Maxence Melo: Pole sana Tundu Lissu, Mungu akuponye!

Maxence Melo: Pole sana Tundu Lissu, Mungu akuponye!

Status
Not open for further replies.
~~>>>Get well soon brother..... Watanzania tunakuhitaji sana kuliko hayo manyang'au!
 
Amen!!!Mungu atamponya na atawaumbua wale walotaka kuutoa uhai wake.

sent from my Infinix S2 Pro using JamiiForums mobile app
 
Ukweli ni kuwa nchi yetu kwa sasa hakuna aliye salama.Eee Mwenyezi Mungu tuepushe na balaa hili,mponye Tundu Antipas Lisu, mrejeshee afya yake awe kana kwamba hakuwahi kupigwa risasi. Naomba Mwenyenzi utusikilize waja wako na kuwaaibisha maadui wa mtetezi huyu wa waja wako wanaoonewa na wenye nguvu na kiburi cha utawala!
 
Ni habari mbaya mno kwangu,
Nilipopata taarifa hizi moyo wangu uliumia sana, mikono yangu ililegea.
Mungu amponye Lisu sawa na wingi wa rehema zake.
Tunaelekea wapi?
Matunda ya chuki hii ni nini?

Je tusikosoane?
Tusiambiane ukweli?
Tutakomaa kisiasa lini?
Nchi yangu nchi yangu.
Mwisho wa haya ni nini?
Lisu anahatarisha nini?
Lakini kwanini wamwogope?
 
Maneno mazito sana.. Get well soon Lissu..Ni nani mwenye courage ya kusema ukweli? Ni nani atatusemea Lissu? [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24]
Wenzetu hapa Kenya wanamkosoa rais wao hadharani tena redioni na vipindi vya kumkosoa waziwazi bila hofu na rais haoni tatizo..lakini kwetu wanataka kuabudiwa.
To be honest nimechukia kiasi cha kuingiwa na roho ya chuki dhidi ya watu flani
 
Ni habari mbaya mno kwangu,
Nilipopata taarifa hizi moyo wangu uliumia sana, mikono yangu ililegea.
Mungu amponye Lisu sawa na wingi wa rehema zake.
Tunaelekea wapi?
Matunda ya chuki hii ni nini?

Je tusikosoane?
Tusiambiane ukweli?
Tutakomaa kisiasa lini?
Nchi yangu nchi yangu.
Mwisho wa haya ni nini?
Lisu anahatarisha nini?
Lakini kwanini wamwogope?
Nyie ndio ambao munatafutwa mukaisadie police..... siasa zimetoka wapi hapo... kukosoa ndio nini...

Sala kwanza jamaa apone jaman... tutayajua mengine... unaconclude we km nani...... tulia tupishe vyombo vifanye kazi.. damu ya mtu haipotei

Sent from "La -Vista"
 
Mungu amponye na kumpigania, waaibuke na wafadhaike wanaotaka kuitoa roho yake!
 
Maxence Melo,
Mh. Lissu alijua hatari inayomkabili katika harakati zake za kutetea utawala wa sheria, haki na usawa ndani ya taifa hili lakini hakutetereka kimsimamo. Ni wachache ndani ya taifa hili lililogubikwa na unafiki na tamaa wanaoweza kuvaa viatu vya Mh. Lissu.

Kama alivyowahi kunena alikuwa yuko tayari kukabiliana na njama zozote zile za kumnyamazisha bila woga. Utayari na ujasiri, pamoja na baraka za Mwenyezi Mungu, vimemtia nguvu na vitaendelea kumpa nguvu katika kupigania maisha yake.

Mh. Tundu Antiphas Lissu alivyoishi kwa kuwapigania wanyonge na wanaoteseka, hivyo hivyo Mungu hawezi kumtupa. Tuzidi kumuomba Mungu wa rehema ampiganie kama alivyowapigania wanyonge na wanaoteseka maisha yake yote...bado tunamhitaji.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom