Lakini nilisikia kuwa mtu akiingia na mkaa au ndimu kwenye chumba cha maonyesho wanamsitukia na kumfukuza!
PIa ikumbukwe kuwa walikuwa enzi hizo wakija na sanduku la mbao, ambapo kwa wakati huo lilikuwa likionekana la fasheni ya kawaida tu!
Ahahhahahaah wengine walikua waongo sana ! niliwahi kuhusika na mchezo mchafu alikuja Mwanamazingaombwe simkumbuki jina , akaomba vijana watatu wajanja , nami nikala shavu ! kumbe anaenda kutufundisha uwongo wake.
Mimi alinifundisha akipuliza dawa yake nijidai sioni amenipofusha kwa dawa zake !
Mwisho wa siku nikapewa Tsh. 20
Umenikumbusha mbali mkuu! Hii ilikuwa miaka ya 1980; alikuja mwanamazingaombwe mmoja na sanduku la mbao, akiitwa Profesa Eyesso. Kabla ya mchezo kuanza, alipiga mkwara kuwa mwanafunzi yeyote aliyeingia na ndimu ukumbini atoke nje la sivyo atampofua macho. Nakumbuka vijana wawili walitoka nje kwa aibu kubwa.
mwaka jana kwenye East Africa trade fair kulikuwa na mazingaombwe ya kichwa kisicho na kiwiliwili lakini kinaongea. kilikuwa kimewekwa mezani. me nilikwenda kushuhudia lakin ile naingia tu nikaona kama kimenipiga kope kikaogopa nikatoka. dah cjui ni ufundi gani jamani?