Mpaka Kesho Sijui Niliachwa Achwaje huko
Saa ya ukutani ilikuwa ikigonga tiki-taka, kila sekunde ikionekana kama pigo la nyundo moyoni mwangu.
Nilikuwa nimekaa kwenye kochi letu lile lile la rangi ya kijivu, nikiwa nimeshika simu yangu ambayo dakika tano zilizopita ilikuwa imejaa msg za mahaba, lakini sasa ilikuwa imepooza kama barafu.
"Samahani, siwezi kuendelea nawe tena!. Nakutakia kila la kheri katika maishq yako," huo ndio ulikuwa ujumbe wa mwisho kutoka kwake.
Hakuna salamu, hakuna maelezo, na mbaya zaidi—hakuna kosa. Tulikuwa tumetoka kula chakula cha jioni saa mbili zilizopita.
Tulicheka, tulipanga kuhusu harusi yetu ya mwakani, na hata alinibusu paji la uso akiniambia, "Wewe ndiye mwanaume wa maisha yangu."
Nilijaribu kupiga simu.
“Mteja unayempigia hapatikani kwa sasa...” Sauti ile ya upole ya mhudumu wa mtandao ilikuwa ikinichoma kama kisu.
Nilijaribu kutuma ujumbe wa WhatsApp; tiki moja ya kijivu iligoma kugeuka kuwa mbili. Alikuwa ameshaniblochi (block).
Nilikumbuka kila kitu. Je, kuna neno nilisema vibaya wakati wa chakula? Hapana, alikuwa akitabasamu muda wote
Je, kuna mtu alimpigia simu? Hapana, simu yake ilikuwa mezani muda wote na hatukuwa na siri.
Nilikesha usiku kucha (kama leo

) nikiangalia mlango, nikidhani labda ni mchezo au "suprise" fulani. Lakini asubuhi ilifika, jua likachomoza, na hakuonekana.
Nilienda kazini kwake, nikaambiwa ameacha kazi wiki mbili zilizopita—kitu ambacho hakuwahi kuniambia. Nilienda nyumbani kwake, nikakuta kumeingia mpangaji mpya.
Ni miaka 20 sasa imepita. Maisha yanaendelea, nimekutana na watu wengi, lakini kila nikijitazama kwenye kioo, swali lile lile linanirudia: Hivi niliachwa achwaje?
Bila ugomvi, bila kelele, bila hata nafasi ya kusema "kwaheri."
View attachment 3572833