha tena na kuwa binadamu.

Basi nikaenda sokoni nikawakusanya watu, nikamgeuza jamaa kuwa panya.

Kulikuwa na mama mmoja pembeni akajigeuza na kuwa paka, kisha akammeza yule panya, na baada ya hapo akarudi kwenye umbo lake la ubinadamu.

Nilijuta kuzaliwa, sitaki kukuelezea kilichotokea baada ya hapo.

hahah hahhahahha hhhahahhahahahahah hahhahahahhahahha

Slave

JF-Expert Member
Dec 6, 2010
5,316
2,000
Kuna siku nilienda kufanya mazingaombwe kule Sumbawanga. Nilikuwa na uwezo wa kumgeuza binadamu kuwa panya kisha nikamrudisha tena na kuwa binadamu.

Basi nikaenda sokoni nikawakusanya watu, nikamgeuza jamaa kuwa panya.

Kulikuwa na mama mmoja pembeni akajigeuza na kuwa paka, kisha akammeza yule panya, na baada ya hapo akarudi kwenye umbo lake la ubinadamu.

Nilijuta kuzaliwa, sitaki kukuelezea kilichotokea baada ya hapo.
hahaha.bujibuji naona uliogopa ile mbaya maana ulijua sasa zamu yako.loh ningekuwa mimi ningemuachia vumbi tu.yaani kwenye kona angekuwa anasikia fyuuuu!! Tyaaaaa!! Shaaaa!! Yaani kisigino na kisogo.acha kabisa.

MWENDAKULIMA

JF-Expert Member
Jul 17, 2009
953
195
Kuna siku nilienda kufanya mazingaombwe kule Sumbawanga. Nilikuwa na uwezo wa kumgeuza binadamu kuwa panya kisha nikamrudisha tena na kuwa binadamu.
Basi nikaenda sokoni nikawakusanya watu, nikamgeuza jamaa kuwa panya.
Kulikuwa na mama mmoja pembeni akajigeuza na kuwa paka, kisha akammeza yule panya, na baada ya hapo akarudi kwenye umbo lake la ubinadamu.
Nilijuta kuzaliwa, sitaki kukuelezea kilichotokea baada ya hapo.

Halijawahi kutokea hilo tukio,acha usanii.

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
27,135
2,000
Mazingaombwe ya kukusanya Shilingi mia mia kwa wanafunzi na wapita njia hayana dili, utaishia kuuza sura na mwisho wa siku utakufa maskini tu ndani ya nchi kama hii.
Kwanini usijigeuze upepo ukaingia mahali kama BOT na kukomba mabilioni yanayosubiri dili feki za EPA usepe nayo??!!
Hayo ndio mazingaombwe/uchawi wenye tija.
Tuache kufikiria mambo yasiyo na tija kwetu,
Ndio maana tuna wataalamu wengi tu wa kusomea na wenye vipaji lakini hatuwaendelezi!!

Baba V

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
19,493
2,000
Nadhani serikali yetu inayajua vizuri sana mambo hayo, kama vle jairo anapoharibu anachuniwa kiaina na wa TZ hamfanyi chochote hayo ndo mazingaombwe

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,620
2,000
Eti nasikia wakati hawa jamaa wanafanya hayo maujanja ukiwa umevaa kandambili halafu umegeuza, basi utaona huo usanii wao live bila chenga!

tindikalikali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,858
1,195
Wakuu kipindi nipo primary nimeshuhudia sana hiki kinachoitwa mazingaombwe. Toka kipindi hicho nimekuwa nikijiuliza maswali ambayo mpaka sasa sijapata majibu yake. Baadhi ya maswali ni haya.
1. Je kuna uhusiano wowote kati ya uchawi na mazingaombwe?
2. Kama hakuna uhusiano, je ni nguvu gani wanazotumia?(maana kuna wasioamini uwepo wa Mungu wala uchawi).
3. Je kuna mahali wanasomea haya mambo?
4. Vipi kuhusu historia yake, na yana nafasi gani katika hii dunia ya utandawazi?

Natanguliza shukrani...karibuni.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom