Mawaziri wakutwa gesti

Andrew Nyerere

JF-Expert Member
Nov 10, 2008
3,007
2,429
Gazeti la Sani laandika kwamba Mawaziri wawili, Sophia Simba, na Shamsa Mwanguga wamekutwa gesti ya Mikumi Inn, Magomeni, Jumapili iliyopita.

Wamepiga picha ya magari yao, STK 4472, na T274AOD.

Ulikuwa ni mkutano wa akina mama tisa au kumi, wakiongozwa na hawa Mawaziri wawili. Haijulikani walikuwa wanaongea nini. Ni mkutano ambao ulianza saa tano asubuhi mpaka saa moja jioni.

Ilikuwa tu ni kikao cha siri. Walionekana wakiwa na mafaili mengi. Hakuna habari zozote kama walikuwepo pale kujirusha,ingawa walionekana wananchi wengi wengine,wakiwa katika pilika za kujirusha,kama kawaida ya Guest house,lakini hii haikuwasumbua hawa akina mama.

Mwandishi wa habari zile ameshangaa sana kwamba hawa Mawaziri hawakwenda kufanya mazungumzo,pahali ambapo ni more salubrious.
 
walikuwa wanafanya huo mkutano chumbani?, ama walikuwa na mkutano sehemu za vinywaji, hapa namaanisha sehemu wazi?, jee hilo Gazeti halikuwahoji wamiliki wa hiyo Gesti walikuwa wanafanya nini manake wamiliki watajua, ama kuwahoji hao mawaziri. Sababu kuwa Gesti si kosa kwa Waziri.
 
Si unajuwa mh. Sofia anatafuta cheo kingine ili azidi kuendelea kumchanganya yule mtoto aliyemwuliza Lowasa juu ya mantiki ya maana ya methani -mshika mawili mojoja humponyoka-ambayo hufundishwa mashuleni na hali halisi katika maisha. Wakati mwingine watoto wanasumbuka sana kuweka yale wayasomayo katika halihalisi ya kimaisha.

Yawezakuwa wapigakura walikuwepo maeneo hayo ya gesti ndiyo maana na hao waheshimiwa wakawepo pale
 
Gari la serikali jumapili?

Inawezekana,ila kwa kibali maalum cha kukupa ruksa ya kulitumia kwa siku hiyo.
Ila hii habari ningeomba wahojiwe wamiliki wa hiyo Guest House ili watujuze nini hasa kilochopelekea hawa mawaziri kuwepo pale.
 
Hizi picha nimeipata kule anakopendelea Kibunango na baadhi wachache sana sithemi mnapapiga marufuku sana hapa hiyo sehemu mtakuwa mnajua ni wapi.....
simba.jpg
simba2.jpg
 
Inawezekana,ila kwa kibali maalum cha kukupa ruksa ya kulitumia kwa siku hiyo.
Ila hii habari ningeomba wahojiwe wamiliki wa hiyo Guest House ili watujuze nini hasa kilochopelekea hawa mawaziri kuwepo pale.

Kwa nini wasiulizwe mawaziri wenyewe?
 
ni T274AQD,nafikiri hii ni mambo ya kampeni ya UWT.wamechagua mahali ambapo wanafikiri kuna privacy na watu wa kambi ya Mama Janeth Kahama wasingeweza kupenyeza kirahisi.Inaweza kuwa sababu ya kufanyia kikao chao Mikumi Inn
 
Ifike mahali hao Sani na wadaku wengine waje na picha za mabaki ya vyakula vya mawaziri
 
Nakubali kwamba wakina mama kuwa guest si makosa.Ninachokataa ni wakina mama waliopewa dhamana ya kuliongoza taifa kuwa guest.Niseme wazi,sio heshima kwa kiongozi mkubwa wa serikali kama Waziri kukutwa guest.Kuna picha mbovu na nyingi ambazo zinaweza kuchorwa,na hatima ya picha zote hizo ni kuiaibisha serikali na taifa kwa ujumla.Waziri ni mtu aliyepewa dhamana kubwa na serikali,kwa hiyo sio vema kutembea hovyo hovyo.Ni lazima ajiheshimu.
 
hii inaaibisha taifa ina maana hicho chama au ntubani kwao hakuna maeneo ya vikao macho yao yaliona hiyo guest watu hawa ukiwapa uongozi ujue hawataona matatizo yenu watakachoona ni mambo yao wanainchi tafakari chukua tahadhari hawa watu waonywe mara moja du........inachosha akili inashangaza acha nipumzike.
 
Kwani huko kwenye ma guest houses ni shughuli moja tu inayoweza kufanyika? Jamani, huenda ulikua mkutano wa faragha sana. Hawa waandishi wa habari hawajawatendea haki hawa wakina mama. Mbona mawaziri wengi tu wakiume wanaendaga kwenye ma guest houses na hawa waandiki? Fair play, please!!!
 
Back
Top Bottom