Maxence Melo: Pole sana Tundu Lissu, Mungu akuponye!

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
3,784
2,000


Nakumbuka ambavyo mwaka 2008 nilipokamatwa ikidaiwa mimi ni GAIDI ulijitoa na kuja kuwa wakili wangu bila kuombwa na hata hukuniomba senti. Wakati huo hukuwa katika "active politics".

Maisha yakaenda mbele, ukawa mwanachama wa JamiiForums kwa jina halisi (verified Tundu Lissu) na kuniambia unataka kuonesha support kwa huduma tunayoitoa.

Disemba 2016 nilipokamatwa kwa madai ya kutotoa 'ushirikiano' kwa vyombo vya dola, hukuniacha ukaja hata bila kuitwa. Ulinisisitiza "Max, tumetoka mbali hata kabla sijaingia kwenye siasa, leo unanikimbia? Sikuachi uumie, nitakutetea bure na hata kufunga safari toka Dodoma kila kesi yako itakapotajwa." Tukacheka na kutiana moyo!

max lissu.jpg


Ni wiki mbili zilizopita tulipopiga picha hii, hapa ulikuwa unarekebisha kalenda yako kuhakikisha tarehe ya kesi yangu unakuwepo ili kuhakikisha sizamishwi na walionipania (na nakumbuka ulithubutu kuwaambia usoni mbele zangu).

Habari ya wewe kushambuliwa kwa risasi (ni wazi waliutaka uhai wako) imeniumiza sana, imenitia simanzi kuu na kunifanya nikose la kufanya zaidi ya kupata japo dakika kadhaa kukuombea (the best I could do).

I happen to know you Tundu, nje ya siasa wanazoona walio wengi! Mungu akusaidie upone haraka na kukurejeshea afya yako hata kuyaponya majeraha yako.

Mungu wetu ni mwingi wa huruma; kama amekuepusha na kifo leo - atakuponya!

Get well soon brother...
 
Top Bottom