Mawaziri wanane watakiwa kung'oka...!

Mawaziri wanane watakiwa kung'oka...!

Jamani mbona mnatoa list zinazokinzana!
Ngeleja lazima awemo
 
Je kitendo cha ccm kuwawekea kikao Mawaziri waliovurunda na kuwalazimisha kujiuzulu kwa madai ya kuinusuru ccm, ni kweli kutakisalimisha chama hicho kwenye mtizamo wa jamii, chaguzi ndogo na hatimaye uchaguzi mkuu 2015?

Maoni yako tafadhali!
 
Hawa jamaa mawaziri waliolazimishwa kujiuzuru ni matajiri sana, tena wametajirika kwa muda mfupi.
Watueleze hizo mali wamepataje kwani mishahara yao si mikubwa ki hivyo.

Kama wewe Maige; yasemekana una nyumba Ghorofa umenunua Kariakoo unataka kulivunja uangushe kitu!!!

wenzangu je? tetesi ya mali za hawa watu..........?
 
Vipi? ilikuwa tetesi, niliposema ipelekwe jukwaa la udaku, nikaambiwa sasa ni "confimed", nikauliza "wewe ndiye uliyewaajiri"? nikatolewa maneno ya Munkar.

Nauliza kiko wapi?
 
january makamba apewe nishati na madini bcoz jamaa anamachungu na gharama kubwa za umeme.

Ni mnafiki tu hana uchungu wowote...Anajikosha mbele ya wananchi tu lakini yakitakikana maamuzi magumu hataweza kusimama imara kupingana na udhalimu.
 
Baada ya kujiuzulu, washitakiwe kwa kutumia madaraka yao vibaya na kuliingizia taifa hasara, na ikiwezekana wafungwe kwa muda mrefu sana gerezani. Kujiuzulu tu halafu wakaenda kutumbua mali waliyotuibia hakutoshi; ningetegemea watoa hoja waongeze kipengele hicho kwenye hoja hiyo.

Raisi naye awajibishwe kwa kushindwa kuwasimamia watu aliowapa madaraka hadi wakaliingizia taifa hasara kubwa kiwango hicho; naye ashitakiwe (ingawa najua sheria hiyo haipo).

Naunga mkono hoja %100:
 
Waziri anaweza kuomba kujiuzulu lakini Rais ndio mwenye mamlaka ya kukubali au kukataa, hakuna yeyote anaeweza ku "confirm" hilo, msidanganye watu.
 
Hii haitoshi wapelekwa mahakani, washitakiwe na mali walizo chota zirudishwe serikalini na pia naona hata Pinda awafuate manake wakati wanachota pesa alikuwa anawaona, na yeye awafuate ili iwe fundisho kwa hawa watakao baki.

Acha hizo wewe inamaana mtoto akiwa mwizi, wazazi wake nao wezi? na mashitaka ya mtoto huyo waweza kuyahamishia kwa wazazi wake? Waziri mkuu hausiki katika hilo na ndiyo maana yeye kama kiongozi mkuu wa shughuli za serikali amewaita na kuwalazimisha wajiuzuru vinginevyo wataondolewa sasa si vizuri kumtupia lawama PM labda uwe na chuki zako binafsi na kizuri zaidi huyu PM ni msafi hana tabia za udokozi na maamuzi yake huwa si ya kukurupuka uwa anafuata taratibu na sheria zilizopo!
 
Sasa ni wakati muafaka kwa JK kuunda baraza dogo la mawaziri atakalolimudu!

yeah ni sahihi kabisa maana baraza lililokuwepo alilifanya kubwa kwa kuamini ndilo litakuwa la ufanisi zaidi kumbe ulaji na uzandiki
 
(1)Wamejidhihirisha wao ni genge la wezi watupu, (2) wamejidhihirisha kuwa hawana uwezo wa kuwajibishana mpaka wapigwe mkwara na wapinzani (wanalindana) (3) wameipa chadema umaarufu mara 90
 
Kwa ninavyowajua Watanzania wamepokea kwa furaha uamuzi wa mawaziri kujiuzulu.

-Kesho utawasikia wanaanza umbea wa nani atateuliwa na Rais kuwa waziri.
-Hatutaki kukubaliana na dhana kwamba tatizo si watu, tatizo ni mfumo.
-Tumeng'ang'ania katika uwajibikaji wa watu na si Uwajibikaji wa Mfumo.
-Tutambue wazi kuwa watu wanakuja na kupita ila mfumo bora utasimama kizazi hata kizazi.
-Mfumo ndio siri ya mafanikio ya mataifa yaliyoendelea ikiwemo Marekani.

NI NAMNA GANI BASI TUTAUNDA KATIBA ITAKAYO HAKIKISHA (GUARANTEE) UWAJIBIKAJI-HII NDNIO IWE AGENDA KICHWANI MWA WATANZANIA.
 
Nitaendelea kuwa "TOMASO";Kujiuzuru kwa Waziri wa Tanzania kwa kashfa za jumla kama hizi SIDHANI KAMA INAWEZEKANA maana kuwa waziri TZ ni utajiri!

Sasa Waziri atakubali aachie dili la utajiri kwa sababu ya RIPOTI YA CAG MBAYO IPO VERY COMPREHENSIVE?NO WAY!
 
well sina uhakika sana kama hili Jambo la kujiuzulu kwa hawa Mawaziri litawezekana coz historia ya nchi hii na mfumo we2 haupo hivyo hata wakifanya madudu ya namna gani kama aliyewapa dhamana hana nia dhabiti ya kuwawajibisha ni kazi bure. sidhani kama kuna m2 atajiuzulu its virtually impoosible.
 
Waziri anaweza kuomba kujiuzulu lakini Rais ndio mwenye mamlaka ya kukubali au kukataa, hakuna yeyote anaeweza ku "confirm" hilo, msidanganye watu.

Uko sahihi,man lakini fahamu kama raisi atadiriki kuwazuia mawaziri hawa,basi ni kwamba anaendelea kuiangamiza CCM na ni dhahiri sasa chama kitakufa mikononi mwa ******
 
Back
Top Bottom