Ukweli kuhusu mazingaombwe....! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli kuhusu mazingaombwe....!

Discussion in 'Entertainment' started by tindikalikali, Dec 26, 2015.

 1. Mwiyuzi

  Mwiyuzi JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 861
  Likes Received: 304
  Trophy Points: 80
  Enzi zile nasoma shule ya msingi kulikuwa na vijana waliokuwa wakija shule kwa ajili ya mazingombwe. Walikuwa wakifika shuleni mara kwa mara kwa ajili ya maonyesho hayo.

  Walikuwa wakipewa kibali na mwl mkuu/mwl wa michezo pamoja na kupewa darasa la kufanyia mazingambwe yao kama ukumbi. Pia kulikuwa kiingilio ili kuweza kuingia ukumbini (darasani) kwa ajili ya kuangalia mazingaombwe hayo.

  Ndani ya ukumbi, wanaofanyia mazingaombwe walikuwa wakifanya vituko mbalimbali ambavyo baada ya kuvikumbuka nikaamua kuleta uzi huu kwenye hili jamvi la chitchat ili tukumbushane. Nakumbuka:

  • Kuna siku walimuita mvulana mmoja wakampasua tumbo hadi utumbo ukawa unaonekana kwa nje, baadae wakaongea maneno fulani yule mtu akazinduka na hakuwa na kovu lolote lile
  • Siku nyingine wilimuita mtoto aliyekuwa mdogo kuliko wote darasani wakamuweka ndani ya gunia lililokuwa tupu mara baada ya dakika kadhaa... pipi na biskut zikajaa kwenye lile gunia...
  Naombeni tukumbushane vituko vyilivyokuwa vikifanyika kwenye mazingaombwe

  Vilevile nimejiuliza maswali yafuatayo:
  1. Nini kilikuwa kinasababisha tuone mtu aliyepasuliwa tumbo hana hata kovu eneo lililopasuliwa?
  2. Mazingaombwe bado yanafanyika mashuleni mpaka sasa?
  3. Je Wizara ya Elimu ilikuwa inakuridhia mazingaombwe kufanyika mashuleni?
  Mtazamo wako ukoje katika haya?
   
Loading...