Maxence Melo: Pole sana Tundu Lissu, Mungu akuponye!

Maxence Melo: Pole sana Tundu Lissu, Mungu akuponye!

Status
Not open for further replies.
Nakumbuka ambavyo mwaka 2008 nilipokamatwa ikidaiwa mimi ni GAIDI ulijitoa na kuja kuwa wakili wangu bila kuombwa na hata hukuniomba senti. Wakati huo hukuwa katika "active politics".

Maisha yakaenda mbele, ukawa mwanachama wa JamiiForums kwa jina halisi (verified Tundu Lissu) na kuniambia unataka kuonesha support kwa huduma tunayoitoa.

Disemba 2016 nilipokamatwa kwa madai ya kutotoa 'ushirikiano' kwa vyombo vya dola, hukuniacha ukaja hata bila kuitwa. Ulinisisitiza "Max, tumetoka mbali hata kabla sijaingia kwenye siasa, leo unanikimbia? Sikuachi uumie, nitakutetea bure na hata kufunga safari toka Dodoma kila kesi yako itakapotajwa." Tukacheka na kutiana moyo!

View attachment 583487

Ni wiki mbili zilizopita tulipopiga picha hii, hapa ulikuwa unarekebisha kalenda yako kuhakikisha tarehe ya kesi yangu unakuwepo ili kuhakikisha sizamishwi na walionipania (na nakumbuka ulithubutu kuwaambia usoni mbele zangu).

Habari ya wewe kushambuliwa kwa risasi (ni wazi waliutaka uhai wako) imeniumiza sana, imenitia simanzi kuu na kunifanya nikose la kufanya zaidi ya kupata japo dakika kadhaa kukuombea (the best I could do).

I happen to know you Tundu, nje ya siasa wanazoona walio wengi! Mungu akusaidie upone haraka na kukurejeshea afya yako hata kuyaponya majeraha yako.

Mungu wetu ni mwingi wa huruma; kama amekuepusha na kifo leo - atakuponya!

Get well soon brother...
Aameen
 
Naamini Mungu atakuponya Brother Lissu na kila mtu anayehusika na hata wale wapumbavu mitandaoni wanaomuombea mabaya Mungu utawashuhulikia mmoja baada ya mwingine ili waone UKUU wako
 
Natamani nikasome sheria (japo nina fani nyingine)...niwe kama TL. Niweze kutetea watu wasidhulimiwe, tena bure bila kuwadai malipo! Vijana wa Tz (upcoming Lawyers and Advocates) tunalo la kujifunza from TL. Pole sana brother TL! WaTz wapenda haki tuko na wewe...Mungu yuko upande wako pia. Get well soon!!!
 
Mungu akuponyeshe haraka na akukinge na wabaya wako wote ambao wanataka kuitoa roho yako mweshimiwa Lissu, roho ndio itiayo uzima mwili haufai kitu. Waliopanga kuutuo uhai wako wakamatwe na haki itendeke
 
Ni habari mbaya mno kwangu,
Nilipopata taarifa hizi moyo wangu uliumia sana, mikono yangu ililegea.
Mungu amponye Lisu sawa na wingi wa rehema zake.
Tunaelekea wapi?
Matunda ya chuki hii ni nini?

Je tusikosoane?
Tusiambiane ukweli?
Tutakomaa kisiasa lini?
Nchi yangu nchi yangu.
Mwisho wa haya ni nini?
Lisu anahatarisha nini?
Lakini kwanini wamwogope?
Mkuu umenitonesha, ngoja nifute tu machozi
 
Inauma sana inahuzunisha sana Mungu wetu ni mwingi wa huruma; kama amekuepusha na kifo leo - atakuponya! Tundu Lissu Mungu akutie nguvu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom