Mawaziri wanane watakiwa kung'oka...!

Mawaziri wanane watakiwa kung'oka...!

Hivi kama Mawaziri wanane wanajiuzulu hii haina maana kwamba serikali imefika kikomo? Ina maana wanane wote hawajui wanalolitenda ama ni wabadhirifu. Je wanaowasimamia wao hawana share yao katika uzembe huu?
Haya mambo yanachanganya.
Mkuu Kimbunga, kuna mtu kaiba ID yako nini? Maana siku zite Kimbunga ni mtetezi wa uchafu wa Magamba humu!!
 
Kama ile wizara ya Nundu iunganishwe na ya Magufuri uone mziki wake
 
Hii haitoshi wapelekwa mahakani, washitakiwe na mali walizo chota zirudishwe serikalini na pia naona hata Pinda awafuate manake wakati wanachota pesa alikuwa anawaona, na yeye awafuate ili iwe fundisho kwa hawa watakao baki.
 
JK na Pinda ndio waondoke otherwise ni kubadili chupa tu wakati mvinyo ni ule ule.
Kwa hali ya uchumi ulivyo hivi sasa wakiondoka hao nchi ita-collapse kwa kuitisha uchaguzi mkuu tena!
 
Kwa hapa mkuu wa Kaya hanabudi kupangulua kikosi chake na kupanga upya kwa kuzingatia maoni ya wananchi. Tena ni bora akapunguza wizara kuliko kuendelea kuongeza utitiri wa mchwa wanaotafuna fedha za umma. Huyu Malima hafai anafaa katika masuala ya ulimbwende
 
HATIMAYE mawaziri saba kati ya nane wakiwemo wanaokabiliwa na tuhuma za ubadhirifu, wamekubali kuandika barua za kujiuzulu wenyewe kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kukinusuru Chama cha Mapinduzi (CCM).
Habari za kuaminika kutoka mjini Dodoma zimesema kuwa mawazirihao, walilazimishwa kujiuzulu katika kikao cha dharura kilichokuwa chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kilichofanyika mara tu baada ya kumalizika kwa kikao chaBunge.
Taarifa zimewataja waliokubali kujiuzulu kuwa ni pamoja na Waziriwa Viwanda na Biashara, Cyril Chami;
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika;
Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu; na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.
Wengine wanaodaiwa kujiuzulu ni:
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja;
Naibu Waziri wa Afya, Lucy Nkya;
na Naibu Waziri wa Viwanda, Lazaro Nyarandu.
Hata hivyo, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, ambaye alishambuliwa vikali kwa kuitwa kinara wa ufujaji, hakuwepo katika kikao hicho kwa madai kuwa yuko nje ya nchi, anasubiriwa aungane na wenzake kuachia ngazi.
Kujiuzulu kwa mawaziri hao kumekuja baada ya kuzuka kwa mjadala mzito ndani ya Bunge kwa siku mbili mfululizo kuhusiana na tuhuma za ufujaji wa kutisha wa fedha za umma, kiasi chakusababisha kuwepo kwaazimio la kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

mbona kama maghembe wanamlinda iv coz hapa mwanga(jimboni) kjj cha kisangara alichangisha pesa za walala hoi then mpaka sasa hakuna hata plan ya hayo maji,afu naona kama makamanda wanamuachia huru sana hembu jaribuni kuwasha moto hapa coz nimeona madudu mengi
 
Kelele nyingi zimepigwa kwa muda mrefu toka kwa chama cha upinzani na wadau mbalimbali kuhusiana na ubadhirifu katika serikali,chama tawala CCM na taasisi mbalimbali za umma na serikali lakini hakuna hatua zozote zinazochuliwa na Mh.Rais JK.Hapa ndipo ninapojiuliza tatizo ni mawaziri na viongozi wa taasisi za umma na serikali au Mh.Rais mwenyewe JK na yeye ni sehemu ya tatizo lenyewe.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
january makamba apewe nishati na madini bcoz jamaa anamachungu na gharama kubwa za umeme.
 
Hata kama Mawaziri hao wakijiuzuru na bado tukaendelea na aina ya utawala tuliyo nayo kwenye ofisi kuu ya Taifa hili ni kazi bure.Haikuitaji kuwa na taaluma ya hali ya juu kuweza kujua tatizo hili chanzo chake ni nini.Chanzo ni kukosekana kwa uwajibikaji kuanzia ofisi kuu ya Taifa hili na hakika kama Watanzania tutakuwa jamii ya watu makini hili ni somo tosha kwa ajili ya namna ya kuchagua viongozi wakuu wa Taifa hili katika chaguzi zijazo.
 
Afu hv huyu mama mavifaranga hana sehem aliyo iba kweli! Hembu makamanda tafuteni muanze nae kwanza coz ni tatizo
 
:A S angry: HAITOSHI NASEMA HAITOSHI KABISA, HII IWE HATUA YA KUWEKA MAZINGIRA YA KUWAFUNGULIA MASHITAKA PAMOJA NA WATENDAJI WALIOSHIRIKIANA NAO.
 
Hili la wao kufikishwa mahakamani si suala la wananchi kusemea au kulalamika.
Naamini vyombo vya mashitaka tayari vimerahisishiwa sana mashitaka ya hawa jamaa.
Ni kuwapeleka kama kuku tu mahakamani ili kukamilisha ratiba ya KUFUNGWA KWAO!
 
january makamba apewe nishati na madini bcoz jamaa anamachungu na gharama kubwa za umeme.
 
Tatizo waliokuwepo nje nao wote mambumbumbu.. Ila kwaa sound na kupiga domo nambari one..
 
Afu hv huyu mama mavifaranga hana sehem aliyo iba kweli! Hembu makamanda tafuteni muanze nae kwanza coz ni tatizo

Tena anakera kweli,hayupo kwa ajili ya maslahi ya taifa bali chama, Ndungai Job atleast anaonyesha kukerwa pia na hao mafisadi wa mchana kweupe peee!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom