Inabidi tuwe waangalifu kwenye msamiati. Kughushi cheti kinachosema una sifa fulani wakati huna ni kosa la jinai. Naamini tatizo tulilonalo dhidi ya hawa Mwaziri wetu na Wahadhiri wa Mzumbe si la kughushi.
Accreditation is a relative term. Different bodies have different sets of accredited universities. Labda tunazungumzia accreditation ya TUC. Sasa hao TUC wameshasema shule zipi ndio accredited?
Sidhani kwamba tatizo tulilonalo na hawa vihiyo wetu ni la kusoma kwenye vyuo ambavyo sio accredited. Ni tatizo la kujipatia cheti cha kusema una digrii fulani kwa kununua hicho cheti, na kwa kutosoma kwa kiwango ambacho angalau kinakaribia kweli kilele hicho cha elimu .
Nafahamu, kwa karibu, watu wawili waliojipatia PhD kwa njia hii feki. Wa kwanza alikuwa na MSc ya Mahesabu. Aliwasiliana na PWU, na baada ya kuandikiana kwa miezi kidogo, na bila kusoma Mehesabu zaidi, aliwatumia fedha walizotaka, nao wakamtumia "cheti cha PhD" ya Mahesabu toka PWU. Ngazi yake ya Mahesabu ilibaki pale pale kwenye MSc yake, lakini tangu siko hiyo alidai ana PhD.
Wa pili ana MBA. Anafanyakazi kwenye cho kikuu cha binafsi. Miaka michache iliypita chuo hicho kiliamua ukiwaandikia ukajieleza uzoefu wako na kulipa gharama zinazotakiwa basi wataangalia kama unastahili PhD. Alifanya hivyo na wakampa PhD (ya uzoevu wake). Hakusoma zaidi. Hakuna cha thesis wala cha nini.
Mimi najua mtu yoyote mwenye PhD ya PWU ni kihiyo wa kununua digrii.
Sasa mwajiri wa kihiyo aidha ni kihiyo (kwa kushindwa kugundua vyeti feki) au ni mshirika wa makusudi katika kosa kubwa. Inabidi serikali ingoe vihiyo wote kwenye ajira yake. La sivyo tutajenga uzoefu mbaya.