Mawaziri wanane watakiwa kung'oka...!

Mawaziri wanane watakiwa kung'oka...!

Haiingii akilini hata kidogo sheria ichukue mkondo wake wapelekwe mahakamani na wafilisiwe na hata wengineo kama rostam na n.k.
 
Wakijiuzulu wakamtwe na washitakiwe wafilisiwe kabisa hapo itakuwa vizuri.Wakijiuzulu na chapaa ipo mfukoni hawatajuta
 
zitto huyu ambaye akiutakaga urais mnasema anatumiwa na ccm, leo mnamuona chadema safi,sio kibaraka wa ccm tena,haya bwana siye yetu macho,lakini kijana anatumia jasho lake jingi sana kuibeba chadema ila linapokuja suala la dini yake na mkoa atokao,anatengwa na kuwekwa mbali na mafanikio ya chama
Chadema ni kama barca ,wanacheza wote....total football....wanakaba wote,wanapanda,wanashambulia wote .....mmoja anapewa pasi anafunga .....wote wanarudi kati...huo ndio msemo wao......
 
hata hao saba wakijiuzulu ni hatua mbele, kwa kuwa Rais atabidi kufanya mbadikliko katika baraza la mawaziri kujaza hizi nafasi, wakati wa kufanya mabadiliko tutapima busara yake, je ataendelea na akina mwanri? kama jibu ni ndiyo basi tutajua tatizo ni yeye hivyo next move ni yeye na prime minister wake
 
Afate nyayo za wenzake walioamua kuwajibika kwa maslahi ya umma.
 
Uongozi wa jk watia aibu kabisa kwa madudu na kuvunjwa kwa mabaraza la mawaziri. Ni historia. Na kura za zitto mpaka sasa 74.
 
CCM bado inapendwa na inahitajiwa sana na watz..na mpaka sasa hamna chama mbdala au chenye nguvu kama CCM. Vyama vyetu vya upinzani ni waganga njaa tu.

CCM mtaji wake ni wa wajinga na sasa mtaji umepungua manake watu wamejanjaruka. mtabaki na wimbo huo huo mnapendwa wakati tayari matanga yameandaliwa.
 
Kati ya mawaziri saba waliojiudhuru (Ikumbukwe kwamba Mkullo yeye ndo kabisa hana cha msalia mtume, huko alipo alishafukuzwa tayari); hivyo basi bado kuna list ya mawaziri wengine ambao pia imewapasa wajiudhuru;
inaonekana hawa wanajiudhuru kutokana na ripoti ya CAG.
HATAHIVYO wapo ambao hawapo katika ripoti hiyo ambao aidha ni wabadhirifu kimazingira/kiuhalisia au ni watendaji dhaifu au hawazimudu ofisi zao.

Natoa wito kwao pia wanapaswa wajiudhuru kwa hiyari yao, la kama si hivyo ni sharti wapewe shinikizo kujiudhuru au mkondo wa uwasilishaji wa kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu, iwasilishwe kwa ajili yao.

mawaziri hao ni kama ifuatavyo
1. William Ngeleja na naibu wake Kigoma Malima
2. Shukuru Kawambwa
3. Celina Kombani na Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
4. Mawaziri wa Mambo ya ndani na Usalama wa Raia; Nahodha na Kaghasheski, waziri wa usingizi nk.

Kwangu mimi hao wanatuhuma na wamekosa uwajibikaji, na wanatakiwa wajiudhuru ama kwa kupenda kwao au kwa shinikizo letu watanzania au la wabunge chini ya hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu.

wengine ambao wapowapo tu ni kama mawaziri wa kilimo na chakula, maji na umwagiliaji, utumishi wa umma nk.

huu ni mtazamo wangu, naomba kuwasilisha.
 
HATIMAYE mawaziri saba kati ya nane wakiwemo wanaokabiliwa na tuhuma za ubadhirifu, wamekubali kuandika barua za kujiuzulu wenyewe kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kukinusuru Chama cha Mapinduzi (CCM).
Habari za kuaminika kutoka mjini Dodoma zimesema kuwa mawazirihao, walilazimishwa kujiuzulu katika kikao cha dharura kilichokuwa chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kilichofanyika mara tu baada ya kumalizika kwa kikao chaBunge.
Taarifa zimewataja waliokubali kujiuzulu kuwa ni pamoja na Waziriwa Viwanda na Biashara, Cyril Chami;
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika;
Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu; na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.
Wengine wanaodaiwa kujiuzulu ni:
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja;
Naibu Waziri wa Afya, Lucy Nkya;
na Naibu Waziri wa Viwanda, Lazaro Nyarandu.
Hata hivyo, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, ambaye alishambuliwa vikali kwa kuitwa kinara wa ufujaji, hakuwepo katika kikao hicho kwa madai kuwa yuko nje ya nchi, anasubiriwa aungane na wenzake kuachia ngazi.
Kujiuzulu kwa mawaziri hao kumekuja baada ya kuzuka kwa mjadala mzito ndani ya Bunge kwa siku mbili mfululizo kuhusiana na tuhuma za ufujaji wa kutisha wa fedha za umma, kiasi chakusababisha kuwepo kwaazimio la kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
 
Kwanza ni kosa kubwa kuwaaacha hao wezi, wahujumu uchumi, wauaji wakilanda landa mtaani, wanaweza kuanza kufanya fitina za kuwamaliza wabunge waliotoa hoja. Wakamatwe haraka mara tu baada ya kutangazwa kuachia ngazi na kama CCM wako serious, wawavue ubunge pia kwani wananchi hatuna imani nao.
 
Japo wao wanaita kuinusuru ccm, lakini ccm hainusuriki kwakuwa kifo chake kina baraka zote za Mungu.

Sera yao kubwa ni kufanya madudu ili wafukie madudu kwa hiyo watafanya madudu tu. Tunajua sasa hivi watatoka wakisema tumetubutu, tumeweza na tunasonga mbele.

Baada ya siku kadhaa yataibuka mengine na wataficha nyuso zao kwa aibu kubwa. Mfano mkubwa tulio nao ni pale walipokuja na hoja ya kujivua gamba. Nape na Mkuchika walizunguka hapa na pale wakipata mapokezi. Hata miezi 6 haikupita gari lao la kujivua gamba likakongoroka.
 
Hii nchi ishanishinda. Yasije yakawa yale ya LIYUMBA ya kufungwa miaka miwili then anatoka na kuendeleza maisha!
 
HATIMAYE mawaziri saba kati ya nane wakiwemo wanaokabiliwa na tuhuma za ubadhirifu, wamekubali kuandika barua za kujiuzulu wenyewe kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kukinusuru Chama cha Mapinduzi (CCM).
Habari za kuaminika kutoka mjini Dodoma zimesema kuwa mawazirihao, walilazimishwa kujiuzulu katika kikao cha dharura kilichokuwa chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kilichofanyika mara tu baada ya kumalizika kwa kikao chaBunge.
Taarifa zimewataja waliokubali kujiuzulu kuwa ni pamoja na Waziriwa Viwanda na Biashara, Cyril Chami;
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika;
Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu; na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.
Wengine wanaodaiwa kujiuzulu ni:
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja;
Naibu Waziri wa Afya, Lucy Nkya;
na Naibu Waziri wa Viwanda, Lazaro Nyarandu.
Hata hivyo, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, ambaye alishambuliwa vikali kwa kuitwa kinara wa ufujaji, hakuwepo katika kikao hicho kwa madai kuwa yuko nje ya nchi, anasubiriwa aungane na wenzake kuachia ngazi.
Kujiuzulu kwa mawaziri hao kumekuja baada ya kuzuka kwa mjadala mzito ndani ya Bunge kwa siku mbili mfululizo kuhusiana na tuhuma za ufujaji wa kutisha wa fedha za umma, kiasi chakusababisha kuwepo kwaazimio la kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Kujiuzulu pekee hakutoshi kwani wanastahili kunyongwa publically kwa ufisadi wao wa kutisha.
 
Tujiulize. Kama Raisi
anabakia kuwa yule yule,
Waziri Mkuu yule yule,
Bunge lile lile, Spika yule
yule na wote hao ni wa
chama kile kile, kitu gani
kitazuia vitendo vile vile
kutoka kwa watu wa
chama kile kile chenye sifa
zile zile na historia ileile
visiendelee?
Dawa sio kujiuzulu peke
yake. Wafilisiwe mali zao
kurejesha fedha zote
zilizopotea halafu
wakaionje rumande.
Haiwezekani wezi wa kuku
wataabike magerezani
huku wakifanyishwa kazi
ngumu halafu wabadhirifu
waendele kudunda mitaani.
 
Japo wao wanaita kuinusuru ccm, lakini ccm hainusuriki kwakuwa kifo chake kina baraka zote za Mungu.

Mkuu Yeriko, hatukubaliani na upuuzi wa kuinusuru ccm kwa lao lengo la kuendeleza udokozi wa kitoweo chote cha nchi na kutuachia mfumuko wa bei za kutisha eti ndo maisha bora kwa watz.
 
Wameshakula vyakotosha waachie ngaz tu sema sheria yetu ina loopholes za kutosha kudil na watu kama hawa'
 
Back
Top Bottom